Rais Magufuli atangaza siku 3 za maombolezo ya Kitaifa kufuatia kifo cha Robert Mugabe

Mtu mwenye roho ya korosho halafu awe dikteta! Ni lazima tutasoma sana namba. Nawashangaa sana baadhi ya watanzania wanaomsifia huyu bwana mkubwa na itikadi zake za kufungia pesa akidhani zitaongezeka.

Ajui chochote kuhusu uchumi angebakia kwenye kuhesabu kilometers za barabara ndo kwake. Ajuae uchumi hawezi somesha watu no na kuwakomoa matajiri.
 
Kwanzq Mugabe hakuwa rais mstaafu wa Zimbabwe. Aliondolewa katika mapinduzi ya kijeshi na kulazimishwa kujiuzulu.

Pili kila mpenda demokrasia na maendeleo wa Afrika anajua mabaya yote Bw Robert Mugabe aliyoifanyia nchi ya Zimbabwe.

Ila dhambi ambayo haitasameheka kirahisi ni kuendesha mauaji ya halaiki huko Matebeland, iliyokuwa ngome ya hasimu wake Joshua Nkomo.

Madhambi mengine ni pamoja na kuua na kuwaita vilema wananchi waliokuwa wafuasi wa upinzani, kuua uchumi wa nchi, kuvuruga demokrasia na chaguzi mbalimbali, kupora rasilimali za nchi na kujaribu kuirithisha nchi kwa mke wake dis-Grace Mugabe.

Mimi kamwe sitapoteza muda kusikitika kwa ajili ya huyu Bwana Mugabe. Ila namwombea Mungu amsamehe dhambi zake na ampumzishe. Amen

RIP Mugabe.
Umenisemea hapo kidogo , baadhi ya watu Ni wanafiki sana ,huwezi kumsifia Mugabe aliye wahi kuwaumiza wazimbabwe kiasi kile
 
Tija ipo ukiwatazama watanzania masikini kwa ujumla wao angalau wanafanya kilimo cha kukidhi mahitaji yao ya msingi, fikiria kama ardhi yote ingetwaliwa na wenye fedha hali ingekuwaje kwa watu masikini?
Kilimo cha kujikimu hakina tija unalima then baada ya msimu mmoja tu njaa
 
Anaenda kutana na watu aliowatesa,wabambikia kesi,filisi,aliowauwa ktk harakati zake za kuukimbiza upepo duniani.
 
Alipigania maslai yake na wahuni wenzake kama walivofanya waliojiita wapigania Uhuru wengi,kumbe walipigania maslai yao binafsi uthibitisho ni baada ya uhuru waligeuka ni matajiri wakubwa wao na familia zao huku wakiwaacha mamilioni ya Waafrica waliowasaidia kupata Uhuru kutopea kwenye Lindi LA ufukara huku wakiwauwa ,kuwateka, kuwatesa,kuwabambikia kesi Waafrica wenzao Kwa kuwatendea ukatili zaidi ya hata wakoloni. Kilichobadilika ni Rangi tu toka wakoloni weupe hadi wakoloni weusi.
 
Ameondoka kama alivo atasimama yeye kama yeye mbele ya hukumu Bila walinzi,kamati ya ufundi,pesa,hakuna wasiojulikana. alipewa kazi ya kuchunga kondoo akawaumiza kondoo.Takribani kondoo 20000 walipotea wakiwemo wandebele 2000.
 
Back
Top Bottom