Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,650
- 6,088
leta updates za presconference yenu uliyotujuza hapa mitandaoni usitugeuze wala viroba kama wewe na babu yako.Kauli ya Rais Kikwete kuhusu tuhuma za mwanawe na dawa za kulevya aliyoitoa akizungumza na Watanzania waishio Marekani, na ambayo watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu 'wamepambana' kweli kweli kuhakikisha inapata uzito unaostahili stori 'kubwa' ya rais, inafikirisha na kuibua maswali kadhaa!
Walau kwa kuanzia tunaweza kuuliza swali moja la msingi na mengine kadhaa ya nyongeza;
1. Hivi watu wa mitaani ni akina nani, walau kwa context ya Rais Kikwete, familia yake, Taasisi ya Urais, Serikali yake, CCM na taifa letu kwa ujumla?
i. Mara ngapi huwa anawapuuza watu wa mitaani ambao sisi wengine tunaamini kuwa ndiyo wananchi wake?
ii. Huko mitaani si ndiyo barabarani? Kwa hiyo anathibitisha kuwa watu ambao yeye anawathamini na anaweza kuwasikiliza ni wale ambao HUWA HAKUTANI barabarani? Ref. Hatukukutana barabarani.
iii. Makabrasha ya Serikali yake na CCM na hata kauli za mawaziri wake, watendaji wake na viongozi wake ndani ya chama zinazosema 'watoto wa mitaani'...huwa zinamaanisha ni watu wa kupuuzwa vile?
Rais anasema urais ni taasisi kubwa, kweli kabisa watu makini watakubaliana naye, lakini watauliza;
iv. Rais ameanza kujua lini kuwa taasisi ya urais ni kubwa?
v. Je aliposema taasisi ya urais ni kubwa, alimaanisha inapaswa kulinda heshima yake, kutumia mamlaka yake ipasavyo kuongoza?
Maana ukubwa wa taasisi hiyo haijawahi kuwa issue kubwa tangu aingie madarakani. Watu wa mitaani kama alivyowaita yeye, wanachohoji ni uadilifu, UWAJIBIKAJI, heshima ya taasisi hiyo, ni mamlaka ya taasisi hiyo (imewahi kusamehe wakosaji wa jinai, EPA, badala ya kufikishwa mahakamani, imeshindwa kuwashughulikia majangiri, iliahidi maisha bora kwa Watanzania na sasa inayumbisha na hata kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya) n.k.
Lakini pia Rais Kikwete katika majibu yake bila shaka ametusaidia kufumbua fumbo aliloliweka Dk. Slaa.
Mwaka juzi Dk. Slaa alipomtaka Rais Kikwete atoe kauli juu ya tuhuma kwamba mtoto mmoja wa kigogo mkubwa serikalini alikuwa amekamatwa na dawa za kulevya huko China, taarifa za vyombo vya habari vilivyomnukuu havikutaja jina la mtoto huyo!
Majibu ya Rais Kikwete yamekwenda hatua mbele kadhaa na kutuondolea utata wa jina la aliyekamatwa na kigogo huyo ni nani!
Watu wa mitaani wataendelea kuihoji taasisi yao ya urais kwa sababu wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere juu ya umuhimu wa taasisi hiyo! Tumwachie Rais Kikwete kazi ya kuwapuuza watu wa mitaani. Wananchi.
Kwa hiyo ulikosea tena 2010? Kwa mtu mwenye akili atasema kuwa hukukoseaTulikosea sana 2005
Mkuu, hivi hujui kuwa CHADEMA ni chama cha matukio?neno hilo mbona linatumika kila kukicha na watanzania wala halina maana hiyo unayotaka kuipindua...
Kweli kabisa Mkuu. Wanajidanganya sana hawaCheap politics hazitosaidia chama chenu mfu.
Umeiba Avatar ya kibo10Ukiona nguvu nyingi zinatumika kupinga tukio fulani; msikilizaji unatakiwa ufikirie zaidi ya kufikiria!
Kweli kabisa Mkuu. Wanajidanganya sana hawa
Umeiba Avatar ya kibo10
Rais hawezi kujibu mkusanyika wa mawazo ya kipuuzi rais ana mambo mengi ya kuwatumikia wananchi wake, hayo anawachia nyie na Dr.Slaa.Kauli ya Rais Kikwete kuhusu tuhuma za mwanawe na dawa za kulevya aliyoitoa akizungumza na Watanzania waishio Marekani, na ambayo watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu 'wamepambana' kweli kweli kuhakikisha inapata uzito unaostahili stori 'kubwa' ya rais, inafikirisha na kuibua maswali kadhaa!