Rais Magufuli akutana na Mke wa Bill Gates, Melinda Gates

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Wameongelea masuala ya umasikini na jinsi ya kupambana na changamoto za kilimo ambazo zinawakabili Watanzania zaidi ya asilimia 70.

Wameongelea masuala ya elimu kama njia ya kupambana na umasikini.

Wameongelea masuala ya sekta ya afya na masuala mtambuka afya.

Bi. Melinda Gate amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania na ameahidi kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates itaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo

MAF1.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

MAF2.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAF4.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo
 
Wameongelea masuala ya umasiki na jinsi ya kupambana na changamoto za kilimo ambazo zinawakabili Watanzania zaidi ya asilimia 70.

Hapo kwenye kilimo kagusa penyewe.Waangalie uwezekano wa kijikita zaidi kusaidia eneo hilo ambalo ndilo lina watu wengi duniani wenye uhiytaji mkubwa wa kuondokana na umaskini.

Maeneo hasa ya kilimo na ufugaji wa kisasa katika eneo dogo lenye uzalishaji mkubwa,eneo la teknolojia rahisi ya kisasa ya kilimo,UONGEZAJI THAMANI MAZAO YAWEZE Kuuzika masoko kama ya marekani ,ulaya nk,Uwezeshaji wa wataalamu wa kilimo wanaoishi vijijini kuwasaidia wakulima (MAAFISA UGANI) kielimu bora ya kilimo,Usaidizi kwenye vyuo vya kilimo na utafiti vinavyotoa wataalamu wa kilimo,
Usaidiaji akina mama wa vijijini kwenye kaya maskini kimitaji midogomidogo ya zana za kilimo pembejeo nk

Ni wakati wa wao kujikita vijijini zaidi mijini kuna unafuu fulani.
 
Mbona tafsiri inawahi sana?
Si muweke maneno ya rais kidogo na ya mama Gates?
Watu wasome ngeli jamani!
Mheshimiwa kwenye ngeli ni mweupe kama nywele za Lowassa.
Waliongea kiswahili si alisema kwenye hotuba ya kagame rwanda hatoongea tena ngeli ni kiswahili mwanzo mwenga na ndio maana tunamtuma majaliwa kuwakilisha kule
 
Angalia huyu mama ni bilionea duniani lakini ona anavyoonyesha unyenyekevu na heshima kwa raisi.Lakini UKAWA wakipata tu-posho tu twa vikao vya bunge watu hatulali siku hiyo watakavyobomoka na kutukana kuanzia raisi mpaka sie wengineo.Wana jeuri hao eti jeuri ya pesa!!!! Pesa ya kikao nayo ni ya mtu kujishebedua kuwa ana hela.

Akina mama hasa Halima MDEE umewige huyu mama
 
Hapo kwenye kilimo kagusa penyewe.Waangalie uwezekano wa kijikita zaidi kusaidia eneo hilo ambalo ndilo lina watu wengi duniani wenye uhiytaji mkubwa wa kuondokana na umaskini.

Maeneo hasa ya kilimo na ufugaji wa kisasa katika eneo dogo lenye uzalishaji mkubwa,eneo la teknolojia rahisi ya kisasa ya kilimo,UONGEZAJI THAMANI MAZAO YAWEZE Kuuzika masoko kama ya marekani ,ulaya nk,Uwezeshaji wa wataalamu wa kilimo wanaoishi vijijini kuwasaidia wakulima (MAAFISA UGANI) kielimu bora ya kilimo,Usaidizi kwenye vyuo vya kilimo na utafiti vinavyotoa wataalamu wa kilimo,
Usaidiaji akina mama wa vijijini kwenye kaya maskini kimitaji midogomidogo ya zana za kilimo pembejeo nk

Ni wakati wa wao kujikita vijijini zaidi mijini kuna unafuu fulani.
Wakati fulani ulidai hatuhutaji msaada wowote aidha makusanyo ya kodi kiasi cha trillion moja yanatutosha,ingawa nusu yake Ni mishahara na robo moja inalipa madeni.
Yaelekea umeeanza kubadili midundo
Hongera
 
Hapo UKAWA roho zao zipo papu, papu, papu

Acha tu mkuu.Kama akina mama wa UKAWA watakuwa wivu umewajaa roho zinawauma hadi basi kuona mwanake mwenzao mama Melinda kaolewa na mwanaume tajiri kuliko wote duniani.

Wao wakijiangalia wanaona hadi hasira zinawapanda.

Ndio maana hawaji hapa kuchangia.WIVU UNAWASUMBUA.Mwenzenu ndio hivyo kapata msilie sana wivu ndio hali ya dunia.
 
Hahahahahaaaaaaaa! Wapi kasema kuwa hatutaki misaada? Hatutaki misaada yenye mmasharti kama kukubali ndoa za jinsia moja
Mkuu haikuwa suala la ushoga

Sababu ilikuwa ni kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu

Sasa hivi tungekuwa tunatembea kwenye nchi ya ahad chini ya mikono salama ya lowasa na maalim seif
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom