Rais Magufuli aiagiza TANROADS kuacha kubughudhi wamachinga Mbezi mwisho jijini Dar



Akiongea na wafanyabiashara waliosimamisha msafara wake eneo la mbezi mwisho jijini DSM muda huu Rais Magufuli ambaye pia ni DAKTARI WA FALSAFA ameagiza mamlaka zote jijini DSM hususani eneo la mbezi mwisho kuacha kuwasumbua na kuwakamatakamata wafanyabiashara ndogondogo wanaofanya biashara pembeni ya barabara. Rais Magufuli ameiagiza TANROAD KUHAKIKISHA INAACHA MARA MOJA KUWASUMBUA WAFANYABIASHARA HAO NA PIA AMEWAAGIZA WAFANYABIASHARA HAO KUTOKUFANYIA BIASHARA KATIKATI YA BARABARA KWANI KUFANYA HIVYO NI KUHATARISHA MAISHA YAO. RAIS AMEWAAGIZA WAFANYABIASHARA HAO KUFANYA BIASHARA PEMBENI YA BARABARA KWA MUDA WAKATI MAMLAKA ZA SERIKALI ZIKITAFUTA ENEO MAALUM LA KUWAPATIA KWA AJILI YA KAZI ZAO.

HATUA HII YA RAIS IMEKUJA BAADA YA WANANCHI KUUSIMAMISHA MSAFARA WA RAIS ULIOKUWA UNAPITA UKITOKEA KIBAHA MKOANI PWANI. RAIS ALITOA FURSA YA WANANCHI KUMUULIZA MASWALI NDIPO WAKAMWELEZA KERO WANAZOKUTANA NAZO WAKATI WANAFANYA BIASHARA ZAO.



Du! hii kali, msafara wa Rais unavyopitaga kasi kuna mwananchi atakayeweza kusimama barabarani na kuusimamisha!!!!! si kweli na siwezi kuamini.
 
Hili la machinga kufanya biashara bara barani na kwenye vituo vya mabasi siyo sahihi, angalia pale gerezani palivyo pa hovyo baada ya kuwaruhusu kuuzia mle bidhaa zao.
Ndo Makonda anataka Dar uwe mji wa Mfano? Mji umejaaa Vibanda vya Machinga wamezidiwa na mji wa Njombe ambao ni marufuku kufanya biashara sehemu isiyo rasmi pia ni marufuku kutengeneza vile vimeza au Vibanda vya Mbao.
 
Kimara wabomoleeni , Mwanza waacheni , huyu ndio rais wa wanyonge ? wadanganyeni wapumbavu , maana hata vijijini hamuungwi mkono , hongera Twaweza .
Tukio wanalipanga wenyewe la eti kazuiwa na wananchi? Hivi wanamdanganya nani kuwa msafara Wa Rais unazuiwa na wananchi bila ridhaa yao protoko?
Kama ni hivyo basi hata akitaka kudhuriwa ni rahisi kwani mnazuia msafara kisha mnafanya yenu.
Waache drama watu wameshtuka na wanazidi kuwadharau
 
Hili la kusimamisha msafara wa rais ngoja na mimi sikumoja nije nisikamishe msafara.
 
Siku hizi tuna majasiri wa ajabu Tanzania..wanadhubutu na kufanikiwa kusimamisha msafara wa raia namba wani.....
 
ya mwisho kwa nyie mlioko mitandaoni lakini wananchi waliopewa ruhusa ya kufanya biashara wameshangilia na kufurahia siye tunaishia kumuona mbaya kwenye mitandao tu.
Unakumbuka kipigo cha mbwakoo walichopewa wamachinga wa Mwanza? Rais kaagiza wasibughuziwe akiwa nao kasha kaagiza wakurugenzi wasiache wamachinga wakichafua miji hivyo "piga teke tuu"
We kaa unashangilia tuu!
 
wale wamama walikuwa wanaishi kimachale machale sana na kunyanyasika, afadhali!! hivi kwann pale chooni wanatoza Shs 500/= wakati sehemu zingine zote jijini ni 200/=?
Hili swala linanikera asee, jiji zima huduma ni 200 pale ni 500 kuna nini hasa maana hatupewi hata vitambaa vya kujifuta mkono au hata chochote kwa thamani hiyo ya fedha
 
msafara unavopita kwa kasi ama kweli wanaosimamisha wana moyo wa ujasiri hadi kuusimamsha ukasimama! sijui inakuwa wale wanaotangulia mbele ya mkuu hivi nao wanarudi au?
 
Back
Top Bottom