Mkuu tunafahamu sote kuwa isingewezekana wote wawe wakulima, kwani imeandikwa wapi inchi hii kwamba wafanyabiashara wanyanyasike au kuwa hawaruhusiwi kuuza korosho?Korosho bado tunahakiki inakuwaje mtu ana tani za korosho afu hana hata hatua 1 ya Ardhi!
Mkuu ebu ainisha kwa mifano anuai hizo biashara ambazo zilitegemea mafisadi. Umejaribu kutumia elimu yako japo kidogo kujua effect ya serikari kuhamishia pesa zake zote BOT?Tulikuwa tunajua tangu mapema biashara zilizokuwa zinategemea mafisadi na money launderers lazima zife. Mkuu tulia dawa ikuingie ili upone ugonjwa wa kifisadi
Ndugu mjumbe kuna mmoja amenifuata inbox akaniambia tatizo mkulu ni mkali kias kwamba mtu anaogopa atoeje ushauri, kama hivi ndivyo, ni kwa nini 2020 kwenye kura watu wasiache unafiki wa kufa kijerumani na tai shingoni achaguliwe mtu mwingine?Bado naamini Kama Raisi Magufuli tukimuambia ukweli wa mambo (akatusikiliza) na tukaacha kumpotosha (naamini wanampotosha) Kwa spirit aliyo nayo, Kuna uwezekano wa yeye kuwa Raisi bora kabisa kuwahi kutokea duniani.
Hicho kipande hicho, huo Ukweli unaousema ataambiwa na nani? Ataambiwaje?
Nawaza kwa sauti zaid ya unavyofikiria ndugu m/kiti
Hahahaa mkuu na wewe ni muhanga? Hivi nataka kufahamu, serikali ni kweli kabisa ilijua siku zote wakulima ndo huwa wanauza korosho Vietnam? Mbona mpaka mashuleni tunafundishwa middlemen huwa wapo?Walanguaji tumeula wa chuya japo ilikua ni biashara halali kipindi cha nyuma na na ilikua inaingiza kipato kwa kijiji husika
Ndio maana nikauliza, ashauriwe nini na nani Amshauri!Ndugu mjumbe kuna mmoja amenifuata inbox akaniambia tatizo mkulu ni mkali kias kwamba mtu anaogopa atoeje ushauri, kama hivi ndivyo, ni kwa nini 2020 kwenye kura watu wasiache unafiki wa kufa kijerumani na tai shingoni achaguliwe mtu mwingine?
Maendeleo siku zote yamekuja kwa kupingana kimawazo na kupata wazo moja bora na linatekelezwa, natamani watu waje na mawazo mbadala hapa tujadili kwa hoja kwa kuwa najua hakuna anayejua kila kituTukiacha unafiki wa jibu "NDIYO MKUU" naamini ataweza kubadilika
Duniani kote pesa za serikali hukaa Central Bank na wala si Commercial Banks ilikuwa TZ pekee ambako pesa za serikali zilikuwa zinakaa kwenye Commercial Banks ambapo hizo hizo Commercial Banks zinakwenda kuchukua mikopo BOT kwa kutumia pesa za serikali huu ulikuwa ujinga uliopitiliza ndiyo maana Kenya na India walikuwa wauzaji wa Tanzanite kuliko TZ huo nao ni ujinga uliopitiliza kiasi cha hali ya juu! Sasa amekuja mwanaume wa shoka amewanyoosha ni lazima mtalalamika tu kwa sababu nyinyi mlikuwa wanufaikaji wa mfumo huo wa kifisadi. Kwa waelewa wote wanajua Mh. Rais Magufuli anafanyakazi kubwa sana na atakuwa na wapingaji kama nyinyi lakini tunajua ataendelea kuwanyooka kwa kuwa watz walio wengi wako nyuma yake wanamuunga mkono.Mkuu ebu ainisha kwa mifano anuai hizo biashara ambazo zilitegemea mafisadi. Umejaribu kutumia elimu yako japo kidogo kujua effect ya serikari kuhamishia pesa zake zote BOT?
Aisee !! kwa uandishi wa namna hii halafu unasema umesoma NIT?Ukweli wakati fulani tuwe wa kweli nchi kama zetu hizi kuwa na maendeleo inatakiwa RAIS azibe sikio au hatanya kitu chochote kile ya maendeleo. Awamu zote zimepita lakini cha muhimu hatukuona , umeme hakuna ,bandari ni shida, watu walipeana kazi kiundugu bila na upendendeleo, wakulima wamekuwa wakinyanyaswa sana, wenyeviti wa kamati za bunge walipewa hadi rushwa ya mahama au V8 magari, hawasuluhishi kero, nk Mie sina kazi tokea nimemaliza chuo cha NIT mwaka 2008 hadi maksi walikuwa wanapeana kikabila na kwa ki rushwa lakini kidogo tumepata RAIS anayerekebisha kidogo,hata kama sina kazi hivyo bora, na tofauti na wengine waliomtangulia. Tumwache aendelee, heti tumwache abishane na wehu wanaogombania kahaba kama akina Wema sepetu, .Binadamu si kama kinyonga.
