Rais Magufuli amteua Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Zimamoto

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
POLISI.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.

Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.

Uteuzi wa Dkt. Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

25 Aprili, 2016
 
Ndoto za jamaa kuwa IGP zinazidi kupoteaaa kabisa! media zilimfanyia promo kubwa sana achukue nafasi ya said mwema ila JK alishtukiaaa mapema.
Yani sio kuzidi kupotea, ndo asahau...na Mangu anaondoka hivi karibuni...wamempendekeza mapemaaaaa aondoke
 
hizi taarifa za kuteua na kutumbua zimejikita sana kwenye media sku hizi.
tusijisahau kalamu zetu kuzielekeza kila kona.
 
kadiri utumbuaji utavoendelea uteuzi nao utaendelea na katibu mkuu kiongozi ataendelea kutoa taarifa
 
Back
Top Bottom