Rais Magufuli amsaidia Mzee mstaafu aliyepunjwa mafao na kulalamika kupitia gazeti

Mkuu sisi wengine ungetusaidia japo ukatuandikia hata kwa ufupi kilicho andikwa kwenye barua. Natanguliza Shukurani
Huez kusoma barua fupi namna hio
duu?? halafu sema wewe sio sisi
mana wengine tunao uwezo wa kusoma barua
nimeshangaa ...maneno.yanaonekana sawia kabisa
 
Ni jambo jema na naunga mkono jitihada zilizochukuliwa na Mh raisi katika kutatua tatizo hilo. Nafikiri hili pia litapeleka meseji kwa watendaji wanaosababisha matatizo kama hayo. Jitihada kama hizi zinapaswa kuungwa mkono na wote wanaopenda maendeleo na haki kwa wote. Kwa hili nasema Thumbs Up kwa JPM na endelea kutatua kero za watanzania wengine haswa kwa kurekebisha mifumo zaidi ili wale ambao hawapati nafasi ya kukuandikia moja kwa moja pia waondokane na kadhia kama hizi.
 
Hiyo itakuwa siyo bure, hivi kuna wazee wangapi wa aina ya huyo mzee wanaohangaikia mafao yao kwa miaka na miaka?

Bila shaka huyo mzee amepewa 'upendeleo' maalum kwa kuwa ni kada wa Sisiem......
 
Nimeisoma hiyo barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambayo sehemu ya mwisho inasomeka hivi 'Serikali inatumia nafasi hii kuvipongeza vyombo vya habari nchini vinvyojitoa na kujikita katika kusaidia kutatua changamoto za kweli za wananchi' mwisho wa kunukuu.

Sasa tumuulize swali dogo tu Mheshimiwa Rais kuwa iwapo serikali yake ya awamu ya 5 inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari nchini, iweje sasa serikali yake hiyo hiyo iiandame JF ambacho ni chombo nambari moja hapa nchini na kumfungilia mashitaka 3 mahakamani Mkurugenzi wake Mkuu Maxence Melo?

Iweje pia TCRA wakati fulani mwaka huu iliipongeza JF kwa weledi wake na kuomba mitandao mingine iige mfano wa JF na hivi sasa TCRA hiyo hiyo inaigeuzia kibao JF na kuwaona kama wahalifu wa kutisha?
 
Sijui kwa NINI wizara za Kilimo na ufugaji Tatizo la kupunjwa mafao ni sugu..Sijui ni makusudi au sijui ivi hapo watumishi hawajui watakuja na wao kustaafu?? na atakae kuja kuwashughulikia ni wengine
Wizara ya Kilimo mmezidi wasaidieni Wastaafu kupata stahiki zao..malalamiko mengi..namnafanya kukomoa wastaafu..mnajua mchango wao mkubwa walio jitolea kuleta mapinduzi ya kilimo na ufugaji hapa nchini..KWA HILI RAIS NAKUPONGEZA SANA Kwa hilo NA SIO UYO TUU WAPO WENGI vituo vya mafunzo na utafiti nchini kwamfano Uyole mbeya malalamiko yako ya kupunjwa ni ya mda mlefu..na watendaji hawalifuatilii
 
Raisi wa watu pamoja na kusaidia kitatua tatizi hilo bado kunawatu wanafanya kazi serikakini bila mikataba na wakurugenzi hawataki kutoa mikataba na kulipa pesa Kama mshara hawakipi kwa wakati wanakipa wanavyo taka,unakuta wafanyakazi wanadai muezzin 4-6 then wakitaka wanakipa mwezi mmoja,.Je serikali au wakurugenzi wasiotoa mikataba na kulipa watu kwa wakati nini lengo lao? Watu wawezi? Watu washindwe kuendesha familia zao na kuwa omba omba? Rais fuatilia katika wilaya zote licha ya kufanya uhakiki wa watumishi bado kunawatu wanateseka wako kazini miaka 8-14 hawajapewa barua ya ajira,mkataba na hata kuandikishwa katika mifuko ya kijamii,
 
Kama anataka kuwasaidia wazee wote wanao nyanyaswa kuhusu malipo yao ya uzeeni atoe namba ya simu ya kupigiwa na kuelezwa yanayowakumba atashangaa na roho yake.
Hii haikuwa na sababu hata kutangaza kutafuta sifa za bure
 
Kwa hiyo ameamua kumsaidia mstaafu mmoja mmoja badala ya kuchukua hatua zitakazopelekea wastaafu wote kuepuka uonevu huo?
 
Back
Top Bottom