Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya. Asema si kazi ya Makonda pekee.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

Rais Magufuli amesema anamuomba Jaji Mkuu asizicheleweshe kesi za madawa ya kulevya kwani kuna mtuhumiwa mkubwa wa Dawa za Kulevya anashikiliwa Lindi bila ya kufikishwa Mahakamani.

Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP.

Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.
=======
Wanabodi,

Mimi ni chipukizi kwenye uchambuzi wa medani za siasa. Style ya Magufuli ya uongozi wengi hamtaki kuamini. Mheshimiwa rais ni mzalendo wa juu. Hii season Sasa tutakwenda kushuhudia jambo kubwa.

Hoja ninazo hizi hapa;

1. Kumbuka matukio yamefuatana kama hivi lilianza la siku ya sheria. Rais alionya mambo makubwa alisema hataki mambo ya kuchelewesha kesi.. Aliashiria kitu.

2. Makonda kijana mchapakazi ametoka marekani juzi, amefika akaanza moja kwa moja na hii ishu ya hii vita.

3. Kesho yake wanakuja watu wanawatetea Hawa wasanii kwamba tunakwenda eti kuua brand. Kuna waziri ame mbeep mheshimiwa rais.

4. Tukio lililofuatia ni sauti za Wakuu wa vikosi. Alianza IGP, kisha kamanda Sirro.

5. Kwa akili ya kawaida unaona kabisa hawa wasanii wanamilikiwa na wanasiasa fulani vinara wa unga.

6. Tukio lililofuatia ni rais akamteua mkuu wa majeshi mpya

7. Kisha Akasema kabisa meli ya MV Bagamoyo ya enzi ya awamu ya nne itakuwa ya jeshi kufanya doria. Ikumbukwe baharini ndio unga unapitia sana.

8. Kisha makonda akajitokeza kuwapa siku kumi. Wenye uelewa mkubwa wa saikolojia wanajua ki nacho endelea.

9. Msumari wa mwisho tutashuhudia mpaka mkuu wa nchi amesema tena kama wewe ni great thinker utagundua facial expressions aliyokuwa nayo rais.

Tazama serikali yote ilikuwepo ikulu. Hamuoni hii ishu ni kubwa imefikia?

My Take: Watanzania tumempata Rais. Tumpe ushirikiano kwa vyombo vyake. Tazama litakalotokea hivi karibuni.. Mark my word. Hakuna rais Tanzania kama Magufuli.

Msioamini kuwa hii vita sasa imeanza subirini muone. Hisia zote zinanipeleka jambo kubwa litagusa mpaka vigogo wakubwa. Msishtuke kutajiwa viongozi fulani. Hilo Kwa Sasa Tanzania linatokea.

Ma drug dealer Imekula kwenu. Muda mrefu Sasa mmetamba. Ishara zote Sasa wazi.
 
Safiiiiii safiiiiii... nakufa kwa furaha huku

Salute you Mr. President wa moyo wangu, i feel energized & bursting with joy, nilikuwa nasubiria sana kauli ya Mkuu wa nchi yangu.!

Ukitaka uzime kabisa moto wa drugs dealers mwagia petrol.. hahaaaaaaaaa.. eti Brand.. brand? ya drugs..? et Busara, busara kwa drug dealers..? damn..!!

Wow.. the best ever President JPM..

He is real, kiongozi halisi wa nchi yetu toka moyoni..!!

Nchi hii ilishachezewa sana sana, sasa inatosha, na huyu ndio JPM i used to know, unwavering, unshakable akijua ukweli, with classy, with style, with determination.. a great great leader..!! Na Mungu akubariki daima na milele yote..!!

N.B: Mh. RC Makonda goo, goo ahead..!!

CC: [HASHTAG]#NapeMosesNnauye[/HASHTAG]


Message

Sent ✔ delivered✔ read✔ understood✔ & complied✔



Na kwaheriiiiiiiii...!!





Bashe - bungeni amuunga mkono Makonda




Sheikh: Madawa ya kulevya ni hatariii, haramu.. ujumbe maridhawa 100% msikilize hapa..!!
 

Attachments

  • VID-20170205-WA0003.mp4
    2.2 MB · Views: 87
mh. rais wa Nchi akiongea hivi sasa baada ya kumwapisha mkuu wa majeshi amesema kuwa vita ya madawa ya kulevya inawahusu watanzania wote. haimhusu makonda peke yake wala rais peke yake. amempongeza IGP Mangu kwa hatua aliyochukua ya kuwasimamisha kazi askari waliotajwa kuhusika na biashara hii na kumweleza kuwa asingefanya hivyo angeshamtumbua na yeye.

Tunampongeza sana rais Magufuli kwa hatua zako za kuwalinda watanzania, usiku na mchana.
 
Akizungumza baada ya kumuapisha CDF Mabeyo Rais amesema anaunga mkono operesheni ya kutokomeza madawa ya kulevya inayofanywa na RC Makonda.
Amesisitiza kuwa yoyote atakaye kamatwa awajibishwe ipasavyo na kuomba kesi za madawa ya kulevya zipelekwe haraka haraka.
 
Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya. Asema si kazi ya Makonda pekee.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

Rais Magufuli amesema anamuomba Jaji Mkuu asizicheleweshe kesi za madawa ya kulevya kwani kuna mtuhumiwa mkubwa wa Dawa za Kulevya anashikiliwa Lindi bila ya kufikishwa Mahakamani.

Rais Magufuli asema kuwa anajua kuwa IGP Mangu alipokea simu nyingi sana lakini anampongeza kwa kusimamia msimamo wake kwani kama angeyumba basi asingekuwa IGP leo.
Hivi Lindi na Mtama sindio hukohuko?!!!!!Kuuliza na kushangaa si ujinga.
 
Back
Top Bottom