MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Wameongelea masuala ya umasikini na jinsi ya kupambana na changamoto za kilimo ambazo zinawakabili Watanzania zaidi ya asilimia 70.
Wameongelea masuala ya elimu kama njia ya kupambana na umasikini.
Wameongelea masuala ya sekta ya afya na masuala mtambuka afya.
Bi. Melinda Gate amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania na ameahidi kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates itaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo