Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.

nI KWELI kabisa, JK anafikiri jibu lilojibu shinikizo la walimu ndiyo hilo kwa drs, hapana hawa drs watakachofanya wanaweza kurudi kazini kwa shinikizo lake lakini kitakachofanyika ni kupunguza ratio hii 1:26,000 yaani dr mmoja kwa wagonjwa 26,000 na kuwa hata 1:2,000 na hakuna atakayeuliza lakini madhara yake tutayona pale mutuary na kwenye cemetaries
 
ni kweli mkuu, na kwa nini ni wazee tu, sisi vijana hayatuhusu?vijitu vyenyewe havina masikio vizuri, vinashangilia kabla hata ya point
 
Rais anatakiwa a-take action, action speak louder than words, sio kuongea na wazee. Wazee wenyewe ndio walio tufikisha hapa na kujiita nchi maskini, akiongea nao anategemea atapata ushauri gani toka kwao au changamoto gani toka kwa wazee!!! Mheshimiwa rais anawaogopa madaktari kwanini?? May be ana inferiority complex, na moja ya njia ya kukabiliana na hali hiyo aliyonayo ni kuongea na wazee. Kwa sababu wazee watamfanya ajisikie vizuri na watamtia moyo na kumfariji kwa kumshangilia na kumpa mkono.

Lakini inaweza kuongea na wazee ikawa sio suluhisho la tatizo, the best way to escape from a problem is to solve it. Na kutatua tatizo ni ku-take action, Rais anajua action ya kuchukua kama mkuu wa nchi. Maongezi ya leo na wazee yana sura mbili, kwanza yatamuongeazea challenge toka kwa wachambuzi mbalimbali kwa hiyo awe makini kwa atakacho ongea. Na kwa sura ya pili ni kwa upande wa madaktari, wamekosea kumpa amri mkuu na hiyo ndio itameza madai yao yote.

Madaktari hawakuwa makini wakati wa hitimisho lao la mgomo, wangetumia busara kidogo sio kutoa amri kwa rais(a good tongue is a good weapon). Kumbuka PM alipotoa amri kwa madaktari kilitokea nini? Kwa hilo mumempa mkulu point za kuongea na muonekane mna makosa, Haya tusubirie ataongea nini.

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][/FONT]
 
kama akichukua maamuzi kama haya tutegemee watu wengi kufa, coz udaktari sio uwalimu ni taaluma inayocheza na maisha ya watu na rohoo zao so atawashurutisha warudi lakini hawata fanya kazi kwa moyo
 
Tunawaomba Mods update za hicho kikao mruhusu kwenye thread nyingine mpya kabisa, hii ishajaa sana.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…