Rais Magufuli atweet asubuhi hii kuhusu Mradi mkubwa

mkuu mbona unajichanganya! Mkataba umeandikwa kwamba TMAA watapima kila mchanga unaosafirishwa na kutoa concentration ya madini yaliyomo ili mrabaha ulipwe. sasa hiyo habari ya 4kg unaitoa wapi mkuu?? ingekuwa hivo kusingekuwa na sababu ya TMAA kuchukua sampuli kwa kila batch ya mchanga.

nakubaliana na wewe kwamba CEO wa TMAA ni mteule wa raisi na anapaswa kuwajibika kwa makosa yake ya kutoa concentration za uongo (kama kweli majibu ya tume ni sahihi), hata bila kumhusisha prof muhongo.

Lakin usitulishe matango poli eti mkataba umesainiwa kwamba kuna 4kg za dhahabu kila contena, huo ni uongo wa kiwango cha lami.
Nakubaliana na sahihisho lako. Nimenukuu vibaya. Hoja ambayo bado ni kuwa Muhongo ni mbuzi wa kafara
 
Asome vizuri hiyo mikataba ya bomba na iwekwe hadharani tusome wote tujirizishe
Sio kuisaini kwa mbwembwe badaye tunaanza kulialia tunaibiwa
kwa kweli isije kuwa faida yetu ni bomba tu kupita vingine wanafaidi wengine.
 
Nakubaliana na sahihisho lako. Nimenukuu vibaya. Hoja ambayo bado ni kuwa Muhongo ni mbuzi wa kafara
mimi naamini muhongo hauhusiki na upigaji huu.. lakin kumbuka vile ni vyeo vya kuteuliwa na raisi. hata kama huna kosa lolote, anaweza kukuondoa na kuweka amtakaye. kama alivyokuteua bila kulazimishwa na mtu, anaweza kukuondoa siku yoyote akiamua.

Muache prof apumzike tu, waje wengine waendeleze kazi. Ila muhongo is a good person. si mpiga madili.
 
Hongera Rais John Pombe Magufuli kwa kufanikiwa kuishawishi Uganda hadi ikakubali ujenzi wa mradi huu mzuri kufanyika nchini kwetu Tanzania.
Watanzania tuanze kujipanga ili kuitumia vyema fulsa hii ya kiuchumi.
Kazi kwetu.
tujipange kama tulivyojipanga bomba la gesi mtwara.
 
Habari nyingine mbaya sana kwa chadema na wenzao wasio tutakia mema.Si ajabu wameitana Dodoma watapinga pia na huu mradi kwa kusema utaharibu mazingira
 
Bravo JPM. Go go go. Maana hapa ni mtandaoni, sitegemei kuona waliothirika na mabadiliko ya route ya Mkongo au waliothiriwa na utenguaji wa nafasi waje hapa waseme vitu positive juu ya utendaji wa JPM na kasi anayoifanya kuhakikisha nchi inasonga mbele. Kama watakuja hapa JF kumsifia JPM nitawashangaa kwelikweli.
Hivyo, JPM Kanyaga twende baba, timiza ndoto zako juu ya Tanzania uitakayo. Kelele za mlango hazizuii mwenye nyumba kupiga usingizi.
 
mimi naamini muhongo hauhusiki na upigaji huu.. lakin kumbuka vile ni vyeo vya kuteuliwa na raisi. hata kama huna kosa lolote, anaweza kukuondoa na kuweka amtakaye. kama alivyokuteua bila kulazimishwa na mtu, anaweza kukuondoa siku yoyote akiamua.

Muache prof apumzike tu, waje wengine waendeleze kazi. Ila muhongo is a good person. si mpiga madili.
Kwa mantiki hiyo Prof muhongo asingeondolewa kwa sababu za matokeo Tume.
Kwa vile Rais anayo mamlaka ya kuteua na kutengua basi angefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na kumtengua Prof kwa heshima tu na si kwa kumhusisha na hii kashfa.
Kwa nini Naibu Waziri naye asitenguliwe maana wale walikuwa ni team moja. Mbaya zaidi Naibu Waziri ndiye aliyekuwa Mwanasheria wa Wizara kwa Kipindi ambacho mikataba ilikuwa inafanyika? Ukiitaka kusafisha nyuma unafagia vyumba vyote.
 
Hachelew kuja kuundia time huo mrad na kumuwajibisha waziri

Aiseeeh,
Imebidi nicheke .

Tume kwenye hizi project kubwa huwa haiepukiki.

Hebu, Mtafute mtu aliyesoma project management atakuelewesha vizuri kabisa na utaelewa kuwa mtu kuwajibishwa kwenye projects ni jambo la kawaida sana kwa tuliozoea kufanya kazi kama hizo za projects mbalimbali.

Kwa hiyo, watakao pewa kazi hiyo wawe makini na wafanye kwa umakini na tuachane na ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom