A view to a kill
JF-Expert Member
- Jun 9, 2015
- 2,213
- 1,272
Mkapa alimuelewa ndo mana aliporomosha matusi kama mvuta bange kwenye uzinduzi wa kampeni yenu
Rais Kikwete ni mgumu sana kuelewa mambo
Unauhakika?Kikwete amekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya 30 bado hajui kwanini Tanzania ni maskini unategemea amwelewe Sumaye?
Jana katika uzinduzi wa kampeni za Urais Jangwani, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alisema hakumuelewa Sumaye aliyesema kahamia UKAWA kwa lengo la kuimalisha CCM. Katika hili hata mimi sikumuelewa Sumaye zaidi ya yote aliposema kina Mbatia hawana uwezo wa kuunda na kuongoza Serikaali......
Hebu tusaidie wewe ulivyomuelewa sumaye
Kwani anaelewa nini?
Maji hakuna .... haelewi,
Dawa hakuna ....haelewi,
Umeme hakuna ... haelewi,
Mishahara midogo .... haelewi,
Ajira hakuna ..... haelewi
Foleni kali ..... haelewi
haelewi na kweli haelewi kila kitu.
Ila wakati tunaitwa ni malofa na wapumbavu
alifurahia na kushangilia huku akipiga makofi.
Tarehe 25/1/2015 ataelewa tu.
SumayeKwa hio kati ya Sumaye na Kikwete hujamwelewa yupi?
Haeleweki jamaa!Ata mimi kuhusu kusema ameungana na watu kutoka kaskazini ili kuongeza nguvu ya kaskazini kuchukua nchi.. Mie sijaelewa ata mimi.
Vp aliposema kahamia UKAWA kuimalisha CCM ulimuelewa?Sumaye alimaanisha kwa kuwa mwenye uzoefu wa kuongoza serikali aliepo ukawa ni mgombea wao tu ambae ni Lowassa basi nae anaenda ukawa ambao ana uhakika na ushindi wao kuwapa uzoefu wa jinsi ya kuongoza mawizara ya serikali. Uelewe kuna tofauti kati ya kuwa na uwezo wa uongozi na uzoefu wa uongozi. Kwa kuwa wengi wa walio ukawa hawajawa na serikali ya kuongoza zaidi ya hizi zinazoitwa vivuli ambazo nazo huwajibika bungeni tu sasa wanaenda kushika na kuongoza serikali na watawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Sasa kwa msomi na kiongozi wa nchi ni kipi kilichomshinda kuelewa hapo? AU NI KULE KULE KUBEZA NA KUFIKIRI WANANCHI UELEWA WAO BADO UPO CHINI? SEMENI NYIE.
Kwani anaelewa nini?
Maji hakuna .... haelewi,
Dawa hakuna ....haelewi,
Umeme hakuna ... haelewi,
Mishahara midogo .... haelewi,
Ajira hakuna ..... haelewi
Foleni kali ..... haelewi
haelewi na kweli haelewi kila kitu.
Ila wakati tunaitwa ni malofa na wapumbavu
alifurahia na kushangilia huku akipiga makofi.
Tarehe 25/1/2015 ataelewa tu.
Hivi naota au?
KweIi ukombozi wa kweli upo karibu
Vp aliposema kahamia UKAWA kuimalisha CCM ulimuelewa?
Vp aliposema kahamia UKAWA kuimalisha CCM ulimuelewa?
Akisha wapa uzoefu anaenda wapi? au atarudi CCM? Maana hajulikani sasa yupo chama gani, yeye kasema kajiunga na UKAWA na Ukawa sio chama cha siasa!!!!!!!!!!!!!!!!Unapokubali jina la kishujaa lazima mawazo na uwezo wako kweli uonyeshe you have constructive thoughts for sure. Usiwe kama Matumbo nae anaendeleza utumbo hapa jukwaani. Hakuna popote aliposema Sumae anaenda kuunganisha nguvu na watu wa kaskazini kupata serikali.Huo ni upotofu na uendelezaji wa zile bezo nilizozungumzia. Tukirudi kwako kuhusu kuimarika ccm baada ya kuondoka kwa Sumaye ni hivi Chama chochote cha siasa kama ccm ni chama kikubwa ukilinganisha na chochote cha upinzani na chadema ikiwapo.Mbali ya kuwa chama tawala kwa muda mrefu pia kina manguli wengi wa siasa. Hakuna chama cha siasa haswa katika kipindi kigumu cha uchaguzi kingependa kumpoteza mwanachama wake ambae angekipa kura na wote walio nyuma yake.Ikitokea kama tunavyoona wanachama wengi wanakihama kipindi kama hiki ujue kuna udhaifu umedhihirika. Hapo watakaa kwenye vikao vyao vya uongozi na kujaribu kurekebisha kasoro zinazokifanya chama kukimbiwa. Hiyo hatua ndio aliyoiita Sumaye kukiimarisha chama. Ukumbuke hadi sasa wameshandoka mawaziri wakuu wastaafu wawili, wenyeviti wa chama wa mikoa na wilaya na wenyeviti na makatibu vijana wa mkoa kutaja tu wenye vyeo na watu wengi nyuma yao. Kwa vyovyote lazima chama kikae na kutafakari wapate suluhu.Huko ndio kujiimarisha upya. Ujue Sumae haendi ukawa kuimarisha chama bali anaenda kuwapa uzoefu. Utakuwa umepata mwanga.