Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo March 25 2017 amemteua Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kabla ya Uteuzi huo Charles Edward Kichere alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA. Charles Edward Kichere anachukua nafasi ya Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.
Nafikiri nimepitwa kitu fulani hapa, yule Katibu Mkuu wa Ikulu aliyekuwepo zamani kaenda wapi?? Nakumbuka alikuwa mjamaa fulani kutoka Iringa....