Rais Magufuli aagiza kubomolewa kwa Makao Makuu ya TANESCO na Wizara ya Maji, kupisha ujenzi wa barabara Ubungo

Kama walikiuka sheria libomolewe tu, uchungu wa kulibomoa jengo la TANESCO hauwezi kuufikia ule wa kubomolewa nyumba niliyokuwa na mimi nilijenga kwenye reserve road! Sheria ichukue mkondo wake tu.
 
Na ilipofika saa tisa alisema ninaona kiu na wakamletea siki iyokuwa kwenye sifongo nae alipokwisha kuionja alisema yeloi yeloi lama sabakitani akakata roho mara giza likatanda na pazia la hekaluni likapasuka katikati ....mechi imeisha na refa keshapuliza kipyenga cha mwisho..
 
Mi nauliza tu daladala za kuingia simu2000 kutokea tabata mbona sioni mchoro wake au tutashukia darajani kama uhuni kwa kushukia simu2000 kuzurura mpaka ubungo terminal? imagine mwenge mataa na mapipa pamefunga jam hilo daraja litakuwa parking
 
Kule Mbele .Wenzetu huwa wanafanya haya
images (2).jpeg
images.jpeg
 
51B zingetosha kurudisha wazururaji wote shambani jam ikapungua na jiji likabaki safi. Kupanga ni kuchagua
 
Kama walikiuka sheria libomolewe tu, uchungu wa kulibomoa jengo la TANESCO hauwezi kuufikia ule wa kubomolewa nyumba niliyokuwa na mimi nilijenga kwenye reserve road! Sheria ichukue mkondo wake tu.
Halafu utakatwa tena kodi lijengwe lingine au unadhani hiyo ofisi wafanyakazi watakaa nje kama wewe
 
Halafu utakatwa tena kodi lijengwe lingine au unadhani hiyo ofisi wafanyakazi watakaa nje kama wewe
Unadhani wakianzisha kodi nyingine hata kama hilo jengo lipo nitaweza kuwazuia, acha wanikate!
 
Ndiyo matatizo ya kuwasukumizia watu wa ajabu ajabu Ikulu. Kikwete alimkatalia huyu kuvunja hilo jengo sasa anataka kulipiza kisasi. Asset ya mabilioni ya pesa inapotea hivi hivi ndani ya vitabu vya PPF.

Janeth Magufuli ubarikiwe sana wangekusikiliza huyu janga kubwa la Taifa asingetia mguu Ikulu.

View attachment 631231

Rais Magufuli leo atembelea Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu za Ubungo unajulikana kama ‘Ubungo Interchange’.
View attachment 631271

Aidha meagiza kuwa jengo la makao makuu ya Shirika la Uzalishaji na Ugavi wa Umeme nchini TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha mradi huo.
View attachment 631217
Hapa chini ni ramani ya Barabara ya juu ambayo itajengwa Ubungo Dar es Salaam
View attachment 631218
Barabara ya Morogoro ya Chini kwa magari yanayotokea Kimara Kwenda Mjini
View attachment 631219
Barabara ya juu kwa watu wanaotokea barabara ya Sam Nujoma kuelekea barabara ya Nelson Mandela uelekeo wa Buguruni

Mijadala mingine kuhusu hili jengo soma;

Magufuli! Jengo la TANESCO Ubungo ni kisiki na udhaifu mwingine kwake?

Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara

Jengo la Makao Makuu ya TANESCO Ubungo kubomolewa wakati wowote kupisha ujenzi wa 'Interchange'

JENGO LA TANESCO NA FLYOVERS, which one's more important?

Magufuli, nakuombea upate Urais na uanze na TANESCO
 
Unajua kwa muda mrefu serikali zimehangaika kuboresha makazi kwa kuangalia zaidi physical aspects peke yake...

Ila ukitaka mji mzuri ung'ae mpk ukome, boresha hali zawatu.. Ni improved livelihood tu ndio inaleta maendeleo... Mfano kariakoo manzese na Magomeni zinaendelea kunadilika kwa kuwa vipato vya watu vinaendelea kuboreka... Image ya mji inakuja na hali bora za maisha ya watu wake.. Hiyo ndio sustainable development...

Kuvunja jengo ni kukosa ubunifu kwa hao.mainjinia.. Unafanya kazi kwa ubunifu katika mazingira yaliyopo... Cost - Benefit Analysis ni muhimu katika miradi.. Ninauhakika re-designing cost za kipande hicho ni ndogo sana ukilinganisha na Gharama na thamani ya jengo, Gharama za Uvunjaji, Disposal ya Kifusi, ukiachilia mbali gharama za kuhamisha ofisi za serikali na convenience costs zinazotokana na kubadilisha huko.

Word
 
Hivi jengo la tanesco linavunja ni maamuzi ya kikao cha baraza la mawaziri
 
Umeandika vizuri sana Mkuu, lakini unapokuwa na uchwara anayeongoza nchi na wale washauri wake na subordinates wanamuogopa kuliko wanavyomuogopa Mungu wao haya ndiyo matokeo yake. Ukurupukaji mbele kwa mbele mwanzo mwisho.

Unajua kwa muda mrefu serikali zimehangaika kuboresha makazi kwa kuangalia zaidi physical aspects peke yake...

Ila ukitaka mji mzuri ung'ae mpk ukome, boresha hali zawatu.. Ni improved livelihood tu ndio inaleta maendeleo... Mfano kariakoo manzese na Magomeni zinaendelea kubadilika kwa kuwa vipato vya watu vinaendelea kuboreka... Image ya mji inakuja na hali bora za maisha ya watu wake.. Hiyo ndio sustainable development...

Kuvunja jengo ni kukosa ubunifu kwa hao.mainjinia.. Unafanya kazi kwa ubunifu katika mazingira yaliyopo... Cost - Benefit Analysis ni muhimu katika miradi.. Ninauhakika re-designing cost za kipande hicho ni ndogo sana ukilinganisha na Gharama na thamani ya jengo, Gharama za Uvunjaji, Disposal ya Kifusi, ukiachilia mbali gharama za kuhamisha ofisi za serikali na convenience costs zinazotokana na kubadilisha huko.
 
Hapa Ni maneno matstu tu
Bomoa. Hahaaa sasa hapo ndo kashesge. Kubomoa Ni rahisi kuliko kujenga
 
Back
Top Bottom