Rais Magufuli amdhalilisha Meya wa UKAWA Manispaa ya Ilala

Mbona huko si kudhalilishwa Mkuu? Me nilijua umefanyiwa mengine!!! Kumbe Meya mzima unatafuta public sympathy....

Ajikwezae Hushuhswa, Asiyejikweza Hupandishwa....

let's be humble, piga kazi walizokutuma wananchi.

Unaweza ukawa na tatizo la kutambua mkuu! Kama hivyo vijembe ni vya jpm, nachelea kusema huyu raisi ni waccm na wanaccm na sio watz bana! Kama yeye ni raisi kuna haja gani ya kuishi kama watu wa mipasho!? Hata kama hapendi wapinzani wake. Mfano alivyosema kuhusu Makonda na Muhongo! Huo sio ustaarabu ni ulinbukeni bana! Call a spade spade, not a big spoon.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA ALIVYODHALILISHWA NA SERIKALI YA MAGUFULI

Makamanda pipozzzzz! Jana nilipokea mwaliko wa maneno kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kupitia kwa Mkurugenzi wangu Manispaa ya Ilala wakinitaka niungane nao leo (jana) kwenye ziara ya Raisi Kinýerezi kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha kufua umeme wa gesi na mvuke 240 MW (Kinyerezi II), mradi unaotarajiwa kukamilika 2018.

Nilipofika nilipokelewa na kiongozi mmoja wa protocal ambaye ananifahamu kwa kuwa tulikuwa tunasali pamoja zamani akanikabidhi kwa public relation manager wa Tanesco ambaye pia ananifahamu tangu akiwa mwandishi wa habari na mimi nikiwa mwanaharakati wa kupinga wawekezaji wa TTCL.

Kama Meya nilipangiwa kukaa jukwaa kuu la Raisi kati ya matatu ambayo mengine yalikaliwa na waheshimiwa wabunge na wawekezaji, lingine likikaliwa na wakurugenzi na viongozi wengine.

Sasa kituko kikaanza, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco akaanza kutambulisha watu walio ktk jukwaa kuu akataja karibu wote pamoja na mbunge Bona aliyekaa pamoja na mimi kwa heshima ya mbunge mwenyeji akaniruka mimi japokuwa alikwishaambiwa uwepo wangu!

Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone kitakachoendelea!

Kauli hii iliniacha hoi. Kama vile haitoshi akasema tena kwamba amemteua mchapakazi mwingine ambaye wasiopenda maendeleo wanampinga Mh. Muhongo. Ati naye atawakomesha wale waliokuwa wanapenda kukodishakodisha mitambo ya kufua umeme. Ati anampongeza kwa kuvunja bodi iliyokuwa inamshauri kukodishakodisha mitambo ya ajabuajabu.

Yote hiyo ni mipasho kwa wapinzani ambayo haikutakiwa kutoka kwenye kinywa cha Raisi. Ile ilikuwa ziara ya kiserikali siyo ya chama chake. Na madongo mengine mengi kawarushia wapinzani utafikiri akina mama wanaocharurana kwa mafumbo.

Nimejuta kwenda huko na sitakaa niende tena kwenye ziara zake kwani huko ni kufuata maudhi badala ya kufurahia maendeleo ambayo ndiyo lengo la UKAWA.

HII NCHI NI YETU WOTE SIO YA CHAMA ....SIONI KAMA MKIACHA KUHUDHURIA SHUGHULI NI SAHIHI ......NYIE NENDENI TU HUDHURIENI ILI TUWAONE WABAGUZI KWA RANGI ZAO .......PUT THEM INTO SHAME ..................

ILA NILIKUWA NAMUONA MAGUFULI KWENYE MAMBO YA KITAIFA SIO MBAGUZI KWA KUWA PIA ALIOMBA KURA ZA UPINZANI .....KAMA NI KWELI ANAKOSEA ....KIKWETE PAMOJA NA KUWA KADA MZURI ALIKUWA NA MIPAKA SANA LINAPOKUJA EVENT YA KITAIFA
 
Nafikiri kabla mtu hujacomment chochote ingekua vizur ukatafuta kwanza ukweli wa jambo nawasihi wana JF. Tuje kwenye mada ilioletwa nimejitahid kufuatilia hotuba ya raisi kuona kilichoongelewa ni cha kwel bila mafanikio ina maana huyu meya sasa kaanza kutudanganya maana maneno hayo cjayaona wala kuyasikia kwenye hotuba sasa kama meya unaweza kutudanganya hiv vip hayo mengine yenye maslahi na ilala na unainterest nayo???? Acha kutafuta kick piga kazi
Mkuu zuberi Abraham umeseme kitu cha maana sana,kwamba watu watafute kwanza ukweli wa jambo...Na ukweli wenyewe kwa sisi kama wakazi wa Jimbo la Segerea ulipo mradi wa Kinyerezi tulihamasishwa na diwani wetu ambao mradi upo eneo lake kwamba tufike kwa wingi,na diwani pamoja na mbunge wa Segerea Kaluwa pamoj na yule dada viti maalumu wa CHADEMA walituambia mradi wa umeme hauna itikadi ya vyama...Na kweli tulihudhuria kwa wingi....Lkn tulichoshuhudia ni hayo yaliyoandikwa.
Kwamba amemchagua Makonda wenye kujinyonga wakajinyonge!!Kwamba hawezi toa chakula kwa mtoto wa mke mdogo wakati wake yupo huku akimsimamisha Bonna Kaluwa...Huyo Bonna Kaluwa anajua kuwa CCM kwenye kata na mitaa Segerea haina hata nguvu hivyo anahitaji watu wa kushirikiana nae,akiiga siasa za JPM za vijembe na yeye Segerea itamshinda
 
Meya mwenyewe amekaa kihasarahara halafu anataka apewe heshima. Mtu unacheo kikubwa namna hiyo halafu unalialia hovyo kama mbwa koko. Kweli Tanzania ilipotea kabisa, enzi za nyerere meya alikua meya hasa sio wa leo hawa waganga njaa
 
Hivi unaji
Mwita wewe ni ndugu yangu lakini ni pumbavu uliyetukuka. Jana nilikuwepo hapo kinyerezi katika msafara wa Rais. Kwa nini unapotosha umma hivi!!!!!????? Mbona sisi watu wa mara hatuna tabia hizi za kishenzi Mwita!!!!!! Huyo Meya wa Ilala ulitaka Mh Rais ampakate ili kutambua uwepo wake!? Mbona ITIFAKI ilizingatiwa sana jana.
tambua kweli wewe unajua kuwa eneo la kimyerezi lipo chini ya meya wa ilala , na mbunge anakuwa chini ya mayor ambaye ndio mwenyekti wa kamati za maendeleo za jimbo la segerea na manispaa nzima? Hapo itifaki haikuzingatiwa ilibidi uwepo wa meya utambuliwe kabla ya uwepo wa mbunge? Je wajua kuwa mbunge anaweza asifanye kazi zake vizuri ikiwa mayor atakuwa na tabia kama ya rais wenu ya kubagua na hivyo bajeti kuelekezwa maeneo mengine! Acha siasa ktk maisha ya watu
 
Punguza jazba, Ndugu yangu...matusi hayasaidii wala hayajengi...Haisaidii kabisa kusema sijui huyu 'junk' au 'ana akili ndogo' na kadhalika. Halafu uwe una-edit post zako, 'Mbeya 'nadhani unamananisha 'Meya', nadhani pia 'maswala' unamananisha 'masuala'. 'Swala' ni 'ibada' na maana nyingine ni aina ya 'mnyama'. Edit pia maneno ya kiingereza, hakuna kitu kinaitwa 'brotocal'. Inawezekana ni hasira zako zinakufanya ushindwe kuweka maneno yako vizuri... Kwa maoni yangu 'Protocol' inawezekana imekiukwa...hoja yangu haihusu kamwe ukiukwaji wa protocol au la. Hoja yangu ni namna hoja hiyo ilivyowasilishwa na nani aliyewasilisha, je, aliyewasilisha hoja hiyo humu JF ni Meya au mtu mwingine? Kama ni Meya then it is a problem. Hiyo ndiyo hoja yangu.
Asante kwa kuyaona mapungufu,Siku edit post yangu...Ebu pitia post yako,jinsi ulivyo m crush mtoa mada.
Pia nashukuru kwamba umekiri kwamba protocol ilikiukwa kwa Nia ya kumdhalilisha meya.
 
