Tujenge utamaduni wa kuwajenga watoto wetu kwamba jukumu la kumsomesha mtoto ni la mzazi mwenyewe hivyo tutakuwa na kizazi ambacho tayari kimejiandaa kisaikolojia kuliko hivi sasa kila siku tunawaza bure na kila awamu inakuja na mkakati wake yaani maisha yanakuwa mashakani kila siku yaani huyu elimu bure akiingia mwingine lazima tulipe. (kwa mapato gani ya serikali mpaka tusome bure, na huu mkopo sema wengi wameutafsiri vibaya hasa wale ambao hawajaanza kulipa na vichwani siasa ndio kila kitu katika mfumo wa maisha).
Kwa mfano walivyoanza kukusanya walikuwa wanamwomba mwajiri aonyeshe ushirikiano kwa kuwataja wanafunzi waliosoma kipindi cha kuanzia 1994 kisha bodi inaleta deni ofisini kila mtu aliangalie na kukubali kama ni kweli na yupo tayari kisha unaandaliwa utaratibu wa kulipa na wengi walikuwa wanalipa kati ya 30,000 mpaka 50,000 haijalishi unadaiwa shilingi ngapi, uzembe wa serikali kwa miaka iliyopita na wanufaika wenyewe kukimbiakimbia wakidhani watalipishwa laki kadhaa ndio umetufikisha hapa mpaka Bodi ikaweka kiwango cha marejesho kisipungue 8% ya mshahara wa mnufaika