Rais Kikwete kwa hili sikusamehi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete kwa hili sikusamehi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ringo Edmund, May 1, 2011.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Rais umekuwa mwepesi kuliko marais wote niliowahi kuwasikia hapa duniani. Kwanza nijuavyo Rais ni kiongozi na kiongozi ni lazima akae mbele ili aliongoze kundi mahali pa kuelekea.

  Na kauli ya Rais najua ni ya mwisho, hatakiwi kukurupuka kuzungumza kwani ana washauri wa kutosha.

  Kauli za Kikwete zenye utata.

  1. Mimi ni mmoja wa wasiotaka DOWANS isilipwe, wewe kama rais unaungana na wananchi kulia nani wa kutusaidia?
  Je unataka tufunge na kuomba ili Mungu atuondolee DOWANS?

  Kwani ulikaa kimya muda mrefu tukawa tunakusubiri labda utatuokoa na hiki kikombe kichungu lakini kumbe na wewe huna msaada.

  2. Uzio uliojengwa jangwani ubomolewe, ulipotoa hilo agizo nikawa nasubiri utekelezaji, lakini wapi, halmashauri nimesikia imegoma.

  Sasa najiuliza je unajua uzito wa kauli yako kwa sasa kama rais na si kama Jakaya? Ni bora usiwe unazungumza rais wangu kwani sauti yako walio chini yako wameizoea mpaka sidhani kama wanakusikiliza tena.

  3.Sijui kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali zote zilizopo, hapo ndipo ulinichosha sana rais wangu. Uliomba kuwa rais wa Tanzania ili kiwe nini?

  Nakuombea umalize miaka yako minne iliyobaki kwa amani ili tujipange upya ila kwa hayo sikusamehi.
   
 2. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ringo nilidhani kuna mengine...kumbe haya tu! Binafsi huyu bwana kuingia madarakani 2005 nilipiga moyo konde...kwamba nchi itakaa likizo kwa miaka 10 na probably ndicho tunachokiona sasa!
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sikutegemea jipya kwa jk tangu awali kwa kuwa namfahamu ni mtu wa mizaha, kujionesha, umaarufu, na hana mtazamo anao upigania katika uongozi popote alipowahi shika.
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Huu urais wake ni wa Hisani...ni km mchezo wa bahati nasibu ambao mshindi hakutaraji afanyie nini ushindi huo
   
 5. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Duh! Ndg yangu umenizidishia machungu. Kila kukicha ninaposoma mada za namna hi nazidi kuchoka. Halafu kuna watu wanadhubutu kumtetetea. Eti kafanya mazuri. Unafiki mtupu na cfaham ni nani wa kutusaidia hili ikiwa kama kiongozi wetu hawezi. Sasa anafanya nini madaratjani? Anyway, tuzidi kuvumilia, ila mpaka lini. Ni nchi pee Afr Mash ambayo kila kitu kimepanda bei. Angalieni bei ya mafuta ilivyo juu. Watanzania wote tujipe pole kwa yote haya, hasa kwa kushindwa kusimamia kile anachosema. Na kushindwa kukemea mafisadi anaowalinda na kuwapigania!
   
 6. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Mjomba JK,hana mapya huyu.Ngoja amalize miaka yake akapumzike!
   
 7. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nchi ipo kwenye Autopilot
   
Loading...