Sumaye aliongea jambo gumu sana kwa mtu kuliongea mbele ya wenyeji wako lakini ni kweli.
Moja kwamba anaenda UKAWA kuongeza nguvu na hatimae uzoefu wakati wa kuongoza serikali.. kuna mambo mengi yapo nyuma ya pazia yanayoishia kwenye vikao vya ndani na madocument tele yaliyopigwa mihuri ya CONFIDENTIAL.. watawala wapya watakapokwenda huko wataanza kuyaona madudu hayo lakini sio kuyaona tuu hata watendaji wenye visasi watasakizia madocument ya wabaya wao wachukuliwe hatua kisha kila mtu anaweza kushitaki kila mtu taasisi au wizara nzima ikabaki haina msafi hata mmoja.. je ukiwafukuza wote kazi zitafanyika? Au badala ya kwenda mbele tutasimama kwanza tusafishe kisha tupige mark time tukifundisha watumishi wapya ghafla uchaguzi mwingine huu hapajafanyika kitu cha maana? Si hayo kuna mengi yanaweza kuharibika mtu asiye na uzoefu akapewa kuendesha kitu kikubwa na usisahau wenyeji wana tabia za kupima wageni sehemu za kazi hasa mgeni akija ni bosi wenu sasa uzoefu unahitajika hapo.. ni kweli kalisema hili mbele ya macho ya kina mbatia na mbowe na halikuwa jambo rahisi kusema lakini ndio ukweli ukibisha ni kwavile umezaliwa mbishi. Wanasiasa wengi wa upinzani wametoka shuleni wakaingia kwenye harakati za siasa za upinzani kisha wakashika kasi na vyeo lakini bado ni wageni serekalini.. yako mambo makubwa sana ya siri hata kwanini flani alibidi afungwe au afichwe au auwawe ili nchi ibaki salama.. lazima uzoefu utumike hapo katika regime change kabla kila kitu hakijawa miguu chini kichwa juu mwishowe ukasikia jeshi limechukua nchi kwa muda maana viongozi wote waliopita wako jela..
Mbili kutoka kwake kunaenda kuimarisha CCM.. ni wazi kwamba kila aliyetoka CCM kwa namna moja au nyingine ni mtu wa lowasa.. yeye si mtu wa lowasa na ametoka kumfuata lowasa.. hiyo ni ishara dhahiri kwa watu ambao ni wasafi na wana nia njema ingawa si watu wa lowasa kujiunga na mtoko huu.. wasafi hao wakishaondoka chama kitabaki na waliosalia sijui niwape jina gani lakini kikishatupwa nje ya dola kitaendelea kupukutika kabisa na watakaosalia mpaka duru ya mwisho ni wafia chama ambao sasa watapata nafasi ya kujipanga upya na kujenga chama kipya imara na kisicho na mawaaa kama kilivyo sasa... baada ya hapo kitarudi tena miaka mitano baadae na sera nzuri na watu wazuri wazoefu waliopumzika na wenye ushindani wa kweli wa kutaka kusaidia wananchi usio na hila kama huu wa sasa wa kuwaza kuiba kuiba kura tuu na kulazimisha watu kwamba watashinda kwa gharama yoyote..
NOTE: usisahau falsafa ya sumaye ni kuona vyama vikubwa viwili vikichuana na kubadilishana dola jambo ambalo alilielezea vizuri kwamba alitamani alifanye akiwa CCM.
Sumaye kaongea mambo magumu sana mbele ya wenyeji wake lakini ni ya kutafakari kabla hujatokwa na mapovu mdomoni na puani