Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Mbunge anapewa fungu gani la kutumia kutatua matatizo yote ya wananchi. Bure kabisa!Mh.Rais kasimamishwa na watu wakati akielekea ziarani Morogoro, wananchi hao wamemsimamisha huku wakiwa na mabango yanayoonyesha mahitaji na matatizo yao, miongon mwa kero ni kutosajiliwa kwa shule ya kijiji ambayo ipo darasa la tano.
Katika kujibu kero zao ametoa kiasi cha milioni tatu na kuagiza shule isajiliwe ikiwezekana mwezi huu.
Katika hali ya kushangaza Mh.Rais wakati akijibu swala la umeme kwanza ameuliza mbunge wa eneo husika na baada ya kujibiwa kuwa ni mpinzani.' naye kawajibu ''Mjifunze kuchagua'' Magufuli
Zile kauli za maendeleo hayana vyama zinakuwa na maana gani!??