Rais Kikwete ni Kiongozi mashuhuri Duniani.

Rais Kikwete ni Kiongozi mashuhuri Duniani.

kikwete ni mmoja kati ya maraisi bora kabisa afrika!! sijui leo angeenda yule mr GONGO angetoa mipovu ya aina gani
 
Siku zote sizikubali hotuba zake lakini leo amefanya kitu ambacho nimefurahi nacho nakujivunia ni Rais wangu
 
JK Nyerere ni kiongozi mashuhuri!Kikwete katembelea jina la Nyerere tu leo,alikuwa akilitaja tu anapigiwa makofi.
Hata akichaguliwa rais BOGUS kiasi nakuhakikishia akienda anga za kimataifa na kusema anatoka nchi ya Nyerere ataonekana bonge la GENIUS!
 
Nchi ndio imembeba vinginevyo heshima zimwendee aliyeiandaa hotuba ile.
 
Katika taarifa yake ya habari leo saa 2:00 usiku,TBC Taifa imesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi mashuhuri Duniani waliopata fursa ya kutoa hotuba katika Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Je ni kweli katika Viongozi mashuhuri duniani na Jakaya Kikwete yumo?

viongozi mashuhuri walitoa hotuba Uwanja wa FNB
 
Sasa kabook mapema ulitegemea wamteme.yeye anajua mambo FIFO-First In First Out.
 
Rais ni alama ya TAIFA hivyo UMASHUHURI wake ndio UMASHUHURI wa TAIFA.Binafsi nimeipenda hotuba aliyoitoa kwenye PODIUM ile hakika ilinikumbusha speech moja ya MWalimu ambayo nilibahatika kuiona kwa macho yangu,nikiwa nasoma Ordinary level wakati anamnadi Mzee Mkapa alisema kuwa zamani mtanzania katika mikutano ya kimataifa alipokuwa akitaka kuongea watu wote walioko kwenye kikao hicho walikuwa wanakaa sawa kusikiliza kwa umakini wasipitwe na jambo kwwa kuwa wanajua wana mambo ya kuondoka nayo toka kwa huyo Mtanzania.Hakika kwa Speech ile JK alijitahidi sana KU-MAP TANZANIA.Na siku hizi kadri siku zinavyodhidi kwenda hakika NAKUBALI BINAFSI kuwa AMEJIMUDU SANA kwenye SIASA za KIMATAIFA.

Naamini kadri unavyoonekana zaidi machoni mwa viongozi wakuu wenzio duniani ndivyo unavyoongeza confidence ya TAIFA lako,sura ya KUJIAMINI anayoionyesha JK kwenye jukwaa la KIMATAIFA dhidi ya viongozi wenzie KISAIKOLOJIA pia inaliinua TAIFA kwa namna furani.

Japo tuna mapungufu yetu kama TAIFA kama vile madawa ya kulevya,lakini mambo mengine kama haya ya SA yanaludisha HESHIMA na wakiludi nyuma kufuatilia TAIFA na kukutana na taarifa kama za JESHI letu CONGO mamawee wanazima fegi.

Ndivyo Mwalimu alivyowaweza Mataifa kwa kuwa na SPEECH zenye mvuto na weredi wa kuziwakilisha paspo kuhofu japokuwa ni Taifa dogo,lakini lenye kujiamni.Na binafsi naamini HAKUNA kitu wazungu wanogopa kama UNAPOJIAMINI.Sura ya JK kujiamni kama Rais wa Nchi,inajenga hivyo hivyo watanzania kuaminika.Kwenye sekta ya JK kujiamini kimataifa kafanikiwa kiasi kuwa MISSION nyingi za Kijeshi kimataifa Tanzania imezidaka sana na hivyo kuongeza credit ya KIMATAIFA.

SHOW me your friends And I will tell you who your!!!Jamaa amedaka Marafiki wa KIMATAIFA leo hii na kwa historia ya BABA wa Taifa JK amekuwa na influence.
 
