Rais Kikwete kweli ni Jembe

Ndugu yangu, suala la Rushwa si rahisi kama CHADEMA wanavyolizungumzia. Kiongozi mpya (Katibu wa chama) wa chama cha KIKOMUNISTI CHA CHINA katika hotuiba yake amelieleza tatizo la rushwa ndani ya chama kama changamoto kubwa iliyopo kwa chama sasa hivi.

Kumbuka kama kuna nchi unapata adhabu ya kifo kwa viongozi wa juu wanapokutikana na hatia hiyo duniani, ni CHINA. Lakini tatizo bado ni pevu. Hili ni tatizo zito na wala si la kutatuliwa kwa mwaka wala miaka mitano.

La msingi ni kulikubali tatizo na kuwa na dhamira ya kulitokomeza.

kwa mtazamo wako rushwa inazungumzwa na chadema tu.kwa hiyo kiongozi mkuu kuhusishwa na rushwa kwa ccm rukhsa,
kumbuka jk alikejeli chadema kuweka hadharani list of shame,lakini mwishowe akaweka kamati ya kuwasafisha kagoda.
vipi richmond na dowans?
hapo dhamira ya kupambana rushwa iko wapi?
kuwa mzalendo ipende nchi yako hakuna rafiki wala adui wa kudumu ktk siasa ndiyo maana nchi kama ufaransa Miterand hakuweza kurudi madarakani kwa muhula mwingine kwa sababu hakukidhi haja.
hapa miaka hamsini na ukweli mnauona lakini kwa sababu ya matumbo yenu mnataka kuleta upotoshaji eti si rahisi kama chadema wanavyosema tuelezee ccm mnapambanayo vipi?
Kwa kulalamika jukwaani?"..zamani rushwa ilikuwa na wanaume lakini sasa hata nyinyi wanawake.."
ana takukuru,tume ya maadili ya uongozi etc etc.polisi anawatumia kupiga chadema si kukamata wala kupeleka mahakamani.
kwa style hii i prefer chadema.bakini na upambe wenu wa ccm
 
Hapo umechinja kabisa!!!!!. Watu hawataki kukubali ukweli J.K atachukua Mo. Ibrahim na chadomo watabaki kusema aaa eee. Sijawahi ona rais makini ktk kushughulikia issues za taifa kama J.K. Viva rais kichwa Mungu yu pamoja nawe hakika.
Kibaraka usie na haya wewe! Mungu yupi unae mzungumzia?tutolee kamasi hapa nguruwe mkubwa wee.
 
Haina ubishi kuwa J. Kikwete ni rais pekee ametawala kwa mizengwe lakini namna anavyoipangua mizengwe hiyo, anastahili pongezi kubwa. Ikumbukwe zengwe la kwanza ni lile la kukataliwa na CHADEMA kuwa si rais halali, wakaenda mbali zaidi kwa wabunge wake kumzilia hotuba yake ya ufunguzi na kutoka nje ili kumdhalilisha, huku katibu mkuu kutangaza kuwa atahakikisha J.K hatawali.

Kikwete kwa umahiri mkubwa alitulia na kuendelea kuhutubia huku akiwahakikishia kuwa "ipo siku watarudi kwake" (walirudi hawakurudi?). Zengwe lingine ni la kudai kumshtaki J.K kwa wananchi ili kumshinikiza aondoke madarakani. Hili pia lilifanywa na CHADEMA kupitia maandamano sehemu mbalimbali za nchi wakilenga zaidi kutengeneza propaganda ya kuidanganya jumuiya ya kimataifa kuwa J.K hakubaliki na wananchi.

Hilo lilishindwa kwakuwa J.K alitulia na wala hakutaka kutumia nguvu ya dola ambao kimsingi ndiyo mtego ulikuwa umewekwa na CHADEMA. Maandamano yaliposhindwa, ukaanza ushawishi wa migomo kwa wafanyakazi walimu na madaktari, nalo lilishughulikiwa kwa umakini kila mtu anajua. Propaganda ya Ulimboka iliyoshikiwa bango na CHADEMA na wanaharakati kwa kumlazimisha Ulimboka aseme hata yasiyokuwepo, iligonga mwamba.

Zengwe zimezidi kuendelea kupitia M4C ya CHADEMA ambayo kwa mgongo wa elimu ya uraia ililenga kushawishi wananchi kuikataa serikali ya J.K kwa mtindo wa Libya, Tunisia na Misri, hiyo nayo nia wazi wananchi wameishtukia kuwa haina nia nzuri na hatma ya Amani ya Tanzania. Imekataliwa na ushahidi ni matokeo ya udiwani wa kata 29 uliofanyika hivi majuzi ambapo CHADEMA pamoja na nguvu kubwa ya M4C iliambulia kata 5! huku CCM ikijikombea kata 22 kati ya 29 zilizokuwa zinagombewa.

J.K amezidi kuimarisha CCM huku CHADEMA wakichelewa kugombania nani agombee urais/uenyekiti wa chama na kibaya zaidi na bila kujijua wote wamejikuta wanaimba wimbo wa CCM na kukiacha chama kikizidi kuangamia. Aliyozuiliwa Zitto kuyafanya, ndiyo yafanywayo na Mbowe.

Juzi juzi hivi Mbowe amesikika akiupongeza urais wa J.K na kukiri kuwa ni urais uliotukuka uliojaa busara na hekima na kwamba kwa TZ hakuna kama J.K. Kimsingi Slaa amejikuta akibaki peke yake aking'ang'ana na siasa za chuki na utovu wa nidhamu kwa J.K huku wenzake wote waliomzunguka wakimuasi bila yeye kujijua. J.K hajateteleka kiutendaji , zaidi ameendelea kukomaa na kujawa na maarifa zaidi.

Sote tumeshuhudia jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyovunja rekodi kwa ujenzi wa miundo kupitia hotuba ya Magufuli wakati wa Mkutano mkuu wa CCM Dodoma.

Kwa hakika J.K ni rais ambaye amewabaini wabaya wake mapema na sasa anacheza nao kama atakavyo. Anajua pia wabaya hao bado wanamtafuta kwani bado hawajakidhi haja ya kiu yao ya kuona J.K akitolewa ikulu kwa madai ya kuushindwa Urais. J.K kweli ni zaidi ya "jembe".

JK, mutu ya msoga,
 
Hii forum imekuwa kama China sasa. Serekali ya China imeajiri watu kabisa kufanya kazi kwenye mitandao ya kijamii ku neutralize discussion. Raisi naye sijui ameajiri watu sasa ku neutralize discussion. Maana naona hakuna hata moja la sifa hapo. Tanzania na rasilimali zilizoko lakini watu wanaishi ufukara wa kutupwa wakati nguvu za wanyonge zinaibiwa kila leo na raisi anachekelea na kutabasamu kwa mafisadi na kuwapongeza kwa kuibia wanyonge leo unampa sifa hata asizostahili. Kweli utumwa ni mbaya, hata wana wa Israel walikataa kutolewa Misri kwa sababu walikuwa wameshazoea utumwa
 
Kwa nini unafikiri kuwa rais ameajiri watu wa ku neutralize discussion humu? Au kazi ya mitandao ya kijamii hususani huu ni kukandia tu wether it is true or not? Au unataka kutuambia mtandao huu ni kwa ajili ya kumkandia rais tu, vinginevyo you don't belong, bado mtasema mengi humu, kwenye ukweli uwongo hujitenga.
 
images
images
images

Jembe? Amua mwenyewe!
 
JK jembe la uhakika kwa kutengeneza demokrasia ya kwake kwenye uchaguzi wa CCM yaani kumwona kwa macho yake kuwa fulani kanipigia kura ya hapana na fulani kanipigia kura ya ndio.Na ujembe huo kawaahidi wanaCCM kuwa wawili(2) waliomkataa wamwaachie atawashugulikia.
 
Kha!..
Mtoa hoja mwenyewe jina lake,mjinga sasa atatoa hoja ya maana?..
Mkuu watu kama nyie nikuwaacha tu na ujinga wenu!..
Eti jk jembe?..yaani cwezi hata kumlinganisha na uwezo aliokua nao kiranja wangu wa chekechea!..
 
Kwa nini unafikiri kuwa rais ameajiri watu wa ku neutralize discussion humu? Au kazi ya mitandao ya kijamii hususani huu ni kukandia tu wether it is true or not? Au unataka kutuambia mtandao huu ni kwa ajili ya kumkandia rais tu, vinginevyo you don't belong, bado mtasema mengi humu, kwenye ukweli uwongo hujitenga.

SINTO FAHAMU, ukweli ni kuwa hakuna ufisadi Tanzania na Uwongo ni kuwa Raisi Kikwete ni kiongozi mzuri kwa kuwa anatuia akili na muda mwingi kwenye siasa kuliko utendaji. Hiyo ni kutokana na comment yako.

Kulingana ninavyoangalia mambo mimi na uzoefu wangu katika mambo yanayoendelea nchi nyingi, tukipata viongozi kama JK miaka mingine kumi ijayo, Tanzana itakuwa masikini kuliko zote ulimwenguni. Tutasikia tu wenzetu Rwanda wakipaa kuelekea kwenye dunia ya kwanza wakati hata rasilimali hawana. In fact Rwanda is over populated, hata eneo la kulima hawana. Sisi tutakuwa tunaendelea kung'ang'ana na kupigana vijembe kwenye majukwaa badala ya kujibu hoja kiutendaji. Vyama vya siasa vinatakiwa viwe watch dogs, hoja inayotolewa na vyama vya siasa ni kwa ajili ya kurekebisha mambo serekalini sio chama kilichoko madarakani kujibu hoja kwa vijembe kwenye majukwaa.

Kumbuka maneno ya unayemsifu, HOJA ZENU NI ZA MSINGI, LAKINI NIKIZIKUBALI WENZANGU KATIKA CHAMA WATANIELEWA KWELI?
 
Haina ubishi kuwa J. Kikwete ni rais pekee ametawala kwa mizengwe lakini namna anavyoipangua mizengwe hiyo, anastahili pongezi kubwa. Ikumbukwe zengwe la kwanza ni lile la kukataliwa na CHADEMA kuwa si rais halali, wakaenda mbali zaidi kwa wabunge wake kumzilia hotuba yake ya ufunguzi na kutoka nje ili kumdhalilisha, huku katibu mkuu kutangaza kuwa atahakikisha J.K hatawali.

Kikwete kwa umahiri mkubwa alitulia na kuendelea kuhutubia huku akiwahakikishia kuwa "ipo siku watarudi kwake" (walirudi hawakurudi?). Zengwe lingine ni la kudai kumshtaki J.K kwa wananchi ili kumshinikiza aondoke madarakani. Hili pia lilifanywa na CHADEMA kupitia maandamano sehemu mbalimbali za nchi wakilenga zaidi kutengeneza propaganda ya kuidanganya jumuiya ya kimataifa kuwa J.K hakubaliki na wananchi.

Hilo lilishindwa kwakuwa J.K alitulia na wala hakutaka kutumia nguvu ya dola ambao kimsingi ndiyo mtego ulikuwa umewekwa na CHADEMA. Maandamano yaliposhindwa, ukaanza ushawishi wa migomo kwa wafanyakazi walimu na madaktari, nalo lilishughulikiwa kwa umakini kila mtu anajua. Propaganda ya Ulimboka iliyoshikiwa bango na CHADEMA na wanaharakati kwa kumlazimisha Ulimboka aseme hata yasiyokuwepo, iligonga mwamba.

