Rais Magufuli anafanya haya yote kwa niaba ya Watanzania

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Watanzania tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwani Mwenyezi Mungu ametupenda zaidi kwa kutupatia Rais John Magufuli ambaye ukitazama matendo, kauli na maisha yake yanaonyesha amejitoa kwa ajili ya Watanzania.

Dkt. Magufuli ni Rais wa kipekee ambaye amekataa kabisa kupanda ndege kwenda safari za kimataifa nje ya nchi na badala yake amewaachia wengine na yeye ameamua kujikita kutatua matatizo ya Wananchi. Katika hili Watanzania tumepata faida ya kupata Rais anayetumia vyema kodi zetu na si kuzifuja pia matatizo kumalizwa na maendeleo kupatikana kwa uharaka.

Ni Rais Magufuli huyu huyu ameamua kuthibiti rasilimali zetu ili ziwanufaishe Wananchi na si wajanja wachache. Rais Magufuli ameamua kuzuia usafirishwaji wa mchanga wa madini nje ya nchi, kujenga ukuta wa Mererani, kuzuia uchimbaji holela wa madini hali iliyozaa vita vya kiuchumi baina yetu na wale waliozoea kufaidi rasilimali za Taifa. Haya yote anafanya kwa niaba yetu Watanzania.

Bado wapo baadhi ya Watu wanamlaumu Rais Magufuli kuwa anapeleka pesa nyingi kwenye ujenzi wa miundombinu na kununua ndege! Tumeshajiuliza hiyo miundombinu inajengwa kwa faida ya Magufuli au ya Watanzania? Hizo ndege zinanunuliwa kwa faida ya Magufuli au ya Watanzania? Ndege zitapandwa na Watanzania wote, madaraja yatatumiwa na Watanzania wote, Reli ya umeme inapandwa na Watanzania wote na si kwa maslahi ya JPM. Tukishajua anafanya kwa maslahi ya Watanzania wala hatutaweza kulaumu chochote.

Wengine wanamlaumu Rais Magufuli kwa Serikali anayoiongoza kushupalia ukusanyaji wa kodi ambao wengine wanaona wanakamuliwa mno. Watu hao hao wanasahau ya kuwa anachokifanya Rais Magufuli ni kujenga uwezo wa ndani wa kifedha ili tuweze kujitegemea lakini kubwa tuweze kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ili Serikali iweze kujenga miundombinu, kupeleka huduma za kijamii kama umeme, maji na elimu bora na bure kila kona ya nchi. Rais Magufuli atawezaje kuendesha Serikali, kutoa elimu bure, kujenga miundombinu nk pasipo kukusanya kodi? Ni wajibu wetu kutambua kodi zinazokusanywa si kwa mkomoeni wala si kwa faida ya Rais Magufuli bali kwa faida ya Watanzania wote.

Rais Magufuli ameweka pembeni tabasamu kwenye mambo ya hovyo na badala yake amekuwa mkali pindi anapotaka kurekebisha masuala. Ameweka ukali kuwatimua wenye vyeti feki waliokuwa wanaziba ajira za Vijana wasomi; aliamua kufuta Watumishi hewa waliokuwa wanakula mishahara hewa na hivyo kufanikiwa kuokoa pesa walizokuwa wanalipwa; ameamua kuwatumbua watendaji wa hovyo na wabadhilifu wa mali za umma ili kujenga nidhamu ya uwajibikaji kazini.

Haya yote Rais Magufuli anayafanya si kwa maslahi yake bali kwa manufaa yetu Watanzania. Jambo tunalotakiwa kulifanya ni kumuunga mkono na kumuombea kwani ameonyesha nia, uwezo, dhamira safi na malengo chanya ya kiukombozi kwa Taifa letu kiuchumi.

*Shilatu E.J*
 
Ukiona Baba anapigiwa upatu na rafiki zake kwa watoto ili wampende na kumuona Baba bora basi ujue wanataka bia za bure ama wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa!!
 
Siku zote aliewakung'atwa na nyoka hata akiguswa na jani hupiga kelele..
Tangu akoswe koswe kwenye ile ajali ya holkopta pale mongo la ndege kama mwoga hadi sasa sio kwanba hapendi kwenda nje hapana anaogopa kupanda ndege ya kwenda masafa
 
Wandamba, ukijisikia haja unashauriwa kwenda chooni kuliko kuharisha hadharani kama ulivyofanya. Kilangila.
 
Nadhani Tuvute subra kwa miaka kumi itatoa jibu la maendeleo. Kwa sababu hivyo vyote ulivyotaja kwa kiasi kikubwa ni miradi ambayo inaweza kujiendesha kwa faida au hasara na wakati huo huo. Hatuwezi kuitathmini kwa sasa mana ndio bado mipya mingine ndio inaanza.

Mfano ni Awamu ya Nne kwa miaka kumi kila MTU Leo anaona jambo la kusema. Yawe ni mabaya au mazuri.