Jakaya ni Raisi maarufu na makini. Nimefuatilia hotuba zote zilizotolewa kwenye msiba wa Madiba, hotuba aliyotoa Jakaya ilikuwa na msisimko, mvuto na mtiririko ulipangiliwa vizuri sana. Ukumbi wote ulikuwa unazizima na kuipokea hotuba hiyo kwa furaha sana. Pia hotuba aliyoitoa kenya kwenye sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya, ilikuwa ni hotuba nzuri sana na yenye mvuto wa kipekee.

Unaakilia finyu kweli kama kweli umefuatilia zote na umeona hiyo ndio bora. Hata ya Joyce Banda umeiona?
 
Haya ni matunda ya Mwalimu Nyerere na si zaidi .Viongozi mashuhuri walitoa speech zao mapema mwanzoni mwa wiki pale Uwanjani .Leo kasimama sababu ya Mwalimu na mazimbu nk .So ni Mwalimu na si JK kama yeye .

Mkuu, kama Nyerere asingefanya aliyofanya angekuwa na lipi la kuongea? Watu wanasahau kuwa pale kilichokuwa kinawekwa wazi ni Mahusiano ya Mandela na Nyerere na utawala wake katika jitihada za ukombozi.
JK amekuwa mara nyingi hata katika matukio ya ndani akikwepa sana kumtaja Nyerere kwa sababu zake mbona jana kang'ang'ania jina la Nyerere? Lunyungu, ajabu ya JF eti sasa hivi anayesifiwa ni JK? Nimeona Kule FB kuna watu kama Zitto naye anamsifia,mtoto wake Ridhiwan ndio usiseme na wengi wengineo kwa kujali cover ya kitabu badala ya yaliyomo.
Wanzetu wanajali kilichoongelewa, hivyo sii ajabu watu wa nje wametambua juhudi za Nyerere kwenye ukombozi ila leo ukiwauliza yule aliyetoa hadithi za Nyerere ni nani wakakujibu hatumkumbuki!
 
Last edited by a moderator:
Katika taarifa yake ya habari leo saa 2:00 usiku,TBC Taifa imesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi mashuhuri Duniani waliopata fursa ya kutoa hotuba katika Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Je ni kweli katika Viongozi mashuhuri duniani na Jakaya Kikwete yumo?

Kwanza angalia ni televisheni gani iliyotangaza.....TBC...Pili angalia ni audience gani iliyoityangazia.....Tanzania,.....tatu angalia kama wewe mwenyewe unaona ni kweli JK ni kiongozi maarufu duniani au la, nini kinamfanya maarufu au mashuhuru duniani. Nenda Zambia, au Namibia uwaulize rais wa Tanzania ni nani, wengine wanajua bado ni mzee Mwinyi. Kulekule SA kwenyewe watu ambao hawakusikia JK akitambulishwa walikuwa wanajiuliza huyu ni nani.

Kama nchi yenyewe si maarufu usitegemee hata kidogo kusikia kuwa rais wake ni maarufu. Huu ndio ujinga wa TBC yetu, very low level of journalistic standards.
 
Jakaya ni Raisi maarufu na makini. Nimefuatilia hotuba zote zilizotolewa kwenye msiba wa Madiba, hotuba aliyotoa Jakaya ilikuwa na msisimko, mvuto na mtiririko ulipangiliwa vizuri sana. Ukumbi wote ulikuwa unazizima na kuipokea hotuba hiyo kwa furaha sana. Pia hotuba aliyoitoa kenya kwenye sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya, ilikuwa ni hotuba nzuri sana na yenye mvuto wa kipekee.

Makini kwa kudanganya...anasema mandela alikuja tz january 1992 badala ya dec 1992..huyu ndo makini
 
Haya ni matunda ya Mwalimu Nyerere na si zaidi .Viongozi mashuhuri walitoa speech zao mapema mwanzoni mwa wiki pale Uwanjani .Leo kasimama sababu ya Mwalimu na mazimbu nk .So ni Mwalimu na si JK kama yeye .
Nimekuelewa lakini nina wasiwasi kama wengi wetu watakuelewa pia! Tumshukuru sana 'mzee/ndugu' Nyerere.
 
Back
Top Bottom