Rais Magufuli aache kupotosha wananchi

Rais Magufuli aache kupotosha wananchi

Hauhitaji hata kufika darasa la saba kujua hii concept ya kupinga bajeti
Ukipinga bajeti ni sawa na kukataa maendeleo,ndio mana kuna bajeti kivuli kuonesha kuwa hamkubaliani na bajeti ya serikali,lakini kuikataa mana yake hata nyie hamtaki kulipwa
Rais yupo sahihi
Hupumuliwi kichogoni lakini wewe
 
Bajeti iliyopitishwa n wengi ni halali. Jee hao wabunge wa upinzani waliopinga bajeti bungeni, na leo wanomba fungu lao, wanaomba wapewe bajeti haramu ni sawa.

Jana ilikuwa haramu lakini leo halali
 
Ni muhimu tuelewane; Baadhi ya Wabunge hasa wa upinzani kuipinga Bajeti ya JPM sio kwamba wanayakataa Maendeleo ya Wananchi, bali huwa wanafanya hivyo ili kuitaka Serikali kufanya Marekebisho ya Msingi kwenye Bajeti husika inayokuwa inapendekezwa Bungeni ili iwe Bajeti itakayowasaidia Wananchi kukabiliana na hali ngumu za Maisha yao, badala ya kupitisha Bajeti inayokwenda kufanya mambo ya hovyo kama haya ya kununua Viongozi wa upinzani ama haya ya kununua Ma-Bombadier na kufanya vitu vingine vya hovyo bila kufuata na kuzingatia Kanuni na taratibu za Matumizi ya Fedha za Watu.

Serikali inaposhindwa kufanya Marekebisho ya Msingi kwa maslahi mapana ya Wananchi wa hali za chini wanaohitaji Huduma za Afya kama vile Dawa, Barabara na Maji ya kunywa, inakuwa vigumu kwa Wabunge wa upinzani kuwa sehemu ya Bajeti hiyo ili kuepuka kuwa "Mhuri" wa kuhalalisha Bajeti haramu ambayo haina msaada kwa Wananchi wa hali za chini hasa walioko maeneo ya Mijini na Vijijini.

Aidha, Wapinzani wanapoipinga Bajeti ya mwaka husika huwa wanatoa sababu za Msingi na ni kwa bahati nzuri huwa wanaueleza umma juu ya kwa nini wameipinga Bajeti ama ni kwa nini wamesusia mjadala wa Bajeti ya mwaka husika. Na mara zote, Watanzania wamekuwa wakiwaelewa vizuri sana hawa wapinzani tofauti na JPM anavyofikiri na kutaka kuwapotosha.

Ni kwa bahati mbaya sana, Rais anayewalaumu Wabunge wa upinzani kuzipinga Bajeti zake, yeye na Serikali yake, hawajawahi kujibu hoja za wapinzani dhidi ya sababu zao za kuzipinga Bajeti zake ambazo mara zote zimeonekana kuwa hewa kutokana na kuwa na maandalizi ya hovyo yasiyo na tija kwa Wananchi.

Mara zote Watanzania wameshuhudia kuona Bajeti za Serikali hii ya awamu ya tano zikikiuka Kanuni na taratibu za Matumizi ya fedha za Umma; Mfano; Hadi leo hii, Wananchi wanahoji kuhusu fedha zinazojenga Uwanja wa Ndege wa Chato zilipitishwa na Bajeti ya mwaka upi na lini licha ya Serikali hii inayojiita ya Magufuli kuwa na Matumizi mabaya ya fedha za Umma yasiyofuata taratibu za Fedha.

Aidha, Wananchi wanashuhudia aibu na kashifa nzito ya upotevu wa fedha za kodi zao kiasi cha 1.5Trillioni sawa na Billioni 1500 ambazo hadi leo haijulikani ziko wapi na zilifanya nini. Haya yote na mengine mengi, ni moja ya Matumizi mabaya ya Fedha za Watu yasiyofuata wala kuzingatia taratibu za Kisheria ambazo mara zote Wabunge wa upinzani wamekuwa wakizipigia kelele Bungeni hata kufikia kupinga na kususia mijadala ya Bajeti husika.

