Rais kubeba matofali ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa

Rockabie

Member
Nov 25, 2011
26
13
Wana JF nimetazama taarifa ya habari ya TBC leo saa 2usiku nimeona Rais wa Burundi Pierre Nkulunziza akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya mkuu wa mkoa nchini humo na inaelezwa kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wake wa kila wiki kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii kwa lengo la kurudisha moyo wa kizalendo.

Mnalionaje hili? na kama ingekuwa hapa kwetu unapendekeza Rais ashiriki shughuli zipi?
 
Jk hana moral command aache tu maana matendo yanatoka moyoni siyo kutafuta picha za magazeti kama anavyofanya
 
Wana JF nimetazama taarifa ya habari ya TBC leo saa 2usiku nimeona Rais wa Burundi Pierre Nkulunziza akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya mkuu wa mkoa nchini humo na inaelezwa kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wake wa kila wiki kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii kwa lengo la kurudisha moyo wa kizalendo.Mnalionaje hili? na kama ingekuwa hapa kwetu unapendekeza Rais ashiriki shughuli zipi?

Yeye na Pinda na mawaziri wengine wote wakashiriki katika kusafisha jiji la Dar ambalo limekithiri kwa uchafu. Hii iwe ni kila wiki kama afanyavyo Pierre Nkurunzira.
 
Wana JF nimetazama taarifa ya habari ya TBC leo saa 2usiku nimeona Rais wa Burundi Pierre Nkulunziza akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya mkuu wa mkoa nchini humo na inaelezwa kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wake wa kila wiki kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii kwa lengo la kurudisha moyo wa kizalendo.Mnalionaje hili? na kama ingekuwa hapa kwetu unapendekeza Rais ashiriki shughuli zipi?

Aende Saigon kunywa kahawa na kucheza karata.
 
Watafanya hivyo sa ngapi, Pida yuko bize anakunywa chimpumu na Bilal mpanda, Mkwe re yupo bize kwenye flight, labda apande mimea humo ndani ya ndege
 
Yeye si wa kwanza. Hata mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake alishiriki sana kazi za mikono vijijini na mijini
 
Wadau nadhani mliona coverage ya Rais wa burundi akisaidiana na wananchi wake kumjengea mkuu wake wa mkoa ofisi huko burundi, lakini vilevile kule rwanda Kagame anayafanya hayo hayo kwa kupitia mfumo wa Umuganda ambapo rais anashiriki kwenye shughuli za kijamii kila mwezi kwa kujitolea kufanya kazi za mikono na wananchi kama ilivyoripotiwa na daily news 28/11/2011 uk 5

Hivi ni vinchi vidogo lakini watatuacha sisi kwa sababu tunajidanganya kwa ukumu wa eneo bila kutumia fikra sahihi kujikomboa!!
 
Mkulima wa kweli Mwl. Nyerere ndiye aliweza kushirikana na wananchi wake ktk shughuli za maendeleo.
 
securedownload.jpeg

securedownload-2.jpeg

securedownload-1.jpeg
 
Wanajamvi wenzangu, kweli hatuko serious. Viongozi wetu, waliosoma hata development studies na kujua wajibu wetu kwa jamii, wamejaa umangi meza. Wanapenda kupiga magoti kwenye mikeka wakifanya kazi. Wanapenda wanyenyekewe.

Wako wapi akina Nyerere? Wako wapi akina Nyerere waliokuwa wakichimba mitaro tangu asubuhi hadi jioni kama kawaida?

Walikalia au kupigia magoti mikeka ili wafanye kazi? Hapana. Kwa nini? Si wa wananchi.
 
Watafanya hivyo sa ngapi, Pida yuko bize anakunywa chimpumu na Bilal mpanda, Mkwe re yupo bize kwenye flight, labda apande mimea humo ndani ya ndege

Jamani tusipoteze matumaini. Iko siku tutapata Nyerere wengine. Nawashauli angalieni ndani ya CDM. Wako wengi tu. Ni vigumu kujua kama mheshimiwa waziri mkuu anakuwa amekasirika au amefurahi. Lakini picha ile ilionyesha sura kukunjamana zaidi wakati anashiriki kimpumu kama alikuwa anasikia kinyaa vile. Uzalendo ulinimshinda kama vile alikuwa anaogopa kuambukizwa magonjwa ya kuhara.
 
Back
Top Bottom