Rais Magufuli aiagiza Wizara ya Nishati kumrejesha kazini mara moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dkt. James Mataragio

Si

Ni hivi, dkt matarajio aliletwa nchini na JK, baada ya kina muhongo kusema kuna mchapakazi namfahamu yupo U.S.A!

Kijana wa watu alitoa tender kwenye kampuni ambayo alikuwa anawajua wapo vizuri kwa kazi, na kwa bei ndogo!

Alikataa tender ya waliokuwa wamependekeza, akasema anawajua hawana utaalamu huo, na bei zao zilikuwa juu! Kama kawaida ya mibongo, ilivyoona kakataa, ikaunda jungu kuwa kapatia kampuni tenda kinyume na sheria za PPRA!

Kijana wa kwetu majimoto MARA yakamkuta! Ila hana hamu nao!
NI BUSAWE SIO MAJIMOTO
 
2016 wameonewa wengi sana kwa kuwa kipindi kile Rais alikuwa na Mzuka sana lakin angalau sasa kaelewa kuwa pia kuna watu walichomekewa watimuliwe na kusimamishwa wakat walikuwa watu safi

Ni Vizuri Mh. Rais akaipitia kwa weledi orodha yote ya Maafisa wakubwa waliosimamishwa 2016

Taratibu za manunuzi zikikiukwa Mwenyekti wa Tender Board anaponaje, Mkuu wa Idara ya Manunuzi anaponaje?

Karibu tena Dr Mataragio
Hoja yako naiunga mkono. Ni vizuri raisi akaipitia orodha yote ya wakuu wa mashirika waliotimuliwa ama kusmamishwa kazi kwa mzuka kunako 2015/2016. Wengi walionewa sana!
 
The dude was based in TX not OK
Sio sahihi Prof Mhongo na JK ndio walimleta na ilikuwa kwa ajili ya kuijenga TPDC akitokea oklahoma.. Siasa inatumika vibaya sana hapa kwetu refer issue ya mishahara ya wakurugenzi wa mashirika na benefits alizokuwa akipata huyu jamaa na kelele za wanasiasa wa chama chetu, jamani mnasahau mapema hivi..
 
Ok,anarejea nan alibariki kuondolewa kwake,mpaka miaka yote hiyo wataalamu wengi waliondolewa kipindi kile kwa mizuka bila fuata weledi.
 
for the first time ktk awamu hii Magufuli amenifurahisha sana, hakuna kitu kiliniuma kama Mataragio kuondolewa TPDC, najiuliza tuu yule mzee wa fitna anayekaimu ile nafasi atakuaje huko aliko? KARIBU NYUMBANI JAMES, HAKIKA SASA KUTANOGA.
Sasa amekufurahisha nini wakati ni mwenyewe ndie alimtoa Mataragiro?! June 2016 JPM anamteua Sufiani Hemed Bukurura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPDC!

August 2016, yaani miezi miwili baadae bodi ile ile inayoongozwa na yule yule aliteuliwa na JPM miezi miwili iliyopita, inamsimamisha kazi James Mataragio kwa madai ya kutoa haki ya utafutaji mafuta kwa kampuni aliyokuwa anaifanyia kazi hapo kabla! Kusimamishwa kazi huko kunafuatia kufikishwa mahakamani!

Na tangia hapo, JPM hajaacha kutangaza hadharani kwamba gas YOOOOOOOOTE tumeibiwa!!!

Yaani hadi hapo bado unashindwa kuunganisha dots, au unajifanyisha tu!!!

Bila kumung'unya maneno, JPM aliitumia tu hiyo bodi kumuondoa Mataragio, kama ambavyo hivi majuzi alivyomtumia DPP kuwaachi askari polisi ambao JPM kwa kinywa chake alitangaza hadharani kwamba ana ushahidi mkubwa unaoonesha hao polisi ni wala rushwa na walikuwa wanasindikiza dhahabu ya wizi yenye thamani ya mabilioni ya shilingi!!!

