Rais Magufuli anaenda kinyume na maneno ya Mwl. Nyerere

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mwalimu Nyerere alikuwa Ni Kiongozi Imara sana na Mwenye Utu wa Ajabu. Alikuwa na amtihani Mkubwa sana wa Kuongoza Nchi katika Siasa za Dunia zilizoathiriwa na Vita Baridi. Na Mapambano ya Kudai uhuru wa nchi za Kusini Mwa Africa.

Makaburu Wangeliweza Wangemtoa Roho wakati Wowote. Lakini wakati wote huo alipenda sana Watu wake, Na hata tulipokuwa na Njaa Miaka ya 1964 aliomba chakula Marekani, Mwaka 1974 na hata Mwaka 1984 Mwaka mmoja kabla ya Kung'atuka Kulikuwa na Njaa na Pia akaomba Wamarekani wakatuletea Misaada ya Mahindi ya Yanga!

Lakini Pia Nyerere alichukia Tabia ya Kufukuza watu Kazi ovyo na Aliweka Mazingira magumu sana kwa Watendaji wa serikali Kufukuza watu kila Mizuka Ikiwapanda.

Contrast

Na Angalia Kuhusu alivyozungumza kuhusu Mahitaji ya Chakula

Contrast
 
Screenshot_20170114-190435.png
 
Watanzania huenda tukawa ni Viumbe wanafiki kuwahi kutokea kwny Uso wa Dunia tangu kuumbwa.

Hatua anazochukua Magu ndio tulikuwa tukizililia
Taja siku mwaka mwezi tarehe na muda ntakubaliana na wewe!!watanzania walitaka raisi anae chukua hatua na mwennye maono watanzania walikuwa wapweke wanyonge na wenye kukata tamaa walihitaji mtu wakurudisha matumaini yao sio wakuja kuwasimanga1!kumbuka ccm wame wanyanyasa watanzania kwa kipindi kirefu na hawakuwa na sauti mapaka sasa walie mtegemea awarudishie imani kawa mtu wa lawama na masimango!!think twice kabla huja comment negro
 
Tuambie ni wapi pameshindikana kwa ukame kama si greenish nchi nzima? Na hata kama kuna drought ni vispots viduchu viduchu. Tatizo lenu hamumuelewi Mh. Rais. Vijana na watu wenye nguvu hawafanyi kazi siku hizi. Kazi yao ni pool table na hata yule anaeonekana anajitambua hataki kulima pia anaendesha boda boda tu. Nchi hii ukiichekea tulipofika utalisha watu mpaka kiama kifike. Rais yuko sahihi. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wafanye kazi ya kuwaelewesha watu wao wafanye kazi na si bidabida na pool. Go Magu go.
 
Alafu kwanini hujiulizi mfumuko wa vijana kuwa bodaboda na kuwa wacheza kamri za pool inatoka wapi!!kilimo kingekuwa kinalipa nani ange komaa na bodaboda na pool acha ujinga wa uttoni kuwa mwanaume mwenye fikra pana
 
Tuambie ni wapi pameshindikana kwa ukame kama si greenish nchi nzima? Na hata kama kuna drought ni vispots viduchu viduchu. Tatizo lenu hamumuelewi Mh. Rais. Vijana na watu wenye nguvu hawafanyi kazi siku hizi. Kazi yao ni pool table na hata yule anaeonekana anajitambua hataki kulima pia anaendesha boda boda tu. Nchi hii ukiichekea tulipofika utalisha watu mpaka kiama kifike. Rais yuko sahihi. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wafanye kazi ya kuwaelewesha watu wao wafanye kazi na si bidabida na pool. Go Magu go.
Well said
 
Taja siku mwaka mwezi tarehe na muda ntakubaliana na wewe!!watanzania walitaka raisi anae chukua hatua na mwennye maono watanzania walikuwa wapweke wanyonge na wenye kukata tamaa walihitaji mtu wakurudisha matumaini yao sio wakuja kuwasimanga1!kumbuka ccm wame wanyanyasa watanzania kwa kipindi kirefu na hawakuwa na sauti mapaka sasa walie mtegemea awarudishie imani kawa mtu wa lawama na masimango!!think twice kabla huja comment negro

1) Tulidanganywa nasi tukadanganyika kuwa Matumizi ya Serikal ni Makubwa hivyo yapunguzwe na sasa JPM kayapunguza tunalaumu

2) Tumelaumu Matumizi ya kawaida kuwa Mengi na ya Maendeleo kuwa kidogo JPM kaanza kubadilisha kwa kupunguza Matumizi ya kawaida na kuongeza ya Maendeleo tunamhoji kwanini kanunua Mahindi machache ya Akiba kuliko Jk kwani mlidhan Akiba ya Chakula ni Matumizi ya Maendeleo? si Mlikuwa Mnadanganywa kuwa Kazi ya Matumizi ya Kawaida Serikalini ni Upuuzi?

