Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Igunga kwa kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata taratibu

Safi Sana Kiongozi anaedhulumu ardhi za wananchi, au anaepanga kudhulumu kwa visingizio flani ,hamfai kabisa, Sasa mh ,kaa Kama week moja ,Muondoe na Lukuvi, maana juzi alitangaza kuanza chukua ardhi za viwanja vya watu, maana lengo la watu wa aina hii nikuwatia umaskini watz
 
Lissu aliwatahadharisha mapema kuwa wakimaliza kuwashughulikia wapinzani wao watatafunana wenyewe kwa wenyewe. Sitashangaa siku moja kusikia Jiwe kampa talaka mama Jesca na kuamuru afungwe kwani kahujumu ndoa. Huku Majaliwa akitumbuliwa na kushtakiwa kala hela ya korosho na DPP kapotea hajulikani alipo baada ya wasio julikana kuondoka naye.
Maajabu makubwa mengi yaja tutayashuhudia.
 
Mliwashughulikia wapinzani ili kulinda nafasi zenu, huu ni wakati na nyinyi sasa kushughulikiwa, au nasema uongo ndugu zangu.
Kuiba ni suala jingine, haina maana ukimshughulikia mpinzani unakuwa umepata ruhusa ya kuiba maduhuri ya serikali.
 
Huu upuuzi sijuhi utaisha lini,tumbua tumbua hii,imekuwa too much,Haina tija,vyumba vya madarasa havitoshi,walimu hawaajiriki,ajira hakuna,sekta binafsi ipo hoi,mikopo ya Elimu ya juu shida,unakopeshwa,unasema,ukija kitaa,hakuna ajira,tunamatatizo makubwa sana,lakini serikali hii kila kiongozi anatafuta Kiki kwa ishu nyepesi nyepesi tu,PM katumbua watu Jana Bandarini,leo Jiwe nae anatumbua,harafu anaona inafanya jambo la maana sana linaloleta tija kwa nchi,hiyo ishu ya DAS ni level ya Waziri Tamisemi.
Kwanini hamfuti vyeo vya wakuu wa wilaya,mikoa,kwanini tutumie V8 na sio Rav 4 serikalini,
Kuna haja gani ya kuwalipa wabunge kiinua mgongo 200M,kuna tija gani kuwa na wabunge 365!!kwani lazima,huo ulazima unatoka wapi!kwanini tusiwe na wabunge 50,ndani ya mkoa,Kuna
RC,DC,RAS,DAS,Mkuu wa polisi,Mganga mkuu,Mbunge,madiwani,Hawa wote wanini!?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo Desemba 28, 2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwaa ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

JPM amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.

Usanii tu huo
 
Siku zinaenda kasi kuliko mzunguko wa dunia -Usiniulize kivipi.
Nimekuelewa sana mkuu, Matunda ya nchi ya chama kimoja.

Kutoka kuiba kura na kusimamia wapinzani wasitangazwe, na sasa anaambiwa utumishi wake haumridhishi aliemteua.
Labda Alitakiwa ATEKE na KUUA wapinzani.
 
KUNA MAKALA JANA NIMESOMA HUMU YA MKUU MMOJA WA MKOA ALIUWA NA MKULIMA KWA SABABU YA DHARAU YAKE NA KUTAKA KUMPORA MKULIMA ARDHI
 
Back
Top Bottom