Rais Magufuli ampokea rasmi Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Aelezea aliyoongea naye

Ekethocho

Member
Jul 19, 2018
99
189
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku 2 kisha atahudhuria Mkutano wa SADC



Rais Cyril Ramaphosa
Namshukuru Rais Magufuli kwa kunialika. Katika majadiliano yetu na Rais Magufuli tumejadili sekta mbalimbali za mahusiano katika nchi hizi mbili. tutampa ushirikiano mzuri Rais Magufuli na Tanzania katika kipindi hiki ambacho anaenda kuwa mwenyekiti wa SADC

Rais John Magufuli
Mazungumzo yetu na Rais Ramaphosa yalijikita katika masuala ya uchumi. Tumepongeza mafanikio yaliyojitokeza katika nyanja ya biashara na uwekezaji hapa nchini

Tanzania na Afrika ya Kusini zinauhusiano mzuri ambao umekuwepo tangu harakati za ukombozi wa Afrika urafiki wetu ulichagizwa zaidi na urafiki ulio kuwepo kati ya Baba wa Taifa letu Hayati Nyerere na Baba wa Taifa wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela

Ndugu wanahabari muda mfupi uliopita mimi na Mh. Rais Ramaphosa tumefanya mazungumzo pamoja kwanza tulifanya mazungumzo ya faragha na kisha tukazungumza rasmi mazungumzo yetu kwa ujumla yalijikita katika ushirikiano wa kiuchumi
 
Mkuu uzi una nusu saa wachangiaji ni sita tu! Ita wanaccm mchangie, au ccm imejaa wazee na watu wasiojua kutumia mtandao?
Wako bize wanafuatilia yanayojiri Ikulu kwenye video, ndiyo maana hawachangii, wewe unawashwa tu
 
Tanzania na Afrika kusini ni dugu moja, tunajuvunia kuwa marais wao wawili walishawahi kuwa na Pasi zetu za kusafiria kipindi kile katika harakati za kupigania Uhuru wao. Hivi walizirudisha??
 
Back
Top Bottom