Huyo James unayemkaribisha nyumbani labda awe STUPID ndo ataendelea kubaki! So long as ameshakuwa cleared, it's a matter of time kabla hajamwaga manyanga na kusepa zake wanakoheshimu mchango wa mtu!
 
Kiufupi pssf,nssf,nhc,tba etc wapewe mabosi wenye mind set za biashara na wenye exposure hao watoto wa wakulima sijui wanyonge wafanye kazi zisizo na impacts ya kuathiri uchumi
Usipozalisha matajiri maskini watapunguaje?
Ndo Maana US kuwa na pesa ni moja ya vigezo vya kuukwa urais,hapa tunajinadi kuwa Rais wa wanyonge/masikini-Shame on us
 
Hivi wale jamaa wengine waliotajwa pamoja na Dr. Mataragio kama Head wa PMU na wengine nao hatima yao ni ipi? Ina maana kesi yao mahakamani imekufa kibudu au wataendelea kushtakiwa? na je nao watarudishwa kazini?
 
Kusikia ,kuona na kuelewa ni vitu tofauti kabisa
Sasa amekufurahisha nini wakati ni mwenyewe ndie alimtoa Mataragiro?! June 2016 JPM anamteua Sufiani Hemed Bukurura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPDC!

August 2016, yaani miezi miwili baadae bodi ile ile inayoongozwa na yule yule aliteuliwa na JPM miezi miwili iliyopita, inamsimamisha kazi James Mataragio kwa madai ya kutoa haki ya utafutaji mafuta kwa kampuni aliyokuwa anaifanyia kazi hapo kabla! Kusimamishwa kazi huko kunafuatia kufikishwa mahakamani!

Na tangia hapo, JPM hajaacha kutangaza hadharani kwamba gas YOOOOOOOOTE tumeibiwa!!!

Yaani hadi hapo bado unashindwa kuunganisha dots, au unajifanyisha tu!!!

Bila kumung'unya maneno, JPM aliitumia tu hiyo bodi kumuondoa Mataragio, kama ambavyo hivi majuzi alivyomtumia DPP kuwaachi askari polisi ambao JPM kwa kinywa chake alitangaza hadharani kwamba ana ushahidi mkubwa unaoonesha hao polisi ni wala rushwa na walikuwa wanasindikiza dhahabu ya wizi yenye thamani ya mabilioni ya shilingi!!!

Huyo James unayemkaribisha nyumbani labda awe STUPID ndo ataendelea kubaki! So long as ameshakuwa cleared, it's a matter of time kabla hajamwaga manyanga na kusepa zake wanakoheshimu mchango wa mtu!
 
Enzi hizo Magugupori anafukuza tu kila Mkurugenzi asiyempenda, kila Mkurugenzi asiyetoka Kanda ya Ziwa au asiye Msukuma, kila Mteule wa Kikwete... now the wranglings within his corrupt political party have brought him to his knees and he is made to swallow his own bitter pills!
Hii haina ukweli huyo unayemsema Dr Mataragio ni Mkurya Toka kanda ya ziwa Mkoa wa Mara Wilaya ya Serengeti
 
Anafanikisha kipi?! Huyo Mataragiro ni mwenyewe JPM ndie alimfanyia fitina; leo hii anamrudisha tena madarakani! Yaani yale yale ya kutangaza hadharani kwamba polisi walikula rushwa kusindikiza wezi wa dhahabu ya mabilioni ya shilingi lakini miezi 6 ae anamwagiza DPP kuwaachia wale wale ambao JPM aliwaita Wahujumu Uchumi na wala rushwa!

Huyu haendeshi nchi hii kwa Mazoea, mtapats taabu sana paka kumuelewa.
 
Mzee ruksa ana 93 yrs.. chochote anaongea.. hata akikutukana usimind..

Ndio hivyo tena kaongea chochote ambacho mabedui wasio itakia nchi hii mema hawapendi kukisikia. Chagua barabara tikueenzi kwa jihudi zaaako. Kwa sauti ya Makamba sr.
 
Back
Top Bottom