Rais Kikwete na mipango ya uchumi kwa Tanzania miaka 5 ijayo

Anasema eti CDM wanaandamana nchi nzima kutukana. Halafu Said Mwema na Vuai wanacheka
 
Mpango wa kwanza wa miaka mitano umekamilika katika kufikia lengo la 2025, vipaombele:-

1. Kukuza vyanzo vya uchumi
2. Kutumia raslimali na mikakati katika kukuza
3. Ajira zinaongezeka kwa kasi zaidi hasa kwa vijana
huyu jamaa muongo tume maliza mwaka sasa home bila kazi.. soon wadogo zetu wanatu join. sasa izo ajira ziko wapi??
 
Hivi anahutubia bunge au ameamua tu kujitokeza kuuza sura kwenye TV? Ningekukuwa naanglia hiyo TV ninge mpiga na jiwe hapohapo kwenye TV!


alikuwa ametembelea kiwanda cha sigara...kwa kuwa sigara ni karibu na TBC pugu, basi kaamua kwenda kuuza sura. jamani uyu rais wa bagamoyo kwa vituko !!
 
Awapiga kijembe CDM, kwa lawama na kuuza sura twenye TV, kulalamikia kila kitu.

Anadai CDM wanafanya maandamano nchi nzima kutukana, hahaha nimeipenda hii,
Kama vile hizi kelele za mlango zinakaribia kumnyima usingizi mwenye nyumba!
 
Billion 14 zinatosha kujenga jengo la Benjamini Mkapa Pension Towers bila kuweka umeme na kupiga rangi. Labda dola au trillion hizo. Hata hivyo hesabu ni janga la Taifa. Pole
 
Mwanzoni kasema alienda Hispania kuomba msaada wakati yuko Hazina akaambiwa wamechokwa watu walewale, chama kilekile.
 
Mkuu anachambua kwa kina miradi ya kuboresha uchumi wa Taifa letu, kiongozi anaupeo mkubwa sana katika uchumi.
 
anajitahidi kuwachekesha, hata amejiosha kwa kumfagilia Lowasa, teh, teh!
 
Gamba Jipya

Hata mimi namsikiliza kwenye Radio TBC ila sijui anawahutubia kina nani? Maana nasikia anamtaja Lowasa, Ole Sendeka, Bill Gates
 
Mpango wa kwanza wa miaka mitano umekamilika katika kufikia lengo la 2025, vipaombele:-

3. Ajira zinaongezeka kwa kasi zaidi hasa kwa vijana

yeah ni kweli. vijana wengi sasa wanajiajiri kwenye sekta ya kula dawa za kulevya.
 
Ngoja niitafute tbc taifa manake huku njia ya kwensa znz umeme tangu asubuhi hakuna na hatujaambiwa sababu au mgao kama kawa:glasses-nerdy:
 
Anasema uchumi umepanda sana, mfumuko wa bei umepanda lakn c juu single digit, so anasifu kwa hlo.
 
Ngoja nimpige picha iiweke P_Jun07_172328.jpg P_Jun07_172331.jpg
 
Back
Top Bottom