Rais Magufuli awaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza sakata la mchanga wa migodini

Mkataba ambao watangulizi wake waliingia na hayo makampuni unasemaje? Hata kama ni mkataba wa kutuibia madini yetu, lakini unasemaje?

Ukishajiuliza hayo maswali utagundua kwamba approach anayotumia mkuu siyo sahihi. Angeenda kwenye mkataba kisha akakaa nao mezani na kuona namna ya kubadili mkataba
Aende kwenye mkataba tena wakati tunataka kujua mchanga unaondoka na madini kiasi gani! Mikataba ni baada ya uchunguzi huo, wataangalia pia mikataba.
 
Mkuu tatizo sio kiasi gani cha madini kilichopo kwenye mchanga tatizo ni mikataba ya serikali na hawa wawekezaji, kama unakumbuka kuna waziri wa madini wa serikali ya awamu ya nne ilisemekana alisaini mikataba na hawa wawekezaji akiwa hotelini huko ulaya. Bunge lilimuomba Proff. Muhongo aweke wazi mikataba ya Gesi lakini alikataa. Mkuu kama wewe uko serious ni wazi upeleke bungeni mikataba yote iliyosainiwa ili bunge lijadili kwa makini what went wrong kwenye masuala haya. Watanzania watakuona wewe mbaya lakini kumbe umerithi uozo mkubwa katika mikataba mikubwa. Ni aibu kubwa sana kwa nchi kama Tanzania kutofaidika na maliasili yao wakati nchi za kiaarabu wakati wanagundua mafuta asilimia 95 walikuwa hawakwenda shule lakini waliweka mikataba mizuri na makampuni yaliyokwenda kuchimba mafuta ndio maana leo hii wanakula matunda ya mafuta hayo.
Sisi hapa Tanzania utafikiri tumelaaniwa leo gesi inachimbwa hapa hapa nchini kwetu lakini tunauziwa na hayo makampuni yanayochimba utafikiri tumeagiza gesi kutoka Russia.
 
Magufuli anajua
Ndugai anajua
Muhongo anajua

Wote hawa wanajua mchezo mzima ulivyo wasitake kuumiza vichwa vyetu, kama hawana kazi ni bora wakae maofisi wanywe juice zao kwa pipi!
 
Tatizo la bwana huyu atawaapisha , alafu atawaambia kile anachotaka kiandikwe badala ya kuacha wafanye kazi kwa mujibu wa utaratibu na si maagizo yanayo zaa maigizo
Ni vyema ahache kuingilia maamuzi ya wanataaluma refer to Nape ripot ambayo haikumfurahisha.
 
Shida ni hiyo mikataba. Na huyu jamaa yetu ni expert kweli kwenye kuikiuka na mwishowe kuishia kulipishwa. Hivyo vikodi vyote alivokusanya naona anatafutia pa kuvipeleka.









Amini nakwambia
 
Huyu si alikuwa mbunge,tena ndani ya jimbo lililoko kanda ya madini 20years ,hata siku moja hajawahi kunyakua kinywa kukemea mikataba mibovu na hajawahi hata siku moja kusema hapana jambo lililokuwa na maslahi kwa CCM, leo kautoa wapi uzalendo huu?
Au kwakuwa sasa hivi ulaji hachotewi na mtu bali anajichotea?
Kasahau hasara aliyoipatia taifa kupitia samaki wale waliokula wafungwa na wanafunzi?
Nakumbuka huyu aliwafukuza kazi my fellow workers TEMESA kama 20 hivi kwa siku moja kwa maslahi yake binafsi na waliposhtaki serikali iliwalipa fedha nyingi.
Watanzania ,hatuna pesa ya kuwalipa ACCACIA, wait &watch this bad game.
 
Kila la heri wataalam wetu, mtuletee mrejesho wa kweli tujue tumekuwa tukipigwa ama lah!
Ikiwa tumekuwa tunapigwa, kwakweli mh rais itabidi "afukue makaburi" kwa yeyote aliesababisha hali hiyo.
Likiwemo kaburi lake.
 
Ndugu wewe ndio hujaelewa...
Mpaka hapo hajavunja mkataba Bali amesitisha usafirishaji wa huo mchanga on grounds that,Wazungu wamekuwa wakitudanganya kuhusu kiwango cha Dhahabu kilichomo kwenye mchanga huo. Hiyo tume imeundwa sio kuangalia mkataba isipokuwa kupima kiwango cha dhahabu.
Kwa karibu miaka ishirini wamekuwa wakidai wanasafirisha Shaba na fedha na kiwango kidogo sana cha Dhahabu 0.02-0.05g/t ya mchanga baada ya kuwa wamechimba.
Ukisoma taarifa ya ACACIA ndio utashtuka sana.
Leo ndio wanatangaza kuwa 30% ya mapato ya kampuni wanapata kwenye usafirishaji.
Kumbuka wamesema ktk madini wanayochimba 95% ni dhahabu na 5% ndio Shaba na fedha na kadhalika. Sasa jiulize iweje 5% ya madini wanayochimba ichangie 30% ya mapato!??
Kuna Maelezo kwamba 70% ktk ile 95% yavDhahabu hupatikana mgodini na 25% hupatikana baada ya kusafirisha mchanga
Sasa jiulize 25% ndio 0.02-0.05gm/t.
Kama haitoshi wanadai kupoteza $1,000,000/= kwa siku ambayo ni sawa na billion 2.2/day!!!!
Hata wakilipa kodi ya 3% ni zaidi ya 66million kwa siku kwa mchanga pekee. Kwa mwaka ni kiasi gani?
Wachache watakuelewa wengi wetu tumebaki kupinga tu mkuu. Wakati kipindi cha nyuma walikuwa wanalalamika serikali haijachukua hatua.
 
Mkataba ambao watangulizi wake waliingia na hayo makampuni unasemaje? Hata kama ni mkataba wa kutuibia madini yetu, lakini unasemaje?

Ukishajiuliza hayo maswali utagundua kwamba approach anayotumia mkuu siyo sahihi. Angeenda kwenye mkataba kisha akakaa nao mezani na kuona namna ya kubadili mkataba
Wee jambazi utakuwa unanufaika na huu wizi
 
Back
Top Bottom