Point kubwa kwakoMkuu, umeongea POINT kubwa lakini kuna watu lazima wakupinge tu.
Aisee !! kwa uandishi wa namna hii halafu unasema umesoma NIT?
Yaani uandishi wako na msimamo wako ni sahihi kabisa.
Nikwambie tu kuwa huyu mheshimiwa kuna mambo machache sana amefanya vizuri lakini mambo aliyoyaharibu ni mengi kuliko hayo machache aliyofanya vizuri...
Excellent kabisa hii kituWanabodi nawasalimu sana .
Nitaenda moja kwa moja kwenye maada.
Ndugu zangu, Tangu utawala huu wa awamu ya tano uingie madarakani, tumeshuhudia mabadiliko mengi kimfumo na kiutendaji ambayo majawabu yake nayo yamekuwa mengi. Mimi sitapongeza juhudi yoyote iliyofanywa na mheshimiwa kwa kuwa hata wanaompongeza ama wanamsanifu ili au ugali wao uwe salama ama hawajui watendalo. Hata hivyo mimi siyo mwana siasa, wala siijui siasa, Haya noyoanika ni maoni yangu tu.
Ni katika kipindi hiki pekee tumeshuhudia benki nying zikifilisika na kufungwa, na kufuatia tamko la Gavana wa BOT kuna benki nyingine zinaenda kupata pigo la kufyekelewa mbali kwa kuwa zinaelekea kukosa uwezo wa kujiongoza. Ikumbukwe kuwa hizi benki zimeajiri wafanya kazi na ukizifuta maana yake hawa watu watarudi mtaani.
Mazingira ya biashara yanakuwa magumu kila kukicha, Na leo nadhani sote tumshuhudia mambo ya FastJet Tanzania, hii inamaana wafanyakazi wake nao including Masha, wanarudi bench. Mobisol Tanzania nayo imefanya Retrenchment na karibu watumishi 106 wameaga mashindano, Hapo hatujazungumzia habari ya Vodacom Tanzania na Tanzania Breweries, hapo hapo tusisahau kujiuliza hatma ya watumishi wa viwanda na magazeti yaliyofungiwa kwa sababu za makosa ya kisiasa.
Kauli mbiu ya wapiga dili imepamba moto bila kufikiria sana, kwa sababu hawa wanaokosa kazi wakielezea ukosefu wa fedha wataitwa walikuwa wapiga deal na kibwagizo cha kuhakikisha waliokuwa wakiishi kama malaika sasa wataishi kama mashetani.
SASA
Katika hali ya kawaida, wengi wanaokosa kazi wangetaarajiwa wachukue akiba zao kutoka mifuko ya jamii ili wakapambane mtaani, kwa bahati mbaya kwa sasa haiwezekani maana serikali ya CCM imetunga sheria inayozuia kuchukua pesa hizo, Ikitokea mtu akapata chanzo kingine akafungua biashara anaenda kukutanza na utitiri wa kodi kiasi kwamba hakuna tena liwezekanalo juu ya nchi. Kamishna wa TRA ameonge kuwa wanaanza kutoza kodi kwa wale wanaofanya biashara mtandaoni, yaani wale wanouza mkongolaa wajiandae kisaikolojia.
Mheshimiwa Raisi Bado anaamini kabisa uchumi unakuwa kwa kasi, sasa swali la kujiuliza, Je, ni kweli Raisi anaamini uchumi wetu unakuwa kwa kasi au? Kama anadhani saivi maisha ni mazuri, ni nani amemdanganya? Tumeshuhudia Gavana wa BOT akitoa kauli kwamba tunazo fedha za kutosha kabisa, Lakini waziri mpango akatoka kwa dhati na kusema kuwa nchi inapitia katika kipindi kigumu sana maana hamna fedha.
Swali, Ni nani amemdanganya raisi kati ya Waziri wa Fedha na Gavana wa BOT?
Hivi ni kweli nchi yenye fedha za kutosha inapitia wakati mgumu? Mimi nadhani tujikumbushe kidogo, Mwalimu Nyerere alipata kusema na nanukuu, "You cant develop people, you must allow them to develop themselves" kwa tafsiri isiyo rasmi "Huwezi kuendeleza watu, lazima uwaruhusu wajiendeleze".
Kwa bahati nzuri Mheshimiwa Raisi ameweka wasomi wengi kwenye uongozi, maana yake wamshauri kisomi, tuna Maprofesa wengi wa uchumi ambao ninaamini wangemueleza ukweli bila kuogopa kutumbuliwa, hii nguvu kubwa anayoitumia ingelenga eneo sahihi basi tungetatua tatizo. Nimesikitishwa sana na tamko la bwana mdogo Augustino Matefu kule kigoma eti Zitto anamroga sana, Ningekuwa na mamlaka ningemfukuza mara moja maana vijana wameaminiwa halafu wanaenda kufanya siasa za kijinga sana.
Siasa inatakiwa itumikie uchumi na siyo Uchumi utumikie siasa, Najiuliza elimu za wabunge wetu, tunao wengi mle hawana elimu lakini wanavyoshupaza mashingo na kuamu masuala makubwa ya kiuchumi nabaki mdomo wazi, IFIKIE MAHALA WABUNGE WANAPOAMUA MASWALA MUHIMU WAACHE VYAMA VYAO PEMBENI, WASIMAME PAMOJA KAMA TAIFA, tuliwachagua wakajenge nchi na siyo kuibomoa, Kuna matamko ndiyo yeametolewa na EU na MAREKANI, Haya matamko siyo mazuri, na nadhani badala ya upande mwingine kufurahia na kukejeli, ni muda wa kukaa pamoja na kujadili kwa hoja na kuangalia njia nzuri ya sisi kujinasua kwenye mtego huu wa wzungu maana mabavu hayajengi.
Kama mheshimiwa Raisi atafanikiwa kuona uzi huu ninamshauri afanye yafuatayo.
Mwisho, Kwa afya ya siasa katika nchi Duniani kote kwa sasa, Upinzani ulio huru ni muhimu tuwe tunataka au hatutaki, Hii hutoa fursa ya watu kubishana kwa hoja na kuwapa fursa wananchi kuchagua vyema ni nani anafaa. Huu mswaada wa vyama vya siasa, Nikiri tu kwamba tunafanya makosa maana kiukweli hauleti afya kwa siasa zetu kwa sasa, Uondolewe haraka, Nasema hivi kwa kuwa hii ikipita, udikteta utaonekana wazi wazi kabisa (Mheshimiwa Raisi usiingie kwenye mtego huu)
- Awaite wachumi wote wakae mezani, wachambue muenendo wa uchumi wetu kwa sasa na baadae waje na ripoti ya hali halisi ya uchumi na njia mbadala za kuhakikisha tunakuwa na uchumi unaokua Kiuhalisia na siyo kinadhalia
- Aanze kufuatilia matamkona matendo ya wateule wake juu ya wapinzani na watendaji mbalimbali hapa nchini maana nin uhakika hawa watu wanatoa matamko na wengine kufanya lolote ili wajifiche humo na kumdanganya Raisi juu ya utendaji wao.
- Aongeze wigo wa watu kutoa maoni maana kwenye maoni ya wengi atapata ukweli halisi wa mambo iwe kisiasa au kiuchumi.
Bado naamini Kama Raisi Magufuli tukimuambia ukweli wa mambo (akatusikiliza) na tukaacha kumpotosha (naamini wanampotosha) Kwa spirit aliyo nayo, Kuna uwezekano wa yeye kuwa Raisi bora kabisa kuwahi kutokea duniani.
TUSIMPOTOSHE RAISI WETU, TUMSAIDIE, TUSIGOMBANE NAYE
"We are not against the progress, but we do not want progress that is anarchic and criminally neglects the rights of others" Thomas Sankara.
Deus iudex est solus
Kidudu
CC GENTAMYCINE VUTA-NKUVUTE Mshana Jr Mshanajr MSAGA SUMU et al.
Ukweli wakati fulani tuwe wa kweli nchi kama zetu hizi kuwa na maendeleo inatakiwa RAIS azibe sikio au hatanya kitu chochote kile ya maendeleo. Awamu zote zimepita lakini cha muhimu hatukuona , umeme hakuna ,bandari ni shida, watu walipeana kazi kiundugu bila na upendendeleo, wakulima wamekuwa wakinyanyaswa sana, wenyeviti wa kamati za bunge walipewa hadi rushwa ya mahama au V8 magari, hawasuluhishi kero, nk Mie sina kazi tokea nimemaliza chuo cha NIT mwaka 2008 hadi maksi walikuwa wanapeana kikabila na kwa ki rushwa lakini kidogo tumepata RAIS anayerekebisha kidogo,hata kama sina kazi hivyo bora, na tofauti na wengine waliomtangulia. Tumwache aendelee, heti tumwache abishane na wehu wanaogombania kahaba kama akina Wema sepetu, .Binadamu si kama kinyonga.
Tulikuwa tunajua tangu mapema biashara zilizokuwa zinategemea mafisadi na money launderers lazima zife. Mkuu tulia dawa ikuingie ili upone ugonjwa wa kifisadi