Hii ya JPM ni kengele ya hatari kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani. Wakati sisi tunafikiria kujenga utaifa, kumbe Raisi wa nchi anafikiria kuijenga ccm kwa gharama ya kudhalilisha viongoxi wa upinzani.

Kwahakika raisi asiendelee kuhadaa watanzania kuwa ni raisi wa wote. Amethibitisha kuwa ni raisi wa ccm.

Kuanzia sasa tutacheza na viongozi wa serikali kadri ya muziki unaopigwa na hatutakubali kiongozi wetu yeyote adhalilishwe tena.

HII NCHI NI YETU WOTE SIO YA CHAMA ....SIONI KAMA MKIACHA KUHUDHURIA SHUGHULI NI SAHIHI ......NYIE NENDENI TU HUDHURIENI ILI TUWAONE WABAGUZI KWA RANGI ZAO .......PUT THEM INTO SHAME ..................

ILA NILIKUWA NAMUONA MAGUFULI KWENYE MAMBO YA KITAIFA SIO MBAGUZI KWA KUWA PIA ALIOMBA KURA ZA UPINZANI .....KAMA NI KWELI ANAKOSEA ....KIKWETE PAMOJA NA KUWA KADA MZURI ALIKUWA NA MIPAKA SANA LINAPOKUJA EVENT YA KITAIFA
 
Fanyeni kazi msiwe watu wa kufatilia v2 vidogvdogo hatukuwachagua kwa kaz ya kutaka kuona mnasifiwa bali kazi!!!mi nikajua umetukanwa?kumbe ni kutotajwa tu?ahgha hii haijaniingia akilin
 
HII NCHI NI YETU WOTE SIO YA CHAMA ....SIONI KAMA MKIACHA KUHUDHURIA SHUGHULI NI SAHIHI ......NYIE NENDENI TU HUDHURIENI ILI TUWAONE WABAGUZI KWA RANGI ZAO .......PUT THEM INTO SHAME ..................

ILA NILIKUWA NAMUONA MAGUFULI KWENYE MAMBO YA KITAIFA SIO MBAGUZI KWA KUWA PIA ALIOMBA KURA ZA UPINZANI .....KAMA NI KWELI ANAKOSEA ....KIKWETE PAMOJA NA KUWA KADA MZURI ALIKUWA NA MIPAKA SANA LINAPOKUJA EVENT YA KITAIFA
Kwa maoni yako ni wazi inaelekekea JK alikuwa dhaifu lakini alijitambua udhaifu wake kitu ambacho ni cha msingi sana katika maisha ya mwandadamu. i.e. 'hakuna binadamu aliye mkamilifu'.
 
Hii ya JPM ni kengele ya hatari kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani. Wakati sisi tunafikiria kujenga utaifa, kumbe Raisi wa nchi anafikiria kuijenga ccm kwa gharama ya kudhalilisha viongoxi wa upinzani.

Kwahakika raisi asiendelee kuhadaa watanzania kuwa ni raisi wa wote. Amethibitisha kuwa ni raisi wa ccm.

Kuanzia sasa tutacheza na viongozi wa serikali kadri ya muziki unaopigwa na hatutakubali kiongozi wetu yeyote adhalilishwe tena.
We Mwita acha Magu awanyooshe, mlimsumbua sana JK kwa kuwa hotoki kabila kubwa na dini yenye structures nyingi nchini! kwa propaganda za media, mlipata sapoti kubwa ya wanaharakati na makudi mbalimbali awamu ya nne. Mkamsumbua kwa maandamano na kejeli,matusi! lakini kamwe hakurudisha ubaya still aliwatreat kama wananchi wake akiwaaita ikulu kujadiliana naye mustakabali wa taifa, sasa mnadhani kila raisi ni kama JK mpole!
Kwa taarifa yenu ile propadanga machine ilokuwa inawapa support awamu ya nne,imeamua kumpa support Magufuli kwa kuwa ni mtu wao! so hata Magu achemshe vp, hawawezi kwenda kinyume naye!
just imagine ingekuwa ni JK amesema kashfa hii kuwa hawezi kutoa chakula kwambwa wakati anawatoto kipindi chake hali ingekuwaje hapa nchini! naamini ingekuwa vurugu kuanzia magazeti,wanaharakati,maandamano,mitandao hadi matamko ya maaskofu! poleni sana hii ni awamu ngumu sana kwenu. UKWELI NDO HUO
 
