Rais Magufuli amteua Phaustine Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Alli Malewa astaafu

Watu
Namkubali sana Dkt. Juma Alli Malewa ,kitendo alichofanyiwa na Kangi hata ingekuwa ni mimi ningeachia Ngazi ni udhalilishaji wa kiwango cha SGR,Kamishna ni mtu mkubwa sana hauwezi kumtoa kwenye kikao kama mtoto.

Big Up Dkt. Juma Alli Malewa kwa kuachia ngazi,Hakuna cha kustaafu wala nini umeachia ngazi mwenyewe.
watu ambao hamjawahi kwenda hata mgambo mna shida kweli! Jeshini mkuu wako hawezi kufika kabla yako and there is absolutely NO EXCUSE unless otherwise umecheleweshwa na mkuu wa mkubwa wako. Seniority and ranks ndo huamua chain of command, siyo huku uraiani baba ndevu,mama ndevu na mtoto ndevu,yaani watu mpaka wanabishana na CinC!!!
 
Mkuu kuna mtu kanitonya sasa hivi kuwa tetesi ni kuwa jamaa kajiuzulu ghafla kwa kuvunjiwa heshima kijeshi. Sasa kisiasa hilo ni pigo kubwa sana na hatari kijeshi hivyo funika kombe ni kutangaza kustaafu.
Hivi mtu anastaafu ghafla? Kwa cheo chake tungesha taarifiwa muda mrefu kuwa anastaafu.
Low level common sense inatwambia hivyo. Nakubaliana na wewe kabisa. Haiwezekani mtu wa cheo kile asitaafu kienyeji. Jiwe anadhani watu wote ni wajinga. Lakini ndivyo watu wa caliber yake walivyo, dictas......
 
Uteuzi huu ni kumtia moyo Mhe. Kangi Lugora kwa speed nzuri ya kuanzia na kutuma ujumbe mzito, loud and clear kwa mawaziri wengine wote kuwa, yeye sio mtu wa mchezo mchezo, alichokifanya Kangi, ndicho kinachotakiwa kufanywa na mawaziri wengine wote. Akisema hataki mchezo mchezo, ni hataki mchezo mchezo na hatanii!, ukiambiwa kikao saa 4:00 wewe njoo saa 3:30, hata kama kumetokea dharura ya msiba nyumbani kwako, acha tuu kwanza hiyo maiti, itasubiri, au kama ni mgonjwa, acha tuu afe kwa kanuni ya ikibidi punda kufa, ache punda afe, lakini mzigo ufike.

Yale mambo ya nitajieleza ni kwa wizara za kiraia, kwa wizara za kijeshi, mambo ni ya kijeshi jeshi, ni amri tuu!. Sasa inapotokea Koplo wa polisi, akapewa wadhifa wa kupigiwa saluti na IGP...
kiukweli "watapata taabu sana"!.

P
Ujumbe sahihi huo Paskali. Katika mambo makubwa anayoyafanya Rais Magufuli ni kulirudisha Taifa kwenye utawala wa sheria na watu wake kufanya kazi kwa umakini na misingi ya kazi husika. Kwamba Tanzania ya wachuuzi na wapiga dili, wa kufanya mambo ili yaende, imepitwa na wakati.

Wahenga walinena Usione vinaelea vimeundwa. Kesho Tanzania itakuwa tofauti kabisa na Tanzania ya sasa ya kuilaumu Serikali. Itakuwa Tanzania ya watu wachapa kazi, wawajibikaji, na watii sheria bila shurti.
 
Mkuu kuna mtu kanitonya sasa hivi kuwa tetesi ni kuwa jamaa kajiuzulu ghafla kwa kuvunjiwa heshima kijeshi. Sasa kisiasa hilo ni pigo kubwa sana na hatari kijeshi hivyo funika kombe ni kutangaza kustaafu.
Hivi mtu anastaafu ghafla? Kwa cheo chake tungesha taarifiwa muda mrefu kuwa anastaafu.
Ha ha ha mambo mengine inabidi ucheke tu , maana , ha ha ha
 
Rais amteua Phaustine Martin Kasike kua kamishna wa Magereza,

Habari zaidi zinakuja.......

=====

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Juma Alli Malewa ambaye amestaafu.

