Rais komesha uhuni huu TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais komesha uhuni huu TANESCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rmashauri, May 21, 2012.

 1. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenzangu, tatizo la umeme linaloikabili nchi yetu ni "man made" yaani ni la kutengenezwa na wanadamu. Katika mkutano kati ya waziri mpya wa Nishati na Madini na wafanyakazi wa TANESCO kanda ya Dar es Salaam na Pwani wiki iliyopita wafanyakazi walimweleza waziri matatizo lukuki yanayoikabili TANESCO na mengi yakiwa ni yakutengenezwa. Gazeti la leo la Mwananchi wameandika habari hiyo na nanukuu kipengele cha maneno ya mfanyakazi mmoja wa TANESCO alivyosema mbele ya waziri:

  [Mmoja wa wafanyakazi hao, Kamil Mwalangwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme wa Mega watts 100 alisema:
  "Katika kituo cha Mg 100 kuna makundi manne yanayonunua gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme,Kampuni ya Tegeta,Simbion, Songas na sisi Tanesco,lakini sisi bei tunayouziwa ni kubwa tofauti na wenzetu,nini sababu inayotufanya tununue kwa bei ya juu?alihoji na kuongeza: "Mheshimiwa Waziri pamoja na kununua kwa bei hiyo wakati mwingine sisi huamuriwa kuzima mashine zote ili kampuni nyingine ziweze kuzalisha na kuuza umeme na maagizo haya hutoka ngazi za juu"alisema Mwalangwa huku akishangiliwa na wafanya kazi wengine]


  Jamani huu uhuni wa baadhi ya viongozi wetu utaachwa uendelee mpaka lini? Mheshimiwa rais tafadhali ingilia kati kuiokoa nchi yetu na hawa wahujumu uchumi wa nchi yetu.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hii nchi bwana, haieleweki kama cheuro, mchele humo humo, karanga, crips
   
 3. K

  Kima mdogo JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ye mwenyewe mh.hu.ni atawezaje kudhibiti wenzie?
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  amesharejea atakusikiza. sijui kama kesho hana safari manake ni sii mkaaji saana.[​IMG]
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu akiamua anaweza sana labda kama na yeye ana mgao kwenye huo uhuni unaofanywa na hawa mabosi wa TANESCO na wizara
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  viongozi wote kwenda kumpokea imekaaje? garama za mafuta,misafara ni hasara kwa umaa. kwann wasiige nchi zingine tajiri hawana mda wa kumpokea mkuu wao,kila mtu anawajibika kwa wananchi.mda sasa umefika wa serikali kubana matumizi, ingekuwa vema rais anapokelewa na helkopta pale airport kupelekwa ikulu kuokoa muda wa wananchi kufungiwa barabara na resouce zingine/. suala la kutokuwa na umeme au uozo tanesco lingeshughulikiwa mapema lkn wao wanapanga siku nzima kumsubiri mkuu wetu. wasiingenda kumpokea wanafukuzwa kazi? mr presida piga marufuku hii kitu haipendezi zama za kifalme zimepita tunataka maendeleo sio saluti[​IMG]
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Lokisa,
  Tatizo hapa ni kuwa hawa wote kula yao inategemea huyo rais. Kama rais angepunguziwa madaraka ya kuteua watu nafikiri misafara kama hii ingepungua pia kwani hapa kila mmoja anajaribu kutetea kitumbua chake.
   
 8. N

  Njaare JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Viongozi wetu wa serikali na mashirika ya umma wanapenda sana kazi za kufanya na middlemen. Sijui ni uvivu au ni nini. Unakuta shirika lina wafanyakazi wameajiriwa kwa ajili ya kazi fulani lakini kazi hiyo hiyo inapewa mtu mwingine wa kati na mfanyakazi husika anakuwa mtazamaji tu.

