Rais Magufuli atangaza siku 3 za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Robert Mugabe

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais Magufuli ametangaza siku 3 za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Baba wa Taifa na aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe kilichotokea leo Nchini Singapore

Katika siku hizo tatu za maombolezo zinazoanza leo Septemba 06 hadi Septemba 08, 2019 bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti

Leo asubuhi Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, familia ya Robert Mugabe, Wananchi wa Zimbabwe, Waafrika na wote walioguswa na msiba

Aidha, Rais Magufuli amesema Robert Mugabe aliipenda Tanzania, alijenga uhusiano na ushirikiano wa karibu, kindugu na kirafiki tangu enzi za uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere

E27FE7EB-08F9-4011-9CA0-A55FA0A9A24E.jpeg
 
Hii ina maana hakuna kwenda kazini siku ya jumatatu au ni maombolezo ya bendera kupepea nusu mlingoti tu?
 
Mugabe ni kati ya viongozi wabaya Africa waliowahi kutokea. Tunapenda kupongeza watu sana kwa kumbambana na mabeberu. Zimbabwe walioumia ni wananchi. Yaani maendeleo ya Zimbabwe badala ya kukua yame didimia kwasababu ya Mugabe. Tusisingizie wazungu kwenye kila kitu Wazimbabwe wamehamia SA wakati walikuwa na nchi nzuri sana.
 
Wenye akili hapa tunaelewa hivi "JPM kafanya hivi kutuma meseji kwa mabeberu kuwa kiboko yenu amefariki kwa heshima yake mi nabeba mikoba yake na mtakunya kwa sababu yule alikuwa mzee mimi kijana" NILICHOELEWA MIMI PIA KATUMIA LOOPHOLE YA KESHO NA KESHO KUTWA NI WEEK END SO KIMAHESABU YA MINUS NI KUWA KATOA SIKU MOJA TU YA MAPUMZIKO.
Mugabe ni kati ya viongozi wabaya Africa waliowahi kutokea. Tunapenda kupongeza watu sana kwa kumbambana na mabeberu. Zimbabwe walioumia ni wananchi. Yaani maendeleo ya Zimbabwe badala ya kukua yame didimia kwasababu ya Mugabe. Tusisingizie wazungu kwenye kila kitu Wazimbabwe wamehamia SA wakati walikuwa na nchi nzuri sana.
 
Kwanzq Mugabe hakuwa rais mstaafu wa Zimbabwe. Aliondolewa katika mapinduzi ya kijeshi na kulazimishwa kujiuzulu.

Pili kila mpenda demokrasia na maendeleo wa Afrika anajua mabaya yote Bw Robert Mugabe aliyoifanyia nchi ya Zimbabwe.

Ila dhambi ambayo haitasameheka kirahisi ni kuendesha mauaji ya halaiki huko Matebeland, iliyokuwa ngome ya hasimu wake Joshua Nkomo.

Madhambi mengine ni pamoja na kuua na kuwaita vilema wananchi waliokuwa wafuasi wa upinzani, kuua uchumi wa nchi, kuvuruga demokrasia na chaguzi mbalimbali, kupora rasilimali za nchi na kujaribu kuirithisha nchi kwa mke wake dis-Grace Mugabe.

Mimi kamwe sitapoteza muda kusikitika kwa ajili ya huyu Bwana Mugabe. Ila namwombea Mungu amsamehe dhambi zake na ampumzishe. Amen

RIP Mugabe.
 
Mugabe alikua Icon ya mtu mweusi aishie Africa. Kwa Sasa amebaki Magu. Kinacho sikitisha ni kua watu wa ujasiri huu wanatokea mmoja mmoja kwenye bara hili lililokua undermined kuliko mabara yote kwenye uso wa dunia.
Nashauri kwa kumuenzi shujaa wetu mzee huyu kifunguliwe chuo kitakacho fundisha Nia Ovu na tricks wazitumiazo mabeberu kuendelea kui- undermine Africa - kiwe research based ili kusaidia serikali za Africa. Na propose Mwenyekiti wa board ya chuo hicho awe JPM, VC awe Prof P.L.O. wa Kenya Raisi wa Tanzania niwe Mimi BIGGAG ili ku- facilitate polical will among African countries kwa maslahi mapana ya bara la Africa.

Rip Nkuruma, P.lumumba and now Mugabe. Wazee wangu Nyerere na Mandela sijawasahau Ila mlikua too fair na Hawa jamaa Ila nawaelewa sana ilikua muhimu kuvusha kizazi kilichokua extremely ignorant kwa Wakati huo.
 
Back
Top Bottom