Rais Magufuli anapoacha kusafiri nje ya nchi huokoa milioni 100, lakini anakosa fursa ya kuvutia uwekezaji wa matrilioni

Kuhusu suala la kusafiri hilo sahauni..ukitaka kujua sababu muulizeni sumaye..ndio anajua vizuri.
 
Kwa kweli nampongeza JPM kwa maamuzi take ta kutosafiri nje ya nchi

Kwa makadirio,anapoacha kusafiri nje ya nchi,huwa anaokoa milioni karibu 100,

Kiongozi anaposafiri nje ya nchi huandaliwa mikutano na matajiri wakubwa wa dunia ambao wana maelfu ya matrilioni katika akaunti zao,wanahitaji fursa tu ziko wapi,wanakuja na malori yaliyojaa hela ambazo hazijawahi kuonekana

Kukutana na midude hii iliyotengeneza hela karne na karne zilizopita ni jambo muhimu kwa mtu yeyote anayelia kuhusu viwanda,ajira na kukuza uchumi

Ni jambo la ajabu kiongozi anakuja kijijini kwetu KAKONKO,Kigoma,anatuambia Tanzania yake ni ya viwanda,nadhani anakuwa hajui kuwa anaoongea nao hata Jana wamelala njaa na hawana hela ya Kununua hata nati ya baskeli,sembuse kiwanda!?

Nchi yetu ina tatizo la mitaji,lakini kuna watu tayari wana mitaji huko duniani,tuwaalike waje wawekeze mitaji yao na tusiwatukane hovyo majukwaani,

Ukituimbia Tanzania ya viwanda huku Itigi,huo mtaji wa viwanda tuutolee wapi ?

Hivi wakati ulaya inaingia katika mapinduzi ya viwanda ,je viwanda hivyo vilitokana na hotuba za majukwaani?au ulikuwa ni mchakato mrefu wa kisayansi ulioleta mapinduzi ya viwanda?

Nadhani mkuu akatafute mitaji huko duniani,ailete hapa,viwanda vishamiri,kutuimbia viwanda hapa KAKONKO na itigi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa

Unaokoa milioni 100,unakosa fursa ya maelfu ya matrilioni,laiti angekuwa anasafiri,hakika angejua neno "tajiri" lina watu wanastahili kuitwa,na angeacha kuhangaika na akina manji

Unafiki wetu watanzania ndiyo huu!
Rais mstaafu JK mlimwita majina ya ajabu kwa kupenda kusafiri nje ya nchi mara kwa kwa mara. Leo Magufuli hafanyi kama Kikwete, ona sasa mnavyosema!!!! Tuache unafiki!!!!!!
 
yule alisafiri sana tukasema huyu hasafiri pia tuna sema ama kweli ubinadamu kazi

Mkuu hakuna tofauti kati ya anayesafiri sana na asiyesafiri sana. Anayesafiri sana ataanza kuwa na safari zisizo na tija, na asiyesafiri hatakaa avutie fursa.
 
Msukuma anaweza kuwa na ngombe 2000 lakini analala kwenye Nyumba ya tope,analalia ngozi,Nyumba ya nyasi,watoto wanaishi maisha kama ngombe,ngombe wakitoka zizizni wanatoka na watoto kwenda machungani(sio shule)

Mchaga anakuwa na ngombe tano,hazururi nazo nchi nzima akiharibu Misitu(piga picha msitu wa mlima Kilimanjaro ungekuwa usukumani),Nyumba take ya bati,tofali za simenti,watoto wake wanasoma shule nzuri,wanavaa vuzuri
umenichekesha saaana kwakweli
 
Zote hizo ni exremes. Alitakiwa kuwa moderate kwa kusafiri kwa kiasi. Hata chakula ukipewa na kikiwa na chumvi nyingi sulihisho lake sio chakula kisiwe na chumvi kabisa.
Kweli kabisa,lazima afanye ziara za kimkakati katika nchi muhimu,na mabalozi wamuwekewee na kumuandalia mikutano muhimu iliyofanyiwa tathmini ya faida zake kwa nchi

Sasa tumekaa wote humu humu,tunatazamana
 
Wawekezaji wakubwa waliopo ndani ya nchi kwa sasa wanawaza kufunga shughuli zao na kuhamia nchi nyingine..
Hao wapya watavutiwa na nini..??
 
tatizo kumbe tupo wengi hatuelewi mambo sera ya viongozi wengi wa afrika sasa hivi ni kutaka kujitawala bila kupigia magoti wakuu wa nchi za ulaya kwa kubana matumizi na kutumia lasilimali zetu to the maxmum pamoja na kukusanya kodi ya kutosha na kubana ukwepaji wa kodi .ili baadae na sisis waje kuomba misaada kutoka kwetu

Na kwa kweli wewe ndo huyaelewi kabisa.. Tafuta weledi wakueleweshe mwenendo wa Mtakatifu Pogba
 
Watanzania watu hovyo sana.

JK alikua anasafiri kila siku mkaanza kulialia, amekuja JPM hasafiri mmeanza kulalama tena.

