Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Ni muhimu tuelewane; Baadhi ya Wabunge hasa wa upinzani kuipinga Bajeti ya JPM sio kwamba wanayakataa Maendeleo ya Wananchi, bali huwa wanafanya hivyo ili kuitaka Serikali kufanya Marekebisho ya Msingi kwenye Bajeti husika inayokuwa inapendekezwa Bungeni ili iwe Bajeti itakayowasaidia Wananchi kukabiliana na hali ngumu za Maisha yao, badala ya kupitisha Bajeti inayokwenda kufanya mambo ya hovyo kama haya ya kununua Viongozi wa upinzani ama haya ya kununua Ma-Bombadier na kufanya vitu vingine vya hovyo bila kufuata na kuzingatia Kanuni na taratibu za Matumizi ya Fedha za Watu.
Serikali inaposhindwa kufanya Marekebisho ya Msingi kwa maslahi mapana ya Wananchi wa hali za chini wanaohitaji Huduma za Afya kama vile Dawa, Barabara na Maji ya kunywa, inakuwa vigumu kwa Wabunge wa upinzani kuwa sehemu ya Bajeti hiyo ili kuepuka kuwa "Mhuri" wa kuhalalisha Bajeti haramu ambayo haina msaada kwa Wananchi wa hali za chini hasa walioko maeneo ya Mijini na Vijijini.
Aidha, Wapinzani wanapoipinga Bajeti ya mwaka husika huwa wanatoa sababu za Msingi na ni kwa bahati nzuri huwa wanaueleza umma juu ya kwa nini wameipinga Bajeti ama ni kwa nini wamesusia mjadala wa Bajeti ya mwaka husika. Na mara zote, Watanzania wamekuwa wakiwaelewa vizuri sana hawa wapinzani tofauti na JPM anavyofikiri na kutaka kuwapotosha.
Ni kwa bahati mbaya sana, Rais anayewalaumu Wabunge wa upinzani kuzipinga Bajeti zake, yeye na Serikali yake, hawajawahi kujibu hoja za wapinzani dhidi ya sababu zao za kuzipinga Bajeti zake ambazo mara zote zimeonekana kuwa hewa kutokana na kuwa na maandalizi ya hovyo yasiyo na tija kwa Wananchi.
Mara zote Watanzania wameshuhudia kuona Bajeti za Serikali hii ya awamu ya tano zikikiuka Kanuni na taratibu za Matumizi ya fedha za Umma; Mfano; Hadi leo hii, Wananchi wanahoji kuhusu fedha zinazojenga Uwanja wa Ndege wa Chato zilipitishwa na Bajeti ya mwaka upi na lini licha ya Serikali hii inayojiita ya Magufuli kuwa na Matumizi mabaya ya fedha za Umma yasiyofuata taratibu za Fedha.
Aidha, Wananchi wanashuhudia aibu na kashifa nzito ya upotevu wa fedha za kodi zao kiasi cha 1.5Trillioni sawa na Billioni 1500 ambazo hadi leo haijulikani ziko wapi na zilifanya nini. Haya yote na mengine mengi, ni moja ya Matumizi mabaya ya Fedha za Watu yasiyofuata wala kuzingatia taratibu za Kisheria ambazo mara zote Wabunge wa upinzani wamekuwa wakizipigia kelele Bungeni hata kufikia kupinga na kususia mijadala ya Bajeti husika.
Naomba niwasilishe kwenu japo kwa ufupi!