Tumeona Madaraja makubwa kama la Kigamboni.
Tumeona mabarababra nchi nzima.
Tumeona bomba la gesi kutoka Mtara mpaka Dsm.
Tumeona Manoari za Jeshi letu.
Siku za maadhimisho ya kitaifa tumeona midege ya kisasa ya Jeshi letu ikipita kwa kasi.
Tumeona demokrasia ikistawi.
Tumeona vijana wadogo wakionyesha uwezo wao kisiasa kutokana na uhuru wa kutoa maoni.
Vijana tunaowaona Leo ndani na nje ya CCM ni zao la demokrasia wakati wa awamu ya NNE.
Demokrasia ingeminywa hakuna mtu angemjua Katambi ni nani.
Uhuru wa kukosoa na kupingana kwa hoja ulitufanya tuwapate vijana wenye uwezo wa kujenga hoja kwa kujiamini.

Awamu ya nne Tumeona sura ya miji na majiji yetu ikibadilika na kukua kwa kasi kubwa.
Uchumi wa MTU mmoja mmoja uliimarika kuanzia wafanyakazi na wafanyabiashara.

Awamu ya nne Tuliona Miradi mikubwa ya Maji .
Tuliona miradi ya umeme wa REA ikianzishwa.
Ujenzi wa Chuo Kikuu cha UDOM.
Ongezeko la wasomi wanaomaliza Vyuo vikuu.
Ujenzi wa Shule za sekondari kila Kata.
Tuliona ujenzi wa maabara nchi nzima.
Ukarabati wa viwanja vya ndege mikoa yote kuanzia na ujenzi wa Terminal III .
Ununuzi wa Magari ya kisasa ya polisi kwa ajili ya kudhibiti vurugu za waandamanaji.
Kuimarika kwa mifuko ya pension.

Awamu ya nne Tuliona kuanzishwa kwa Bima ya Afya kwa wafanyakazi na familia zao.
Kuanzishwa kwa Leseni za udereva za smart card.
Tuliona kuanzishwa kwa vitambulisho vya Taifa na vya kura.
Majengo yenye hadhi ya ofisi za umma kama jengo la Uhamiaji.
Chuo bora kabisa cha kiusalma.
Ukarabati wa Uwanja wa Taifa a.k.a shamba la bibi.
Kuanzishwa kwa mikoa na Wilaya mpya na Kuweka miundo mbinu yake.
Kusomesha vijana wengi wa Udaktari nje ya nchi.
Ujenzi wa Hospitali kubwa ya Mloganzira.
Kuanzishwa kwa mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Tuliona ununuzi wa vivuko jiji la DSM.
Ujenzi wa viwanda vingi vya Sementi.
Tuliona Ujenzi wa jengo kubwa la Mamlaka ya Bandari.
Taasisi ya kubwa kabisa ya Moyo ya Jakaya Kikwete na vifaa vya kisasa.
Awamu ya nne Ajira binafsi na za umma ziliongezeka kila Mwaka.
Awamu ya nne Tuliona serikali ikianzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielectronic kwa kutumia EFD machine.
Tuliona serikali ikinunua Vifaa vya kunasa magari yanayokwenda mwendo kasi maarufu kama Tochi.
Kukua kwa tasnia ya habari.
Kukua kwa tasnia ya muziki.
Kukua kwa michezo ya soka n.k.
Kukua kwa tasnia ya uigizaji na film n.k.
Kariakoo iligeuka kuwa soko kubwa la Afrika Mashariki na Kati.
Maisha ya vijijini yalibadilika kwa kasi kwa watu kujenga nyumba bora za bati .
Vijana na wazee waliweza kumiliki magari binafsi na pikipiki nchi nzima.
Kuongezeka kwa nafasi za Wanawake Ili kiweka usawa wa kijinsia.
Kustawi kwa mfuko wa TASAF.
Mifuko ya Pembejeo kwa wakulima n.k.
Kusimamia hali ya mvutano wa Kisiasa Zanzibar na kujenga maridhiano.

Hayo ni baadhi ya mafanikio ya awamu ya NNE kwa kipindi cha miaka kumi.
Lakini yote hayo hayakufanywa na MTU mmoja kwa fedha zake Bali ni kodi za wananchi.
Kama kuna wanaoumia ni wananchi kwa kutwishwa mzigo wote wa kodi za kila aina.

Na kama kuna wanaofaidi ni watawala kwa kuwa na maslahi mazuri ,heshima kubwa,na mamlaka makubwa kupitia kodi za wananchi hao hao.
Hivyo watu wa kusifiwa pakiwepo maendeleo ni wananchi wanaolipa kodi.

Na watu wa kulaumiwa maendeleo yakikosekana ni viongozi wanaosimamia kodi zetu na rasilimali zetu.
Afrika tunawasifia viongozi na kuwadharau waliotoa pesa za maendeleo ambao ni wananchi kwa kuminya Uhuru wao wa kuhoji matumizi ya kodi zao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom