Rais Kikwete kweli ni Jembe


MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
672
Points
500
MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
672 500
Haina ubishi kuwa J. Kikwete ni rais pekee ametawala kwa mizengwe lakini namna anavyoipangua mizengwe hiyo, anastahili pongezi kubwa. Ikumbukwe zengwe la kwanza ni lile la kukataliwa na CHADEMA kuwa si rais halali, wakaenda mbali zaidi kwa wabunge wake kumzilia hotuba yake ya ufunguzi na kutoka nje ili kumdhalilisha, huku katibu mkuu kutangaza kuwa atahakikisha J.K hatawali.

Kikwete kwa umahiri mkubwa alitulia na kuendelea kuhutubia huku akiwahakikishia kuwa "ipo siku watarudi kwake" (walirudi hawakurudi?). Zengwe lingine ni la kudai kumshtaki J.K kwa wananchi ili kumshinikiza aondoke madarakani. Hili pia lilifanywa na CHADEMA kupitia maandamano sehemu mbalimbali za nchi wakilenga zaidi kutengeneza propaganda ya kuidanganya jumuiya ya kimataifa kuwa J.K hakubaliki na wananchi.

Hilo lilishindwa kwakuwa J.K alitulia na wala hakutaka kutumia nguvu ya dola ambao kimsingi ndiyo mtego ulikuwa umewekwa na CHADEMA. Maandamano yaliposhindwa, ukaanza ushawishi wa migomo kwa wafanyakazi walimu na madaktari, nalo lilishughulikiwa kwa umakini kila mtu anajua. Propaganda ya Ulimboka iliyoshikiwa bango na CHADEMA na wanaharakati kwa kumlazimisha Ulimboka aseme hata yasiyokuwepo, iligonga mwamba.

Zengwe zimezidi kuendelea kupitia M4C ya CHADEMA ambayo kwa mgongo wa elimu ya uraia ililenga kushawishi wananchi kuikataa serikali ya J.K kwa mtindo wa Libya, Tunisia na Misri, hiyo nayo nia wazi wananchi wameishtukia kuwa haina nia nzuri na hatma ya Amani ya Tanzania. Imekataliwa na ushahidi ni matokeo ya udiwani wa kata 29 uliofanyika hivi majuzi ambapo CHADEMA pamoja na nguvu kubwa ya M4C iliambulia kata 5! huku CCM ikijikombea kata 22 kati ya 29 zilizokuwa zinagombewa.

J.K amezidi kuimarisha CCM huku CHADEMA wakichelewa kugombania nani agombee urais/uenyekiti wa chama na kibaya zaidi na bila kujijua wote wamejikuta wanaimba wimbo wa CCM na kukiacha chama kikizidi kuangamia. Aliyozuiliwa Zitto kuyafanya, ndiyo yafanywayo na Mbowe.

Juzi juzi hivi Mbowe amesikika akiupongeza urais wa J.K na kukiri kuwa ni urais uliotukuka uliojaa busara na hekima na kwamba kwa TZ hakuna kama J.K. Kimsingi Slaa amejikuta akibaki peke yake aking'ang'ana na siasa za chuki na utovu wa nidhamu kwa J.K huku wenzake wote waliomzunguka wakimuasi bila yeye kujijua. J.K hajateteleka kiutendaji , zaidi ameendelea kukomaa na kujawa na maarifa zaidi.

Sote tumeshuhudia jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyovunja rekodi kwa ujenzi wa miundo kupitia hotuba ya Magufuli wakati wa Mkutano mkuu wa CCM Dodoma.

Kwa hakika J.K ni rais ambaye amewabaini wabaya wake mapema na sasa anacheza nao kama atakavyo. Anajua pia wabaya hao bado wanamtafuta kwani bado hawajakidhi haja ya kiu yao ya kuona J.K akitolewa ikulu kwa madai ya kuushindwa Urais. J.K kweli ni zaidi ya "jembe".
 
O

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Messages
10,946
Points
1,225
O

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined May 24, 2008
10,946 1,225
Ni kweli jk ni jembe, kwa mke na mtoto kuwa wajumbe wa nec bila kupigwa jamaa ni jembe,
 
MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
672
Points
500
MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
672 500
Wachangiaji ninawasihi tuchangie kwa ustaarabu. Sitaki ban jamani. Mimi nimejenga hoja zangu kama nawe una zako jenga ili kutetea unachoamini ni sahihi. Lugha za dhihaka na matusi si za magreat thinker kama nyie.
 
MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
672
Points
500
MJENGA

MJENGA

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
672 500
Mungi sina wasiwasi na J.K kwa mke wangu ila nina w hofu sana na babu chadomo maana yeye kwa wake za watu ni soooo!
 
D

dotto

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
1,725
Points
1,195
D

dotto

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
1,725 1,195
Kweli ni jembe maana ni zao la Tume huru ya Uchaguzi iliyoongozwa na Makame, Jembe la ukweli Kigoma kama Dubai, Jembe la ukweli kwa hajui kwa nini TAnzania ni Masikini, Jembe la Ukweli maana alikacha midahalo wakati wa KAmpeni 2005 na 2010. JK JEMBE LA UKWELI au KWA MBELEKO!!
 
K

kibananhukhu

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
368
Points
195
K

kibananhukhu

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
368 195
Hakuna Rais aliyetawala kipindi kigumu kama JK. Alianza na Tatizo la UMEME, NO Uzalishaji, Likaja la tofauti za fikra baina yake, na Upande wa Mkapa, Mangula, Salim A, Salim, Butiku, Kaduma na wenzao, Likaja la Mafisadi, Sikuamini Jeetu Patel Alivyowekwa Rumande, Lipo bado la Mramba na Mgonja, Likamalizia la Lowasa Kujiuzulu. Uchumi duni bila uzalishaji, Wizi na Hujuma Reli, Bandari, Uzalishaji umeme, na Maofisini, Uhuru vyombo vya habari na uhuru wa watu kusema, Kukabiliana na changamoto za wasomi wa shule za kata kutoka kila kata na kila aliyemaliza form four anajua kukosoa na kupenda upinzani bila kujua ni yeye karuhusu.

Elimu ya juu, mfano hai. 2002 Nyegezi SAUT Peke yake ilikuwa na wanafunzi 300 leo wanakimbizana na Ellfu 15, nyegezi tu, acha matawi yake ya Mwenge Moshi, Dar, Ruco Iringa, Tabora, Mtwara, Songea nk. Udom pia, Nelson Mandela, Tumaini, St. John. Wote wanaomaliza ni wanasiasa na wanajua sana kuongelea uchumi na kukosoa. Magazeti, Redio, Zanziber, Uamsho, Serikali tatu, Katiba, Udini, Ukabila, Rushwa za ndani na nje ya chama. Doh!!!! Jamani, Mwacheni JK Afanye kazi. Tutamkumbuka, tunamchukia leo. Rais wa kumpenda ni wa kunywa nae chai. Mwl. JKN. Huenda kuchukiwa sn ni dalili njema ili tumkumbuke baadae.
 
mkada

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
1,169
Points
1,500
mkada

mkada

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2011
1,169 1,500
JK is a politician like any other politicians, he plays well, he plays dirty, marafiki zake wa juzi ndo maadui zake leo,maadui zake wa juzi ndo marafiki zake leo,katika maisha its a normal thing,he keeps moving and the ball rolls.I like his survival techniques,na huyu kweli ni Commander in Chief.
 
REMSA

REMSA

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
2,577
Points
1,225
REMSA

REMSA

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
2,577 1,225
Kwenye hoja ujembe wa JK ni kusababisha maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi ya alivyoyakuta na kuahidi maisha bora?Alikuta kilo ya mchele sh.800 sasa ni 2500,Nyama 2500 sasa ni 6000,kiberiti 20 sasa ni 150,unga sembe 250 sasa ni 1200,maharage 600 sasa ni 2000.Tulikuwa na ndege 11 ATCL sasa tuna 1 tena mbovu.Tembo walikuwa wengi sasa ni wa kutafuta,.............Haya ni machache sana yako mengi yanayoonyesha
ujembe wa JK.THINK TWICE"""""!!!!
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
60,015
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
60,015 2,000
Umeijadili Chadema zaidi kuliko Jk ,sasa kwa nini usi edit hiyo heading yako ? Unaonyesha kuwa unautaka umaarufu kwa nguvu , rejea kupanda cheo ndani ya ccm ni lazima uishambulie cdm hata kama huna kitu kichwani ! Mfano hai ni Wasira , Mwigulu , Nape , una akili sana kwa sababu umegundua kwamba tumbo lako ni bora kuliko utu wako , Hongera !
 