Huyu Mag hapendi upinzani na shida yake ni kujaribu kuumaliza kabisa jambo ambalo ni kinyume ...mipasho ya kike inapunguza hadhi yake pia aelewe kuwa kila sehemu hata kama ccm ilishinda lakini si kwa asilimia mia, bado katika kila eneo wapinzani wapo. Wantanzania bila kujali itikadi Zai wanachangia kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa hivyo wote wana haki sawa na kama halitambui hilo basi hafai kuwa kiongozi wa ngazi ya juu.....
 
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA ALIVYODHALILISHWA NA SERIKALI YA MAGUFULI

Makamanda pipozzzzz! Jana nilipokea mwaliko wa maneno kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kupitia kwa Mkurugenzi wangu Manispaa ya Ilala wakinitaka niungane nao leo (jana) kwenye ziara ya Raisi Kinýerezi kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha kufua umeme wa gesi na mvuke 240 MW (Kinyerezi II), mradi unaotarajiwa kukamilika 2018.

Nilipofika nilipokelewa na kiongozi mmoja wa protocal ambaye ananifahamu kwa kuwa tulikuwa tunasali pamoja zamani akanikabidhi kwa public relation manager wa Tanesco ambaye pia ananifahamu tangu akiwa mwandishi wa habari na mimi nikiwa mwanaharakati wa kupinga wawekezaji wa TTCL.

Kama Meya nilipangiwa kukaa jukwaa kuu la Raisi kati ya matatu ambayo mengine yalikaliwa na waheshimiwa wabunge na wawekezaji, lingine likikaliwa na wakurugenzi na viongozi wengine.

Sasa kituko kikaanza, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco akaanza kutambulisha watu walio ktk jukwaa kuu akataja karibu wote pamoja na mbunge Bona aliyekaa pamoja na mimi kwa heshima ya mbunge mwenyeji akaniruka mimi japokuwa alikwishaambiwa uwepo wangu!

Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone kitakachoendelea!

Kauli hii iliniacha hoi. Kama vile haitoshi akasema tena kwamba amemteua mchapakazi mwingine ambaye wasiopenda maendeleo wanampinga Mh. Muhongo. Ati naye atawakomesha wale waliokuwa wanapenda kukodishakodisha mitambo ya kufua umeme. Ati anampongeza kwa kuvunja bodi iliyokuwa inamshauri kukodishakodisha mitambo ya ajabuajabu.

Yote hiyo ni mipasho kwa wapinzani ambayo haikutakiwa kutoka kwenye kinywa cha Raisi. Ile ilikuwa ziara ya kiserikali siyo ya chama chake. Na madongo mengine mengi kawarushia wapinzani utafikiri akina mama wanaocharurana kwa mafumbo.

Nimejuta kwenda huko na sitakaa niende tena kwenye ziara zake kwani huko ni kufuata maudhi badala ya kufurahia maendeleo ambayo ndiyo lengo la UKAWA.
Kama ni kweli basi, Mungu amsamehe JPM maana Magu ajue anaongoza wtz wote bila kujali dini, chama au kabila kama anavyosema mwenyewe kila anapotoa hotuba yake, na ajifunze kwa wenzetu wamerekani uchaguzi ukishaisha ni mwendo wa kuijenga nchi vijembe ni wakati wa kampeni tu.

Hi lini tutaendelea ss waafrika, ni lini tutaelimika? Ajue maombi anayoyapata ni kutoka vyama vyote, wasio na vyama, waislam, wakristo, makabila yote, majimbo yote, mikoa yote na asifikiri anaweza kuishi tu kwa sababu ya makonda na zungu la hasha
 
Back
Top Bottom