  Walianza na kubinafsisha kazi za usafi, wakaingia walinzi wakaendelea manunuzi na sasa kazi za kitaalamu. Miaka ijayo hata wizara zetu zitaundiwa mtu wa kati kuwasiliana na raisi.
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  naam mchakato wa katiba mpya tuondoe kabisa ufalme tuweke uwajibikaji zaidi
  hvi anapoenda na mawaziri kutembea haoni uchungu wa kuifanya tanzania iwe kama nchi zingine kiuchumi?
  nchi nyingi hawajui kama umeme huwa unakatika.wengi wanatumia umeme wa upepo kama njia mbadala kama Denmark nk.tuna gesi ya kutosha iweje hadi leo tushindwe kujikwamua kama sio siasa zinaharibu na hakuna uwajibikaji
  ule wimbo wa tanzania nakupenda kwa moyo wote tunaimba tu kinafiki
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  huyo rais wa kukomesha yuko wapi?
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Rais huyu huyu tuliyenaye anaweza akitaka, na asipotaka anaweza kusukumwa kufanya hivyo hasa na bunge kama walivyomsukuma kuwatema mawaziri ambao kwa ridhaa yake ilionekana hakupenda kufanya hivyo.
   
 12. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili ni swali ambalo hata mimi na wengi huwa tunajiuliza na jibu hasa halijulikani. Utafikiri viongozi wetu shetani kawapofusha macho, wanaona lakini hawaoni, wanasikia lakini hawasikii taabu tupu. Kila kukicha wanaenda nchi za wenzetu hawaoni hata uchungu wa kutamani maendeleo wanayoyaona huko nasi tuyafikie au ndo hivyo wanabaki kusema aaaah sisi ni maskini maendeleo haya hatuwezi kuyafikia, tunabaki kuwa ombaomba tu ili hali tuna rasilimali ambazo tukizitumia ipasavyo inawezekana kuwa na umeme usiokatika, kuwa na usafiri wa umma wenye uhakika na ubora zaidi, standard ya maisha ya watu kupanda, huduma za jamaii kama vile maji na afya kuwa za kisasa zaidi n.k
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi huyo jamaa atafukuzwa kazi,rai yangu naomba chama cha wafanyakazi kimlinde.
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wanaweza kumwekea mizengwe lakini sheria zinamlinda na wahusika kwa hali ilivyo angalau kwa sasa wataogopa kumfukuza kazi.
   
 15. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni upepo tu utapita..........
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tehetehetehetehetehetehetehe. Hapana mkuu ni kimbunga hiki na wasipokaa sawa kitaondoka na mtu (watu)
   
 17. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Matatizo ya umeme ni dharura iliyotengenezwa ili kutunyonya damu. Huku Arusha Symbion wameshamaliza kufunga mitambo yao, wanasubiri dharura ambayo lazima ije ili waanze kunyonya damu za watanzania chini ya uangalizi wa serikali yetu wenyewe.
   
 18. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu hawa Wamarekani nafikiri waliletwa na RA maana haiingi akilini waje wanunue mitambo ya DOWANS yenye utata vile. Binafsi nilishapoteza imani na mataifa ya magharibi katika kutusadia kujikwamua kimaendeleo lengo lao ni kutunyonya tu na wanafurahi kutuona tukiendela kuwa maskini na ombaomba maana ndo habari zinazouzika hata kwenye media zao. Ni bora tuka-tie hata na Wachina ilimradi tu tuhakikishe kuwa hawatuletei vitu feki. Itabidi ifike mahali tuseme yatosha sasa (enough is enough).
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hujuma zimezidi, sisi wakazi wa Bunju beach, tuliomba umeme siku nyingi sana, baadaye akatokea mtu (jina kapuni) anayejiamini, aliwachukulia hatua, akawashitaki, kese akaishinda, walipewa siku tatu umeme uwepo, ni kweli wakatandaza nyaya siku mbili , siku ya kuwasha wakaiba nyaya zote, alafu siku iliyofuata, wakadai bunju beach hakuna ustaarabu , ona wameiba nyaya zote, kumbe ni wao walichukua wakidai kuzibadilisha.
  Kweli jamaa ni noma kwa uhuni, waitishe mikutano tanzania nzima kuna watu wanasiri nyingi, wangetumia njia ya zamani ya masanduku ya kula kwa wanaoona hawawezi kutoa maoni kwa sababy za kiusalama.
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  ccm oyeeeee
  10% oyeeeeeeee

  halafu siku hizi umeme unakatwa katwa sana sijui wanatengeneza mazingura ya mgao....  Kidumu chama cha mapinduzi
   
Loading...