Monyiaichi

Monyiaichi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
1,826
Points
1,250
Age
62
Monyiaichi

Monyiaichi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
1,826 1,250
Hakuna anayekuzuia kumwona kuwa ni jembe, tatizo ni la kulazimisha na wengine nao wamwone hivyo. Halafu, ukilazimisha jambo ambalo watu wengine wanaona kinyume au sio vile, unataka implication iweje, kwa wewe? Unatumikia payroll au kuna ujamaa wa kiaina ulionao na huyo!
 
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,013
Points
1,225
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,013 1,225
Wapinzani kwa ujinga wao hawatambui kuwa utawala wa JK ndolumewapa umaarufu na kujulikana pindi atakapo toka madarakani ndo watakapo tambuwa umuhimu wake.
 
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,542
Points
1,250
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,542 1,250
Kwa mtazamo wako Jemga, JK ni jembe, lakini kwa uelewa wangu naona kama unakejeli. Ironic presentation'.

Unataka watu waangalie kwa upana migogoro iliyotokea wakati wa utawala wa JK. Kapata uraisi kwa mizengwe kisha kaa kimya akisikilizia upepo. Huo kwa mtazamo wako ni ujanja. Madaktari wamegoma, wananchi wengi wakafa, yeye kaenda zake ng'ambo akiacha nyuma sakata la madaktari. Baada sakata kutulia akatoa hotuba kama vile mfiwa anayelia baada ya kuanua matanga kwako wewe, mheshimwa Mjenga huo ndiyo ujembe. Badala ya kujibu hoja za wanachi anawateka, anawapiga, anawaumiza anawatupa Mabwepande, kwako wewe mheshimiwa Mjenga, vitendo hivi nivya kutukuka.Katika nchi za kistaarabu hata tawala za kistaarabu vitendo kama hivi ni ndra kuvisikia, kwako wewe mheshimiwa Mjenga nchi hizo na tawalahizo hazina viongozi jembe isipokuwa kinyume chake.

Mjenga, sidhani kama unamaanisha unachosema ila kinyume chake. Kama kweli una maana ya unachosema, basi sio mtanzania aliyezoea ustaarabu na kulelewa katika mazingira ya AMANI. Umetokea nchi ya wahuni fulani wanaoendesha mabo yao pasi na kufikiri, kujali maisha na haki za wengine. Nchi ambayo wasio na madaraka hawana nafasi ya kusema hiki hapana kile sawa. Una fikira zakitumwa ambaye kila anachosema bwana mkubwa kwako ni hewala, hakuna kupinga chochote, hata akisema ni baba yako, mume wa mama yako, hata kama unamjua babayako mzazi, maskini utasema sawa. SIAMINI, lazima utakuwa unatania
 
M

marembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Messages
202
Points
170
M

marembo

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2011
202 170
Mjenga kanywe uji ulale naona una usingizi wa pono. Unayoongea ni mambo yasiyo na mshiko. Yaani kata zenu mlizokuwa mnashikilia mlitegemea zitachukuliwa ni ushahi kuwa magamba wanaweweseka na wakombozi wa nchi. Matokeo hayo ni baada ya kudhani CDM hawatasimamisha wagombea sehemu mbalimbali za nchi. Kama kawaida kutumia urasimu na mchezo mchafu wa Halmashauri husika na mkoa wa kipolisi Katika kata 3 mlilizokuwa mshikilia zimeondoka kwenda kwenye mkondo wa M4C. Hizo ni rasharasha tu. Tukamsikia Nape anasema hawasikitiki kwa hiko. Walipewa mfano katika maisha ya kawaida watoto wako 3 wakifa unabaki unasherehekea au? Utakuwa mzazi wa ajabu kufanya hivyo. Magamba kwishne mmekumbauka shuka kumepambazuka!
 
ojoromong'o

ojoromong'o

Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
91
Points
0
ojoromong'o

ojoromong'o

Member
Joined Nov 6, 2012
91 0
...JK ni jembe la kupalilia mashamba wezi ili wapate mavuno mazuri,mavuno yamekuwa makubwa mpaka maghara yao ya hapa yamejaa na sasa wemepereka Uswis kuyaifadhi...
 
kizaizai

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Messages
3,022
Points
2,000
kizaizai

kizaizai

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2010
3,022 2,000
Majembe ni sisi wa-TZ ambao tunafikirishwa kwamba mambo yanaenda sawa wakati ukweli tunajua tunadanganywa kwa maneno tu. JK anapoongea mipasho watu wazima na akili zao timamu wanampongeza. Tunazidi kuchakaa kimwili, kiakili mpaka kiroho.
 
C

cencer09

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
2,453
Points
2,000
C

cencer09

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2012
2,453 2,000
Wachangiaji ninawasihi tuchangie kwa ustaarabu. Sitaki ban jamani. Mimi nimejenga hoja zangu kama nawe una zako jenga ili kutetea unachoamini ni sahihi. Lugha za dhihaka na matusi si za magreat thinker kama nyie.
great thinkers unayepotosha ukweli hata kumhusisha Ulimboka?Angalia jinsi upelelezi ulivyoendeshwa kwa kukamata chizi.Mwanahalisi limefungiwa kwa kusema ukweli si mahakamani ambako ukweli ungefichuka.
ni thread iliyojaa ushabiki wakati watz wanaumia
jitayarishe kupokea majibu ya kuudhi kama unavyotaka kuwakera kwa sababu silly question deserve a silly answer.Hapa roho inaniuma nikihisi kutumia busara walau ya kuazima
 
Z

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Messages
2,456
Points
1,500
Z

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2009
2,456 1,500
JK si tu JEMBE, bali ni JEMBE NA SULULU au SHOKA kama ukipenda. Kwa maana nyingine ile alama iliyoko kwenye bendera ya CCM ndio JK. Ukitaka kumjua zaidi JK muulize MO Ibrahim, kwani yeye ndio kamaliza.

Ndugu MJENGA, mada kama hizi CHADEMA hawawezi kujibu kwa hoja, angalia ukurasa wa 3 hakuna aliyejibu hoja. Tafsiri fupi ya hali hii ni kuwa hila na vitimbi vyao vimeshindwa, kwani wao wangependa kuiona nchi haitawaliki na Tanzania inaingia katika VITA. Dua zao zote zimeshindikana, na kibaya zaidi watanzania wamekielewa CHADEMA kama chama chenye nia mbaya na WATANZANIA. Na hii imejionyesha wazi katika matokeo ya UDIWANI kama ulivyoainisha katika mada yako.

Tatizo la CHADEMA ni kushindwa kukubali hata katika yale mazuri ambayo yanaonekana wazi kwa wananchi yaliyofanywa na serikali. Kitendo hiki ndicho kitachoiua CHADEMA, kwa sababu watanzania ni watu wenye akili sana na kuelewa ni nini kinawezekana na nini ni Propaganda.

Katika mafanikio yote umeyasema, lakini kubwa lililowafunga mdomo wapinzani ni la kufanikisha UCHAGUZI MKUU WA CHAMA KATIKA NGAZI KUU MBALI MBALI MJINI DODOMA hivi karibuni. Wengi walifikiri ngumi zitapigwa na chama kitachanika vipande vidogo vidogo kama chembe za mtama. Hilo halikutokea, na ni kwa juhudi na umakini mkubwa wa Mwenyekiti, JK. Safu ilivyojipanga inaitisha CHADEMA na iaashiria mwisho wa mbio zao kuelekea IKULU. Kama kuna CHAMA kinachofahamu umahiri wa JK, basi ni CHADEMA.

Naweza kubet kuwa JK atapata zawadi ya MO Ibrahim mwaka 2016/2017, kwa ufanisi wake mzuri wa kujenga Demokrasia Tanzania ikiwa pamoja na uhuru wa kusema, kuunda urafiki na vyama vyote nchini, kukuza elimu na kuijenga Tanzania yenye matumaini.

Ukitaka kujua mafanikio ya Tanzania katika demokrasia, tathmini hali ya demokrasia katka nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia na Kongo. Ukipata jibu rudi mtandaoni.

JK ni historia kwa Tanzania.
 

Forum statistics

Threads 1,295,163
Members 498,180
Posts 31,201,909
Top