Hatueleweki Watanzania tunataka nini hasa
 
Kwani Rais ni TIC?
Ndio mkuu,aliyemteua pale TIC kamshikia tu nafasi,lakini yeye ndio TIC,si unajua Rais ndio muajiri mkuu na ndio mtendaji mkuu?! Akitenda TIC au mtumishi yeyote,basi ametenda mwajiri mkuu,rais,na mwisho wa siku utamsikia jukwaani akitamba kwamba ni yeye ndiye alitenda
 
Kwa kweli nampongeza JPM kwa maamuzi take ta kutosafiri nje ya nchi

Kwa makadirio,anapoacha kusafiri nje ya nchi,huwa anaokoa milioni karibu 100,

Kiongozi anaposafiri nje ya nchi huandaliwa mikutano na matajiri wakubwa wa dunia ambao wana maelfu ya matrilioni katika akaunti zao,wanahitaji fursa tu ziko wapi,wanakuja na malori yaliyojaa hela ambazo hazijawahi kuonekana

Kukutana na midude hii iliyotengeneza hela karne na karne zilizopita ni jambo muhimu kwa mtu yeyote anayelia kuhusu viwanda,ajira na kukuza uchumi

Ni jambo la ajabu kiongozi anakuja kijijini kwetu KAKONKO,Kigoma,anatuambia Tanzania yake ni ya viwanda,nadhani anakuwa hajui kuwa anaoongea nao hata Jana wamelala njaa na hawana hela ya Kununua hata nati ya baskeli,sembuse kiwanda!?

Nchi yetu ina tatizo la mitaji,lakini kuna watu tayari wana mitaji huko duniani,tuwaalike waje wawekeze mitaji yao na tusiwatukane hovyo majukwaani,

Ukituimbia Tanzania ya viwanda huku Itigi,huo mtaji wa viwanda tuutolee wapi ?

Hivi wakati ulaya inaingia katika mapinduzi ya viwanda ,je viwanda hivyo vilitokana na hotuba za majukwaani?au ulikuwa ni mchakato mrefu wa kisayansi ulioleta mapinduzi ya viwanda?

Nadhani mkuu akatafute mitaji huko duniani,ailete hapa,viwanda vishamiri,kutuimbia viwanda hapa KAKONKO na itigi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa

Unaokoa milioni 100,unakosa fursa ya maelfu ya matrilioni,laiti angekuwa anasafiri,hakika angejua neno "tajiri" lina watu wanastahili kuitwa,na angeacha kuhangaika na akina manji
So it means akianz kwnd nje 2tapata matilioni? Hv hyo matilioni yanatka bure au kw mashart magumu
 
Waafrika tuna matatizo kila kukicha tunawaza kuombaomba, wawekezaji wa dhati huwa wanakuja wenyewe taratibu, Anachofanya Rais na serikali yake safi kwasasa ni kutengeza mazingira salama, mazuri yenye kutokuwa na harufu ya rushwa wala ufisadi kwa wawekezaji wa dhati.

Kutafuta wawekezaji kwa kujipendekeza pendekeza ndio kunakosababisha rushwa na wengine kuihujumu nchi. Pia haiwezekani wawekezaji wakaja kwa mara moja nao wanaangalia mazingira salama ya investment zao. Angalia issue ya Dangote bila ya Rais kuingilia kati tayari wapiga dili walishaanza kumkatisha tamaa mwekezaji katika mradi muhimu kama ule na kwa ujumla mambo haya ndio yanayofanya hata wengine kushindwa kuja kuwekeza maana wanawasiliana kwenye mikutano ya board zao.

Great thinkers walishasema ukimfuhata tajiri kumbembeleza aje kufanya biashara ama kuwekeza mara zote anakupa masharti magumu ingawa kabla ya kufuhatwa alishaonyesha nia ya kuja kuwekeza. Ndio maana marais wa nchi zenye viwanda huwa waanapokuwa na ziara katika nchi za dunia ya tatu uongozana na matajiri ili kuangalia fursa za uwekezaji.

Cha msingi ni kuwashauri wanasiasa wengine waache kupiga kelele fake kila kukicha kujaribu kuonyesha ulimwengu kuwa kuna hali tete nchini, kupotosha kuwa hakuna usalama nchini, hizi kelele haziwasaidii, wala hazisaidii kukuza vyama vyao na wala hazina maslahi kwa nchi. Kwa wenye akili pana wanaona ni upunguani uliopitiliza.

Watu wa karne hii wanaangalia maswala ya kukuza uchumi, mazingira salama na safi, pia siasa safi na uongozi ulio bora kama huu wa sasa, na maslahi kwa nchi. Hizi kelele za siasa tumeanza kuzichoka kwakweli

Uzalendo wa nchi ndo agenda namba moja..... Kuwa mzalendo ...Jenga uzalendo
 
So it means akianz kwnd nje 2tapata matilioni? Hv hyo matilioni yanatka bure au kw mashart magumu
Hakuna kitu mkuu, watanzania ni watu wa kulialia tu kila utakachofanya wanataka ufanye tofauti na unavyofanya.

JK kasafiri sana na tukalalama sana, Magu hasafiri napo tunalalama tu.

