Rais Magufuli alikabidhi Jeshi la Polisi jukumu la ulinzi Bandarini!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,844
43,317
Wasalaam wana jamvi!

Wanajamvi Leo hii Mh Rais ameagiza Jeshi la Polisi kushika jukumu la ulinzi kwenye bandari hii ni katika jitihada za kudhibiti wizi bandarini!

Mtakumbuka jukumu la ulinzi hapo nyuma lilikuwa chini ya jeshi la polisi lakini wakapewa TPA na sasa Rais ameamua kuwa jeshi la polisi liwe na jukumu ya kulinda bandari na mali zake!

Pia kule kwenye mafuta na Flow meter pia jeshi la polisi limekabidhiwa jukumu la ulinzi!

Tuzidi kumuombea Rais wetu mpendwa maana ni wazi ni chaguo la Mungu!

Chanzo: EATV HABARI
 
Polisi hawa hawa au amewaongezea mshahara?
Kama ni hawa hawa basi tumelia
Vipi kuhusu mkataba wa wale waliopita
 
Nilidhani angeweza kuweka kamera sehemu zote ambazo ni njia za kuibia na kamera ziwe access na makao makuu tra,polisi makao makuu,jeshi makao makuu ,usalama wa taifa na tpa wenyewe, ili kama mtu anataka kuiba basi itabidi ahonge hizo idara zote ambapo itakuwa ngumu
 
Nchi haina forensic experts
Nchi ipo ipo tu sijui hiyo middle income ya 2025 itafika lini
 
Back
Top Bottom