samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,174
Sasa nini itakuwa mantiki ya kuishi kwetu hapa duniani jamani ? Ni kama tumekuja kusindikiza wengine tu hapa, ila tusikate tamaa, mimi na wewe, sisi ndo wakuyaanza haya mabadiliko ya kifkra yenye matokeo chanya, tuanze sasa wala sio kesho, tuanze kwa kuamini kwamba tunaweza.
Mkuu sio suala la kuanza, hela ya kula yenyewe inasumbua hapa lazima kwanza uwe na uhakika wa maisha yako kwanza ndio ufuatilie vingine, huwezi kufuatilia vingine katika nchi ya hovyo hivi na kuacha kizazi chako kinaangamia kwa njaa Bro.
Wenzetu huko kuna standards walishaziseti tayari ndio maana unaona kila kitu kinaenda smooth in automatic move. Hakuna anayewaza shule sense vipi, au atapataje elimu bora, hakuna anayewaza atatibiwa vipi, hakuna anayewaza kula na kuvaa. Huku kwetu Bongo hata zile basic need tu ni mziki.
Mazingira yetu yanasababisha hata akili zinakuwa za hovyo tu, ukiwa shule unasoma wakati huohuo unawaza future itakuwaje ukiangalia kizazi chako kwenu huko.