Na Kilawa the Iron
Hii imetokea mara tu baada ya mh Rais John Pombe Magufuli kumtaka mastahiki Mayor wa Kinondoni Mh Boniface Jacob.
Kutoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mpango wa usalama wa jamii katika viwanja vya Biafra.
Mh Rais ameshitushwa sana na kutokuwepo kwake mstahiki mayor mh Boniface Jacob kwenye uzinduzi huo, hali iliyomfanya kupatwa na butwaa kidogo,mh Rais akalazimika kuulizia kama yupo diwan wa eneo husika, akajitokeza kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, ilisemekan kuwa ni diwan wa CHADEMA japo alijitambulisha kwa hofu kidogo, hakuwa katika hali ya kujiamini, alifika mbele na kuishia kusema "Magufuli hoyee....." huku akiwa na na sura ya hofu kidogo.
Na baadaye Ndugu Dovutwa, akatoa salamu zake
Serikali inapaswa kujisahihisha badala ya kupatwa na butwaa.
#BRING BACK OUR DEMOCRACY(BBOD)
Mleta mada ni kana kwamba umeangalia hiyo Taarifa pake yako,wengi tumetazama na tumepata picha tofauti...Ile ilikuwa ni gear ya JPM kumuita Madabida(Muuza ARV Fake)Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dsm aliyekuwa meza kuu.
Alimuita,lkn akashtuka kuwa kakiuka protocol kwa kutaka kumuitwa Mwenyekiti wa CCM wakati Meya anaweza kuwepo,hata ita yake ilikuwa kana kwamba hajui Meya wa K'ndoni ni nani?Maana Rais alisema hivi Meya wa Kinondoni yupo?anaitwa nani vile...Wakamwambia Jacobo,Rais akasema nani jina lake!?Maana sijui jina lake...Baadae akaita akasema Meya huko ulipo njoo hapa(Wakati ilitakiwa ajuwe kwa tukio lile Meya alipaswa kuwa HT kuliko hata Madabida)
Na ukitaka kujuwa Rais ni "mchonganishi" akasema Meya wa Kinondoni hayupo naona hachukii ujambazi na uhalifu,Akaongeza "Karibu mwenye kiti wa CCM mkoa,wewe upo hapa sababu unachukia majambazi na uhalifu"...(akasahau huyo Madabida ana tuhuma ya uhalifu ya kutuuzia ARV fake ambayo yeye JPM kakataa kulipa fidia baada yakusema kesi ya kimagumashi kwa Madabida kushinda)
Kwa aibu akasema hakuna diwani wa CHADEMA?Akapanda jamaa mmoja hivi diwani wa chadema,alipotaka kuongea KIKWETE akachomeka akamwambia "Sema Magufuli hoyeee"...Jamaa akawa anasita,Kikwete akasisitiza...Sema Magufuli hoyeee!!Jamaa ikabidi aseme "Magufuli hoyeee"..Halafu akamgeukia JK akamwambia "Umeridhika sasa niliposema Magufuli hoyeee"
Baada ya pale jamaa alitoa salamu,na kusema mimi ni Chadema na sisi Chadema tunachukia uhalifu.Kwa hiyo mtoa mada watu tulikuwa makini kuangalia...Na kuna kitu leo tumeendelea kujifunza juu ya JPM na siasa za Tz
=========
Meya ajitetea Sababu ya kutokuhudhulia, Soma=>Meya wa Kinondoni amjibu Rais Magufuli, hakuwa na mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi wa Polisi