Rais Magufuli ashangazwa na Mstahiki Meya wa Kinondoni Boniface Jacob kutohudhuria Biafra

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Na Kilawa the Iron

Hii imetokea mara tu baada ya mh Rais John Pombe Magufuli kumtaka mastahiki Mayor wa Kinondoni Mh Boniface Jacob.

Kutoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mpango wa usalama wa jamii katika viwanja vya Biafra.

Mh Rais ameshitushwa sana na kutokuwepo kwake mstahiki mayor mh Boniface Jacob kwenye uzinduzi huo, hali iliyomfanya kupatwa na butwaa kidogo,mh Rais akalazimika kuulizia kama yupo diwan wa eneo husika, akajitokeza kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, ilisemekan kuwa ni diwan wa CHADEMA japo alijitambulisha kwa hofu kidogo, hakuwa katika hali ya kujiamini, alifika mbele na kuishia kusema "Magufuli hoyee....." huku akiwa na na sura ya hofu kidogo.

Na baadaye Ndugu Dovutwa, akatoa salamu zake
Serikali inapaswa kujisahihisha badala ya kupatwa na butwaa.
#BRING BACK OUR DEMOCRACY(BBOD)


=========

Meya ajitetea Sababu ya kutokuhudhulia, Soma=>Meya wa Kinondoni amjibu Rais Magufuli, hakuwa na mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa Polisi
 
Leo ni siku ya uzinduzi wa usalama wa raia,na shughuri inafanyika viwanja vya biafra hapa kinondoni karibu na Morocco.mgeni rasmi ni raisi John Joseph Pombe Magufuri.kiutaratibu raisi anapokuwa eneo lolote ni lazima wawepo viongozi wote wa eneo husika(mbunge,dc.diwani n.k).sasa ajabu ni kwamba leo raisi amewaita viongozi wote na wapo kwenye ratiba lakini mbunge wa kinondoni hayupo na hata meya wa kinondoni hayupo pia na ni kutoka ukawa wote.sasa jaman hata ishu kama hizi wanaziweka kisiasa?? Kweeeli? Big up kwa diwani wa kinondoni kutoka chadema yeye alikwepo japo najua atakoma huyo
 
hahahah hapo inaonyesha wazi kuwa upinzani labda unashirikiana na majambazi na ndio maana haupendi tukio kama hili la leo. inawezekana kabisa baadhi ya majambazi ni wafadhili. hakuna maelezo mengine tunayoweza kutoa wajameni kwa sababu hata kama kuna burning issues za kisiasa, lazima kupembua matukio. tukio la leo ni la kitaifa na sio kisiasa wala kichama. tubadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…