Naomba niwasilishe kwenu japo kwa ufupi!
Wewe au cdm mtaani kwenu mmefanya kipi zaidi ya majungu?
 
Hauhitaji hata kufika darasa la saba kujua hii concept ya kupinga bajeti
Ukipinga bajeti ni sawa na kukataa maendeleo,ndio mana kuna bajeti kivuli kuonesha kuwa hamkubaliani na bajeti ya serikali,lakini kuikataa mana yake hata nyie hamtaki kulipwa
Rais yupo sahihi

Acha unafiki ww, kupinga bajeti ya serikali ni moja ya demokrasia kuonyesha kwamba ww una yako ambayo ni bora zaidi. Kama ni kuunga mkono tu, huyo Magufuli yuko bungreni zaidi ya miaka 20 na wakati huo ndio nchi iliingia mikataba mingi ya wizi huku wapinzani wakipinga mikataba hiyo, ambayo leo Magufuli anataka asifiwe kwamba anarekebisha. Je wakati ule alikaa kimya kwanini asiwaunge mkono wapinzani mpaka tumepigwa ndio atekeleze hayo hayo ya wapinzani.

Leo Magufuli anatekeleza elimu bure, lakini wapinzani walihubiti hili kwa nguvu kubwa hiyo 2010 na ndani ya bunge, huku Magufuli na ccm yake wakisema haiwezekani. Mbona hakujitokeza aunge mkono, ni kwamba hakutaka wanafunzi masikini wasome? Ni hivi, Magufuli hawezi siasa za ushindani na ni mtu anayeamini kwenye hisia zak tu, sasa kwa udhaifu wake anataka nchi nzima iishi kwa hisia zake.
 
Bajeti iliyopitishwa n wengi ni halali. Jee hao wabunge wa upinzani waliopinga bajeti bungeni, na leo wanomba fungu lao, wanaomba wapewe bajeti haramu ni sawa.

Jana ilikuwa haramu lakini leo halali
Mbona mkuu unajichanganya? Umeshasema bajeti iliyopitishwa na wengi ni halali. Na kama ni halali ni kwa nchi nzima, siyo kwa CCM peke yao? Hata sheria mbovu ikipitishwa na bunge inakuwa halali na itatumika kwa wote, siyo kwa wale tu waliyoipitisha. Bajeti ya nchi inaendeshwa na kodi za wananchi wote, siyo kodi ya wanaccm peke yao!!!
 
Hauhitaji hata kufika darasa la saba kujua hii concept ya kupinga bajeti
Ukipinga bajeti ni sawa na kukataa maendeleo,ndio mana kuna bajeti kivuli kuonesha kuwa hamkubaliani na bajeti ya serikali,lakini kuikataa mana yake hata nyie hamtaki kulipwa
Rais yupo sahihi
elimu yetu imeshuka kwa kiwango kikubwa sana
angalia utumbo huu
 
Ok.. Kama wananchi ambao mbunge wao amepinga au kukosoa bajeti ya sirikali hawana haki ya kupelekewa miradi ya maendeleo, vipi kuhusu ulipaji wa kodi, waache kulipa??
 
Vitu muhimu vinavyohitajika tena vya msingi ni vingi lakini huko nyuma pesa zilipitishwa na bunge kufanya shughuli za maendeleo lakini zikaliwa na mtandao wa mafisadi karibu miaka 30 na zaidi.
Sasa anachofanya Magu ni kuhakikisha hio shilingi kidogo ikipangiwa kufanya shughuli fulani isitumike hovyo.Value for money for service rendered.Japo sio kazi rahisi kutokana na waliowengi kufanya kazi kwa mazoea.
 
Nyie kina MwanaHabari Huru acheni usanii.
Nyie ndio wapotoshaji wakubwa katika nchi hii, mlitupotosha wananchi kuwa Lowassa ni fisadi papa na alihusika ktk richmond na mpaka kwenye website ya chama mkamuweka kwenye orodha.
Leo hii mnamsujudia na mnataka kila mtanzania awaelewe!!!

Matapeli wakubwa nyie!

Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
Kwani wewe ni kasuku!!???
 
Back
Top Bottom