Rais Magufuli awafariji wafiwa Chato, awataka wadumishe mshikamano katika kipindi hiki kigumu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,229
2,000
Mzee Admirabilis Mbabe Manyama alikuwa ni mzee mwenye umri wa miaka 82 ambaye alikuwa ni mmoja wa wazee maarufu na wanaheshimika kutokana na hekima na busara zake, Chato Mkoani Geita.

Mzee Admirabilis alikuwa jirani na pia rafiki wa karibu na Baba wa Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa ni miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.

Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.

''Unapotokea msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee''

Kwa upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.

Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.

Rais Magufuli yuko Chato kwa sherehe ya Krismasi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akielekea msibani

Rais Magufuli akisalimia na wananchi mbali mbali wakati akielekea kwenye msiba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita.

Mdogo wa Marehemu, Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama.

Rais akiagana na ndugu na jamaa wa Marehemu baada ya kuhudhuria msiba.

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.

Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.

''Unapotokea msiba kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za uhai wa mzee''

Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule wakati akisoma.

Kwa upande wake Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.

Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato, Geita.

29 Desemba, 20
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom