Rais Magufuli akutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki Ikulu Dar Es Salaam

SniperBoi

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,103
1,125
proxy

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Novemba, 2016 amekutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki ambapo viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu Umoja wa Afrika (AU).
Pamoja na kuzungumzia masuala yahusuyo Umoja wa Afrika, Rais Mstaafu Thabo Mbeki amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Mstaafu Thabo Mbeki pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika uongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja aliokuwa madarakani.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Thabo Mbeki kwa kumtembelea na kufanya nae mazungumzo na pia amempongeza kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Usomi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Novemba, 2016
 
Wanafiki walojawa na machuki wanakuja sasa hivi, ngoja niwaachie
 
Hivi jamani neno rais linatakiwa lianze na herufi kubwa kama lipo katikati ya sentensi? Naomba kujuzwa maana kila lilipoandikwa limeanza na herufi kubwa hata kama sio mwanzo wa sentensi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom