Rais Magufuli alipokuwa Wizara ya Ujenzi alifanikiwa na kujijengea sifa na heshima kubwa sana. Kwenye Urais sijui anakwama wapi

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,440
Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi wetu wakati akiwa wizara ya ujenzi alitenda kazi kwa weledi mkubwa na speed ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana ktk wizara nyingine yoyote. Hii ilimjengea kuaminika na kupendwa Sana na Wananchi wengi nikiwepo Mimi binafsi.

Hii sifa ya kuaminika ndiyo iliyosababisha hata ushindi wake wa Uraisi.
Sasa hivi ktk Uraisi wake inaonekana mambo hayaendi sawa kabisa, kwa sababu kila mahali ni malalamiko hasa ya hali mbaya ya maisha, namaanisha uchumi wa watu unapukutika, ni jambo la hatari.

Wana JF Nina imani humu ndani kuna watu wenye taaluma na maono tofauti, Ebu kwa umoja wetu tumshauri Raisi wetu namna ya kurudisha ile Heshima yake na mapenzi yake kwetu Kama alivyo kuwa Waziri wa Ujenzi kwa nia njema kabisa.

Mimi binafsi ushauri wangu Muhimu kwake ni Kuhakikisha anamfukuza kazi Mkuu wa ushauri wa mambo ya Siasa

2- Kumfukuza kazi mshauri wake wa mambo ya uchumi haraka iwezekanavyo

3-Kumfukuza kazi haraka aliyemshauri kuhamia Dodoma wakati akijua kabisa bajeti hairuhusu.

4- Kumfukuza kazi na kumuweka ndani(jela)aliyemshauri kununua Ndege wakati akijua Kabisa hii biashara ni Cansa hata uipambe kwa maneno mazuri kiasi gani bado inabaki kuwa ni hasara kubwa kwa Taifa

5- Kumkamata haraka na kumfunga jela, pamoja na viboko 20 kila Siku ijayo kwa Mungu aliyemshauri kuingilia biashara ya Korosho.

6- Kuwaamuru wakuu wa Majeshi yote ya Tanzania kuwasaka popote walipo hawa Watu wanaoitwa WASIOJULIKANA. Usiku na mchana ndani ya Mwezi Mmoja wote wawe wamekamatwa. Hawa Adhabu Yao ni kupigwa Risasa Hadharani Tv Zote zikirusha live Kama alivyouwawa Osama.

Mimi Nina Imani akifanya hayo, Imani ya Wananchi inaweza kurejea. Lakini kwa hali ilivyo sasa, wananchi wamejenga majeraha makubwa sana miyoyoni Mwao, Siyo wa vyama vya upinzani Tu, wengi wanaokwazwa ni wa Ccm, na wasio na Vyama Kama Mimi. Tunataka Airudishe Nchi ktk upendo aliotuachia Baba wa Taifa ambao Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliurithi na wakauendeleza na wakamuachia JPM.
 
Raisa wetu wa sasa!
masoudkipanya_BxbvQZLgnSY.jpeg
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi wetu wakati akiwa wizara ya ujenzi alitenda kazi kwa weledi mkubwa na speed ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana ktk wizara nyingine yoyote. Hii ilimjengea kuaminika na kupendwa Sana na Wananchi wengi nikiwepo Mimi binafsi.
Ile ilikuwa kazi ya unyampara, hii aliyonayo sasa hivi ni kazi ya uongozi. Kwa mujibu wa hayati Kingunge Ngombale Mwiru(RIP) alishauri abaki kuwa mnyampara.
 
Magu ni mzuri sana akitafutiwa pesa afanye miundombinu lakini kutafuta pesa yeye mwenyewe hajui, jk alikuwa mtafutaji ndio maana magu akawa anapeta tu
Ndiyo maana moja ya ushauri wangu ni kumtimua kazi Mshauri wake wa mambo ya uchumi
 
Mimi Nina Imani kwamba yeye Kama yeye bado Ana nguvu na uwezo mkubwa, wanaomharibia ni Washauri wake
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi wetu wakati akiwa wizara ya ujenzi alitenda kazi kwa weledi mkubwa na speed ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana ktk wizara nyingine yoyote. Lakini kwa hali ilivyo sasa, wananchi wamejenga majeraha makubwa sana miyoyoni Mwao, Siyo wa vyama vya upinzani Tu, wengi wanaokwazwa ni wa Ccm, na wasio na Vyama Kama Mimi.

Ukiendesha bodaboda vizuri haina maana utaendesha gari vizuri. Ni afadhali angebaki na udereva wake wa bodaboda
 
Rais wetu ana tatizo la kuona mbele? Na ili aone mbele atumie wataalamu ili wamuelekeze kila jambo huko mbele litaleta matatizo gani la sivyo tunaenda kukwama kama taifa kwa ujumla.
 
Ebu kwa umoja wetu tumshauri Raisi wetu namna ya kurudisha ile Heshima yake na mapenzi yake kwetu

6- Kuwaamuru wakuu wa Majeshi yote ya Tanzania kuwasaka popote walipo hawa Watu wanaoitwa WASIOJULIKANA. Usiku na mchana ndani ya Mwezi Mmoja wote wawe wamekamatwa. Hawa Adhabu Yao ni kupigwa Risasa Hadharani Tv Zote zikirusha live Kama alivyouwawa Osama.

Inabidi uwe na akili ya mwendawazimu kama hadi leo hujui kwamba Wasiojulikana ni nani na wanaongozwa na nani na wamewekwa walipo na nani. Lazima utakuwa haupo hapa Tanzania. Watu walianza kutilia shaka kwa nini kesi zote zinazohusu wasiojulikana zinapata amri toka juu ya kusitishwa au visingizio vya rejareja vya polisi, kutia ndani kina Tundu Lissu, MO, Ben Saa Nane nk. Ndipo ilipokuja kudhihirika, mkuu wa kanda.....kwa amri toka juu kuwa na kikosi kisicho rasmi kufanya kazi rasmi kwa bajeti isiyo rasmi. Kwa hiyo wasiojulikana wataendelea kuwapo, na mkuu huyo wa kanda hata afanye kosa gani ataendelea kuwapo, kwa kuwa lazima awe na nafasi inayomwezesha kutekeleza majukumu yake katika kivuli hicho.

Siasa ni mchezo mchafu sana, na niliwahi kusema humu JF kwamba sioni mwanasiasa atakaeingia ufalme wa mbinguni. wengi wana mikono imejaa damu za watu.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Raisi wetu wakati akiwa wizara ya ujenzi alitenda kazi kwa weledi mkubwa na speed ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana ktk wizara nyingine yoyote. Hii ilimjengea kuaminika na kupendwa Sana na Wananchi wengi nikiwepo Mimi binafsi.

Hii sifa ya kuaminika ndiyo iliyosababisha hata ushindi wake wa Uraisi.
Sasa hivi ktk Uraisi wake inaonekana mambo hayaendi sawa kabisa, kwa sababu kila mahali ni malalamiko hasa ya hali mbaya ya maisha, namaanisha uchumi wa watu unapukutika, ni jambo la hatari.

Wana JF Nina imani humu ndani kuna watu wenye taaluma na maono tofauti, Ebu kwa umoja wetu tumshauri Raisi wetu namna ya kurudisha ile Heshima yake na mapenzi yake kwetu Kama alivyo kuwa Waziri wa Ujenzi kwa nia njema kabisa.

Mimi binafsi ushauri wangu Muhimu kwake ni Kuhakikisha anamfukuza kazi Mkuu wa ushauri wa mambo ya Siasa

2- Kumfukuza kazi mshauri wake wa mambo ya uchumi haraka iwezekanavyo

3-Kumfukuza kazi haraka aliyemshauri kuhamia Dodoma wakati akijua kabisa bajeti hairuhusu.

4- Kumfukuza kazi na kumuweka ndani(jela)aliyemshauri kununua Ndege wakati akijua Kabisa hii biashara ni Cansa hata uipambe kwa maneno mazuri kiasi gani bado inabaki kuwa ni hasara kubwa kwa Taifa

5- Kumkamata haraka na kumfunga jela, pamoja na viboko 20 kila Siku ijayo kwa Mungu aliyemshauri kuingilia biashara ya Korosho.

6- Kuwaamuru wakuu wa Majeshi yote ya Tanzania kuwasaka popote walipo hawa Watu wanaoitwa WASIOJULIKANA. Usiku na mchana ndani ya Mwezi Mmoja wote wawe wamekamatwa. Hawa Adhabu Yao ni kupigwa Risasa Hadharani Tv Zote zikirusha live Kama alivyouwawa Osama.

Mimi Nina Imani akifanya hayo, Imani ya Wananchi inaweza kurejea. Lakini kwa hali ilivyo sasa, wananchi wamejenga majeraha makubwa sana miyoyoni Mwao, Siyo wa vyama vya upinzani Tu, wengi wanaokwazwa ni wa Ccm, na wasio na Vyama Kama Mimi. Tunataka Airudishe Nchi ktk upendo aliotuachia Baba wa Taifa ambao Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliurithi na wakauendeleza na wakamuachia JPM.
Na je kwa mfano iwe labda hao washauri wote uliowataja Hawapo kwa kigezo cha kamati kuu ya central government ya kichwani kukaa na kuamua... itakuwaje Sasa?
 
Inabidi uwe na akili ya mwendawazimu kama hadi leo hujui kwamba Wasiojulikana ni nani na wanaongozwa na nani na wamewekwa walipo na nani. Lazima utakuwa haupo hapa Tanzania. watu walianza kutilia shaka kwa nini kesi zote zinazohusu wasiojulikana zinapata amri toka juu ya kusitishwa au visingizio vya rejareja vya polisi, kutia ndani kina Tundu Lissu, MO, Ben Saa Nane nk. Ndipo ilipokuja kudhihirika, mkuu wa kanda.....kwa amri toka juu kuwa na kikosi kisicho rasmi kufanya kazi rasmi kwa bajeti isiyo rasmi. Kwa hiyo wasiojulikana wataendelea kuwapo, na mkuu wa kanda hata afanye kosa gani ataendelea kuwapo, kwa kuwa lazima awe na nafasi inayomwezesha kutekeleza majukumu yake katika kivuli hicho.
Kama kuna jambo baya kabisa linalomharibia huyu kiongozi wetu ni Hawa WASIOJULIKANA . Ilitakiwa achukue maamuzi magumu mapema sana, Watanzania hawataki kabisa kusikia hii kitu WASIOJULIKANA. Kamanda alimuahidi Siku ile kuwa ishu ya Mo angempa majibu baada ya muda Mfupi, lakini naona mpaka sasa Imeshindikan.
 
Back
Top Bottom