Zengwe zimezidi kuendelea kupitia M4C ya CHADEMA ambayo kwa mgongo wa elimu ya uraia ililenga kushawishi wananchi kuikataa serikali ya J.K kwa mtindo wa Libya, Tunisia na Misri, hiyo nayo nia wazi wananchi wameishtukia kuwa haina nia nzuri na hatma ya Amani ya Tanzania. Imekataliwa na ushahidi ni matokeo ya udiwani wa kata 29 uliofanyika hivi majuzi ambapo CHADEMA pamoja na nguvu kubwa ya M4C iliambulia kata 5! huku CCM ikijikombea kata 22 kati ya 29 zilizokuwa zinagombewa.

J.K amezidi kuimarisha CCM huku CHADEMA wakichelewa kugombania nani agombee urais/uenyekiti wa chama na kibaya zaidi na bila kujijua wote wamejikuta wanaimba wimbo wa CCM na kukiacha chama kikizidi kuangamia. Aliyozuiliwa Zitto kuyafanya, ndiyo yafanywayo na Mbowe.

Juzi juzi hivi Mbowe amesikika akiupongeza urais wa J.K na kukiri kuwa ni urais uliotukuka uliojaa busara na hekima na kwamba kwa TZ hakuna kama J.K. Kimsingi Slaa amejikuta akibaki peke yake aking'ang'ana na siasa za chuki na utovu wa nidhamu kwa J.K huku wenzake wote waliomzunguka wakimuasi bila yeye kujijua. J.K hajateteleka kiutendaji , zaidi ameendelea kukomaa na kujawa na maarifa zaidi.

Sote tumeshuhudia jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyovunja rekodi kwa ujenzi wa miundo kupitia hotuba ya Magufuli wakati wa Mkutano mkuu wa CCM Dodoma.

Kwa hakika J.K ni rais ambaye amewabaini wabaya wake mapema na sasa anacheza nao kama atakavyo. Anajua pia wabaya hao bado wanamtafuta kwani bado hawajakidhi haja ya kiu yao ya kuona J.K akitolewa ikulu kwa madai ya kuushindwa Urais. J.K kweli ni zaidi ya "jembe".

Hana ujembe wowote. Bahati yake anaongoza taifa la watu vipofu, viziwi na wafu!
 
kwa mtazamo wako rushwa inazungumzwa na chadema tu.kwa hiyo kiongozi mkuu kuhusishwa na rushwa kwa ccm rukhsa,
kumbuka jk alikejeli chadema kuweka hadharani list of shame,lakini mwishowe akaweka kamati ya kuwasafisha kagoda.
vipi richmond na dowans?
hapo dhamira ya kupambana rushwa iko wapi?
kuwa mzalendo ipende nchi yako hakuna rafiki wala adui wa kudumu ktk siasa ndiyo maana nchi kama ufaransa Miterand hakuweza kurudi madarakani kwa muhula mwingine kwa sababu hakukidhi haja.
hapa miaka hamsini na ukweli mnauona lakini kwa sababu ya matumbo yenu mnataka kuleta upotoshaji eti si rahisi kama chadema wanavyosema tuelezee ccm mnapambanayo vipi?
Kwa kulalamika jukwaani?"..zamani rushwa ilikuwa na wanaume lakini sasa hata nyinyi wanawake.."
ana takukuru,tume ya maadili ya uongozi etc etc.polisi anawatumia kupiga chadema si kukamata wala kupeleka mahakamani.
kwa style hii i prefer chadema.bakini na upambe wenu wa ccm

Subiri, nitafungua THREAD kuhusu maswala ya RUSHWA na UFISADI, vinginevyo kama tukijikita kwenye hili tutatoka nje ya mada.

Kifupi, hayo uliyoyataja ni asilimia 10 tu ya ufumbuzi wa kutokomeza rushwa. Kuna maswala kama ya kipato, maadili, elimu, kuwepo kwa kinachohitajika kutosheleza wahusika, Transparency, ukilitimba(bureacracy) na kadhalika.

Tuombe Mungu, nitarudi na hii mada.
 
Back
Top Bottom