Hatueleweki tunachotaka ni nini
 
Waafrika tuna matatizo kila kukicha tunawaza kuombaomba, wawekezaji wa dhati huwa wanakuja wenyewe taratibu, Anachofanya Rais na serikali yake safi kwasasa ni kutengeza mazingira salama, mazuri yenye kutokuwa na harufu ya rushwa wala ufisadi kwa wawekezaji wa dhati. Kutafuta wawekezaji kwa kujipendekeza pendekeza ndio kunakosababisha rushwa na wengine kuihujumu nchi. Pia haiwezekani wawekezaji wakaja kwa mara moja nao wanaangalia mazingira salama ya investment zao. Angalia issue ya Dangote bila ya Rais kuingilia kati tayari wapiga dili walishaanza kumkatisha tamaa mwekezaji katika mradi muhimu kama ule na kwa ujumla mambo haya ndio yanayofanya hata wengine kushindwa kuja kuwekeza maana wanawasiliana kwenye mikutano ya board zao.
Great thinkers walishasema ukimfuhata tajiri kumbembeleza aje kufanya biashara ama kuwekeza mara zote anakupa masharti magumu ingawa kabla ya kufuhatwa alishaonyesha nia ya kuja kuwekeza. Ndio maana marais wa nchi zenye viwanda huwa waanapokuwa na ziara katika nchi za dunia ya tatu uongozana na matajiri ili kuangalia fursa za uwekezaji.

Cha msingi ni kuwashauri watu kama viongozi wa CHADEMA kelele nyingi fake wanazopiga kila mara kujaribu kuonyesha ulimwengu kuwa kuna hali tete nchini, kupotosha kuwa hakuna usalama nchini haziwasaidii, wala hazisaidii kukikuza chama chao na wala hazina maslahi kwa nchi. Kwa wenye akili pana wanaona ni upunguani uliopitiliza.

Uzalendo wa nchi ndo agenda namba moja..... Kuwa mzalendo ...Jenga uzalendo
Kwa hiyo mmekaa hapo magogoni mnasubiri wawekezaji waje?

Kwa vivutio gani ambavyo havipo kwingine na katika mabara mengine ya dunia?!
 
Mawazo ya kimasikini hayo, ulishaambiwa dunia imekuwa kijiji uhitaji kwenda nje physically kila mara kutangaza vivutio, ama kuita wawekezaji, technologia ya mawasiliano naona imekupita kushoto.

Hayo yalikuwa zamani usiishi kimazoea mambo yanabadilika
Watalii, wawekezaji hawaendi nchi fulani kwasababu kiongozi wa nchi anaenda kuwatafuta, mazingira safi ya uwekezaji ndio jambo la muhimu zaidi na hizo taharifa wanazipata kupitia njia mbalimbali za mawasiliano ambazo ni nyingi sana kama huna habari. Kwenda kupiga domo wakati hali ya nchini kwako ni mbovu na imejaa rushwa na wizi ni kupoteza pesa na muda.

Wenzetu wa dunia ya kwanza huwa wanasoma kila wakati, wanapitia taharifa kila wakati.... Sisi tunawaza kuambiwa, bila kuambiwa hatujui nini kinaendelea duniani, kutegemea sana kuambiwa unaweza kupotoshwa kama hujui (Tumia muda kusoma website zipo nyingi sana sana)

Nina wasiwasi mpaka leo nyinyi ndo mnaoenda Tanesco, ama dawasco kulipia bili bado hamuamini kuwa unaweza kulipia kwa njia za mitandao.
 
Mawazo ya kimasikini hayo, ulishaambiwa dunia imekuwa kijiji uhitaji kwenda nje physically kila mara kutangaza vivutio, ama kuita wawekezaji, technologia ya mawasiliano naona imekupita kushoto. Hayo yalikuwa zamani usiishi kimazoea mambo yanabadilika
Watalii, wawekezaji hawaendi nchi fulani kwasababu kiongozi wa nchi anaenda kuwatafuta, mazingira safi ya uwekezaji ndio jambo la muhimu zaidi na hizo taharifa wanazipata kupitia njia mbalimbali za mawasiliano ambazo ni nyingi sana kama huna habari. Kwenda kupiga domo wakati hali ya nchini kwako ni mbovu na imejaa rushwa na wizi ni kupoteza pesa na muda.

Wenzetu wa dunia ya kwanza huwa wanasoma kila wakati, wanapitia taharifa kila wakati.... Sisi tunawaza kuambiwa, bila kuambiwa hatujui nini kinaendelea duniani, kutegemea sana kuambiwa unaweza kupotoshwa kama hujui (Tumia muda kusoma website zipo nyingi sana sana)
Nina wasiwasi mpaka leo nyinyi ndo mnaoenda Tanesco, ama dawasco kulipia bili bado hamuamini kuwa unaweza kulipia kwa njia za mitandao.
Dunia kijiji?

Hata kijijini kwetu huwa tunatembeza mbogamboga,nafaka au kupeleka mifugo mnadani,huwa hatulimi na kuyaacha hapo hapo shambani ili wanunuzi watutafute,
 
Back
Top Bottom