Lazima kaomba xoz of fedheha
 
Uteuzi huu ni kumtia moyo Mhe. Kangi Lugora kwa speed nzuri ya kuanzia na kutuma ujumbe mzito, loud and clear kwa mawaziri wengine wote kuwa, yeye sio mtu wa mchezo mchezo, alichokifanya Kangi, ndicho kinachotakiwa kufanywa na mawaziri wengine wote. Akisema hataki mchezo mchezo, ni hataki mchezo mchezo na hatanii!, ukiambiwa kikao saa 4:00 wewe njoo saa 3:30, hata kama kumetokea dharura ya msiba nyumbani kwako, acha tuu kwanza hiyo maiti, itasubiri, au kama ni mgonjwa, acha tuu afe kwa kanuni ya ikibidi punda kufa, ache punda afe, lakini mzigo ufike.

Yale mambo ya nitajieleza ni kwa wizara za kiraia, kwa wizara za kijeshi, mambo ni ya kijeshi jeshi, ni amri tuu!. Sasa inapotokea Koplo wa polisi, akapewa wadhifa wa kupigiwa saluti na IGP...
kiukweli "watapata taabu sana"!.

P
Nimekuelewa, no

reasoning....?
 
Rais John Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza, Phaustine Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza kuanzia leo Jumatatu Julai 13, 2018.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema Kamishna Jenerali Kasike amechukua nafasi ya aliyekuwa Kamishna wa Magereza, Juma Malewa ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Jenerali Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga Dar es Salaam.

Julai 6, 2018 Lugola alimfukuza kikaoni Malewa kwa kosa la kuchelewa katika kikao cha kimkakati cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo.

Lugola aliagiza mlango kufungwa saa 5 kamili asubuhi wakati kikao hicho kinaanza, lakini saa 5:01 asubuhi Malewa aliingia na hapo Lugola aliwambia atoke nje.
Hata hivyo, baada ya kuzungumza na wanahabari Dk Malewa na maofisa wengine waliruhusiwa kuingia ndani ya kikao hicho.
uteuzi%2Bpic.jpg
 
Mkuu kuna mtu kanitonya sasa hivi kuwa tetesi ni kuwa jamaa kajiuzulu ghafla kwa kuvunjiwa heshima kijeshi. Sasa kisiasa hilo ni pigo kubwa sana na hatari kijeshi hivyo funika kombe ni kutangaza kustaafu.
Hivi mtu anastaafu ghafla? Kwa cheo chake tungesha taarifiwa muda mrefu kuwa anastaafu.
Tungepata CV yake kwanza,
Kazaliwa lini huyu Juma Malewa?
 
Kumtia moyo kwa vipi Pascal? dadavua! hatanii kwa vipi, what about "watu wake" like Bashite? Pascal nenda zaidi ya hapo ulipofikiria. nakutegemea wewe! Mtu mwenye double standards does not qualify kuambiwa hatanii, hatanii kwa "sio wake"! Tuliokuwa watu wazima, haya tuliyaona kwa Idd Amin, I guess you were still very young vinginevyo ungelikuwa na reference ya watu wa aina hii and well equipped with their modus operandi! !
Kuwa fair retired, at least fair to yourself, unakumbuka Kiongozi wa Uingereza aliyejiuzulu kwa kuchelewa kufika kikaoni?
 
Administrator wa website ya Magereza ulisahau kua-update site kitambo sana , Huyo aliyestaafu hatumuoni kwenye list
upload_2018-7-13_9-50-46.png

Kamishna Jenerali J.C Minja 2012-2016
Kamishna Jenerali Dkt. Juma Alli Malewa 2016-2018
Kamishna Jenerali Phaustine Martin Kasike 2018 hadi sasa
 
Kumtia moyo kwa vipi Pascal? dadavua! hatanii kwa vipi, what about "watu wake" like Bashite? Pascal nenda zaidi ya hapo ulipofikiria. nakutegemea wewe! Mtu mwenye double standards does not qualify kuambiwa hatanii, hatanii kwa "sio wake"! Tuliokuwa watu wazima, haya tuliyaona kwa Idd Amin, I guess you were still very young vinginevyo ungelikuwa na reference ya watu wa aina hii and well equipped with their modus operandi! !
Mkuu msome pasco kwa utulivu kbc utamuelewaa
 
Back
Top Bottom