Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee

Sakata la madawa ya kulevya linazidi kushika kasi kwa mkoa wa dar se salaam, swali langu ni je mikoa mingine hakuna watu walioathirika na madawa, ni kwanini isiwe vita ya Tanzania nzima kutokomeza madawa haya kuliko kutokomeza sehemu moja tu wakati sehemu nyingine mambo yanaendelea?

Napenda kuwaasa wakuu wa mikoa kuiga mfano wa RC wa dar na kuanza mara moja kupigana na hii vita kwa kil mkoa.
 
Hongera za dhati zikufikie Mh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Kiukweli umethubutu kwa kiasi kikubwa, na umeingia kwenye history mpya hapa Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla. Hongera sana kaka mkubwa.

Naimani alie kuchagua hajafanya makosa ya kiufundi hata kidogo, Hongera pia kwa Mh Rais wetu mpendwa, Mh Dr John P Magufuli.

Hatua hii uliofikia ni hatua nzuri ya kupongezwa na kuigwa na wakuu wa Mikoa mingine Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla. Watanzania wenye akili timamu tupo pamoja na nyinyi kwa asilimia zote na msikibali kugeuka nyuma msije kugeuka jiwe la chumvi.

Mh kaka Makonda naomba kujua kwanini umeweza kudeal mpaka na Watanzania wanaoishi mpaka China South Afrika ila baadhi ya sehemu hapa Tanzania unajipa mipaka ikiwa wote ni drugs dealer?

Swali la pili kwanini kwanini usiongezewe mipaka ikawa Tanzania yote kwasababu wewe ni mkuu wa wakuu wote wa mikoa?

Ukizingatia Baba yetu Mh Rais kakuunga mkono wa dhati.

Mungu akupe nguvu na ujasiri katika kipindi iki kigumu, na bahati nzuri umekili una kifua, hivyo mimi ni mmoja wapo nakuunga mkono maana inasikitisha sana mtaani.

Mungu bariki viongozi wetu na Mungu bariki Tanzania.
 
Kwa mara ya kwanza nashudia "meno" ya serikali inayoendesha mambo yake kwa mjibu wa sheria bila upendeleo, na bila woga. Kabla yake sheria nzuri ya madawa ya kulevya ilikuwa kama mapambo tu. Laws must be enforced by the republic. No retreat no surrender. Serikali iendelee kutimiza wajibu wake bila kujali kelele za milango.
 
RC Makonda, vita uliyoianza ni ngumu lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutashinda na kuliokoa Taifa hili katika Madawa ya Kulevya. Kaa ukijua tunakusapoti kwa hali na mali ikiwemo maombi mazito kwa Mungu kwani najua iko siku wanaokupinga na kukubeza watakuja kukupongeza. Hii vita si ya kwako peke yako bali ni yetu sote.

Karibu uweke neno la kumpongeza na kumpa moyo RC wetu kwa vita hii dhidi ya Madawa ya kulevya.

makonda-559x520.jpg
 
Rais Magufuli apigilia msumari Sakata la Madawa ya Kulevya......Ataka Polisi Wasiangalie Umaarufu wa Mtu, Asema hiyo sio Vita ya Makonda Pekee

MPEKUZI / 2 days ago

[https://1]

Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya bila kuangalia umaarufu au cheo cha mtu.


Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Vanance Mabeyo pamoja na viongozi wengine wa majeshi, na mabalozi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kwa hatua nzuri aliyoichukuwa ya kuwasimamisha kazi Askari Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi.


Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.


"Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP.


"Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.


"IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu."Amesema Rais Magufuli


Akizungumzia suala la uendeshaji wa kesi za dawa kulevya, Rais Dkt Magufuli amemwambia Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa kesi hizo zinaendehswa taratibu sana huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya aliyekamatwa mkoani Lindi lakini hakuwahi kufikishwa mahakamani.


"Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani"Amesema Rais Magufuli.


Rais Magufuli amesema kuwa vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake bali ni ya Watanzania wote huku akivitaka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kushirikiana kutokomeza tatizo hili linalopelekea kupoteza nguvu kubwa ya taifa.

Kauli hii ya Rais Magufuli inakuja ikiwa ni siku chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atangaze vita dhidi ya watu wanaohusika na dawa za kulevya akianza kwa kutaja majina yakiwemo ya askari na ya wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde n.k.

Siku tatu baada ya Makonda kuwataja watuhumiwa hao, IGP Ernest Mangu alichukua hatua ya kuwasimamisha askari 12 waliotajwa na kuahidi kuchukua hatua zaidi, jambo ambalo limepongezwa na Rais Magufuli na kumueleza kuwa endapo asingechukua hatua hiyo, angejua kuwa na yeye anahusika.
 
Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.
Mimi nilidhani kasema "hata nikiwa ni mimi, nikamatwe bila kujali jina langu"
Kumbe mke wake!!!!!!!!!!
 
makonda usirudi nyuma endelea kwani kazi unayofanya ni nzuri. Hawa wabunge kwenye mambo ya msingi hawashikamani....waliaacha fao la kujitoa likapita leo hii masuala ya madawa wamekuwa wamoja ndo mujuwe tuna taifa gani tanzania hata kama makonda kuna sehemu anakosea lakini anachofanya ni sahihi kwa nchi hata kama ni kidogo. na watanzania tubadilike tumekuwa watu wa kushabikia sana na kuona kila kitu serikali inakosea
 
Navyojua Mimi wauza ngada ni watu ambao wanajulikana popote ila inashindikana tu kupatikana ushahidi swala hili me naona bora tuachie taasisi husika co kutaja taja majina tu me czani kama kutakuwa na msaada wowote katika vita hii.

kitu
 
Hii list ya jk hii,nani aliiona? Nani anauhakika ilikuwepo? Nani aliiandaa? Kuna ishu ya masogange ya mwaka uleee! Hivi hawezi kuwa ameacha?na je ni kweli tangu pale hakuna wengine walioanza baada yake! Acheni tuhangaike na ya leo siyo historia.Hatutawamaliza ila watapungua.
 
Navyojua Mimi wauza ngada ni watu ambao wanajulikana popote ila inashindikana tu kupatikana ushahidi swala hili me naona bora tuachie taasisi husika co kutaja taja majina tu me czani kama kutakuwa na msaada wowote katika vita hii.

kitu
Ni swala ambalo linge hushisha na nchi za nje kama chini walipo wafunga wa kitanzania walio kamatwa na madawa haya na lingekua kimya kimya kwanza mpaka ushaidi ungepatika na swala la watumiaji kungeanzishwa sheria mpya itakayo wabana .
 
(TANZANIA YA VIWANDA) Hivi kunabkiwanda chochote serikali imeshaanza hata mpango wa kujenga,?? au kufufua,??
 
Back
Top Bottom