Rais Kikwete na mipango ya uchumi kwa Tanzania miaka 5 ijayo

SILENT ACtOR

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
627
181
Nafuatilia hotuba ya rais wenu JK, anatoa historia ya uchumi TZ tangu enzi za uhuru. Eti uchumi umekua kwa asilimia 7 ikilinganishwa na malengo ya asilimia 8.

Anajitahidi kusisitiza kuwa hali ngumu ya uchumi haikuanza leo, kwa mfano anasema "Miezi 18 ambayo mwalimu alitangaza tufunge mikanda ikawa miaka 18, mambo yakaharibika kweli kweli!"

Mpaka sasa haoneshi serikali yake itafanya nini kuboresha hali ila anasema wazungu wanatusifu kwelikweli. Anasema mfumuko wa bei umeshuka!

My take: huku kurudiarudia historia ni dalili za kutaka huruma ili kuficha udhaifu wake na serikali yake.

Anyway ngoja niendelee kutazama.
 
Anaelezea, mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2011/20012 - 2015/2016

Anasema,

Bajeti ya serikali kukaribia trilion 14.
 
Namuona JK yupo live TBC na ITV alitoa taarifa kwa umma kuhusu rasimu ya maendeleo kwa miaka mitano. Moja ya jambo nililolisikia ni kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi.
 
Amesema sasa hivi uchumi unaruhusu hata kufanya yale mambo ambayo zamani ilikuwa ni lazima kutegemea wahisani.
 
By the way hayuko hapo kuelezea bajeti, kwani hilo ni jukumu la waziri mwenye dhamana.
Bila shaka kilichomleta ni kutimiza agizo alilopewa kutimiza kabla ya saa 48 kwisha.
 
Mpango wa kwanza wa miaka mitano umekamilika katika kufikia lengo la 2025, vipaombele:-

1. Kukuza vyanzo vya uchumi
2. Kutumia raslimali na mikakati katika kukuza
3. Ajira zinaongezeka kwa kasi zaidi hasa kwa vijana
 
Jamani tuangalie TBC 1 mhe! Anatoa hotuba afu yule mzee(LOWASSA) aliyetemwa ccm yupo pale mstar wa mbele....
 
By the way hayuko hapo kuelezea bajeti, kwani hilo ni jukumu la waziri mwenye dhamana.
Bila shaka kilichomleta ni kutimiza agizo alilopewa kutimiza kabla ya saa 48 kwisha.

Lazima hili atalizungumzia mkuu,..wait and see.
 
Namuona JK yupo live TBC na ITV alitoa taarifa kwa umma kuhusu rasimu ya maendeleo kwa miaka mitano. Moja ya jambo nililolisikia ni kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi.

Eti eh?
naona niondoke tu JF,
nikiendelea kukaa humu ntapewa ban!
 
Hivi anahutubia bunge au ameamua tu kujitokeza kuuza sura kwenye TV? Ningekukuwa naanglia hiyo TV ninge mpiga na jiwe hapohapo kwenye TV!
 
Can anyone tell me what the doctor is talking about for sure, I don't grasp even a bite of what he is up to.
Tatizo he is mixing the language, and them laughing.
What is he up for in that speech?
 
amenukuu maneno ya mwl. Nyerere kwamba kupanga ni kuchagua.......angependa barabara zote ziwe na lami lakini haiwezekani. Kila kijiji kiwe na umeme lakini haiwezekani kwa sababu resorces hazitoshi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.
 
Awapiga kijembe CDM, kwa lawama na kuuza sura twenye TV, kulalamikia kila kitu.

Anadai CDM wanafanya maandamano nchi nzima kutukana, hahaha nimeipenda hii,
 
Back
Top Bottom