3) Tulikuwa tunasema Serikal Legelege hazikusanyi Kodi kaanza kukusanya tunalaumu

4) Tulilalamikia Wawekezaji wa Migodi kaanza kuwawakia tunamheuka eti anakimbiza Wawekezaji
5) Tulikuwa tunatukana Watawala wengine kwa kushindwa kuifufua ATCl sasa inafufuliwa tunamgeuka

6) Watumishi Wenye Makosa ilikuwa Taratibu za Kiutumishi zikifuatwa mnasema Wanabebana sasa wanatumbuliwa hapo hapo mnasema wanaonewa

7$ Tulilaumu Madili Bandarini kaenda kuyakomesha na wafanya Madili wamekimbia kutumia Bandari sasa tunamlaumu na kumgeuka
 
Watanzania huenda tukawa ni Viumbe wanafiki kuwahi kutokea kwny Uso wa Dunia tangu kuumbwa.

Hatua anazochukua Magu ndio tulikuwa tukizililia
Anaweza kuwa anachukua hatua njema sana lakini kauli zake sio za kusemwa na mtu wa cheo alichonacho..

Kwamfano hiki kinachosemwa sana mitandaoni japo sijajua kama ni kweli alitamka,...kwamba wakulima wauze mazao bei wanaotaka wao na wala wasipangiwe bei na mtu yeyote..hivi ndio wanavyofanya wakuu wa nchi??? Ndio kauli gani hizo??

Kauli ya mkuu wa nchi ina madhara makubwa sana..mkuu anaweza sema neno wenye njaa wakafarijika kabisa..pia anaweza akasema neno wenye njaa wakafa!!

Siamini kama hana zuri..ila mazuri hayatuzuii kuyaona mabaya!
 
Tuambie ni wapi pameshindikana kwa ukame kama si greenish nchi nzima? Na hata kama kuna drought ni vispots viduchu viduchu. Tatizo lenu hamumuelewi Mh. Rais. Vijana na watu wenye nguvu hawafanyi kazi siku hizi. Kazi yao ni pool table na hata yule anaeonekana anajitambua hataki kulima pia anaendesha boda boda tu. Nchi hii ukiichekea tulipofika utalisha watu mpaka kiama kifike. Rais yuko sahihi. Wakuu wa Wilaya na Mikoa wafanye kazi ya kuwaelewesha watu wao wafanye kazi na si bidabida na pool. Go Magu go.
Jifahamu Wewe nimelima heka 10 za ufuta Tanga nimemtumia 3M zilikauka nikavuna Debe 1 tu.
 
Anaweza kuwa anachukua hatua njema sana lakini kauli zake sio za kusemwa na mtu wa cheo alichonacho..

Kwamfano hiki kinachosemwa sana mitandaoni japo sijajua kama ni kweli alitamka,...kwamba wakulima wauze mazao bei wanaotaka wao na wala wasipangiwe bei na mtu yeyote..hivi ndio wanavyofanya wakuu wa nchi??? Ndio kauli gani hizo??

Kauli ya mkuu wa nchi ina madhara makubwa sana..mkuu anaweza sema neno wenye njaa wakafarijika kabisa..pia anaweza akasema neno wenye njaa wakafa!!

Siamini kama hana zuri..ila mazuri hayatuzuii kuyaona mabaya!

Muktadha wa kusema Wauze kwa Bei wanayotaka ilitokana na Kilio Chetu sie wenyewe kuwa Wakulima wanauza Mazao Yao kwa Bei ya hasara sasa ndo akawaambia this time msikubali kuapngiwa bei ya bidhaa zao bado na Hilo tunalaumu.
 
Watanzania huenda tukawa ni Viumbe wanafiki kuwahi kutokea kwny Uso wa Dunia tangu kuumbwa.

Hatua anazochukua Magu ndio tulikuwa tukizililia
Tumia akili brother usidhani Yale mazuri watu hawayaoni na sio lazima tuyasemee coz Magu katimiza wajibu wake, hatukumtuma kugombea!unataka kusema kwa kuwa yapo anayofanya vizuri ndio akikosea tusiseme?amepingwa Mungu baba atakuwa Magufuli?uliza moyo wako Magufuli ana mema tu?kama sio hayo mabaya tutayasema wapi?

Halafu kama ni unafiki mbona hata yeye nchi ilipokuwa inapindwa mbona alikuwa kimya
 
Watanzania huenda tukawa ni Viumbe wanafiki kuwahi kutokea kwny Uso wa Dunia tangu kuumbwa.

Hatua anazochukua Magu ndio tulikuwa tukizililia
Naanza kuamini ule utafiti inawezekana tunaongoza kwa unafiki na uongo duniani mkuu.........maana tunachokiomba leo kesho tunakikana
 
Back
Top Bottom