Rais Kikwete kuhutubia Taifa Jumapili

Rais Kikwete kuhutubia Taifa Jumapili

Kwa vile JK ni Rais wa nchi, ni wazi kuwa ana haki ya kuongea na mtu yeyote na mahala popote

Du unavyomtetea jk, kwani akiutubia taifa bila kuingia gharama ya kuwaleta wanaoitwa wazee hatutamsikia? Au mpaka vigelegele, shangwe, vifijo na nderemo za wazee ndiyo hotuba inanoga
 
Kwani hujasikia kauli ya chama tawala kupia kwa Nape NNaye? Mwenyekiti anakuja kuongelea mambo mengine ya nchi kama maendeleo ya miradi mbalimbali kama barabara, Miradi ya Gesi. katiba atatoa ufafanuzi kidogo sana kwa sababu kauli imeshatolewa.
 
Jakaya-August26-2014.jpg

Rais Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete anatarajia kufanya ziara mkoani hapa ambako atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya barabara, maji na kulihutubia Taifa kwa kuongea na wazee.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, alisema Rais ataanza ziara mwishoni mwa wiki hii kulihutubia Taifa mwishoni mwa mwezi huu Jumapili ijayo.

Kwa mujibu wa Nchimbi, Rais Kikwete ataanza ziara yake katika wilaya ya Kongwa ambako ataweka mawe ya msingi na kufungua miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Akiwa wilayani Kongwa, atapokea madawati kutoka shirika la misheni na kuyakabidhi katika shule ya msingi.

Kisha atafanya mkutano wa hadhara Kibaigwa wilayani humo, kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mbandee-Kongwa inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 14.

Siku itakayofuata Rais Kikwete atafungua mradi wa maji katika wilaya ya Mpwapwa mradi ambao unahudumia wakazi wa kijiji cha Chunyu, kuweka jiwe la msingi katika daraja la Gulwe na kuzungumza na wananchi.

“Rais kwa mara ya kwanza atahutubia Taifa akiwa mkoani Dodoma siku ya Agosti 31 na katika Wilaya ya Dodoma mjini, atakuwa na siku mbili katika siku ya kwanza atazungumza na wazee wa Dodoma jioni,” alisema Dk. Nchimbi

Alisema Rais pia, atafungua mradi wa makazi ya Mkuu wa wilaya ya Chemba na ofisi yake katika wilaya ya Chemba na pia katika wilaya ya Kondoa ataweka jiwe la msingi katika barabara ya Mayamamaya-Kondoa, kuzindua ukumbi wa mikutano wa halmashauri na kuongea na wananchi.

Aidha alisema katika wilaya ya Dodoma mjini Rais Kikwete atafanya ziara ya siku mbili ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa kuboresha huduma za maji manispaa ya Dodoma na katika wilaya ya Chamwino na Bahi na kwamba vile vile, atafanya shughuli mbalimbali za uzinduzi.

CHANZO: NIPASHE

Mkulu anataka ku pre-empt Ukawa
 
Huyu Kikwete anaboa tu. Natumai kutakuwa na mechi nzuri la premier league siku ya jumapili wakati anahutubia. It is worthy hundred times watching football match, than listening to his useless blah blah.
 
taahira kama wewe huwezi ona maana ya hotuba za rais. nenda tu kanywe vitochi tu vinakutosha.

bora hotuba za DR SLAA kuliko za jk ni kuambiawa na wassira hakuna jipya ccm ni janga la taifa
 
bora hotuba za DR SLAA kuliko za jk ni kuambiawa na wassira hakuna jipya ccm ni janga la taifa
unaongelea slaa yupi? yule kibabu aliyewahi kukana kuwepo kwa kipengele cha ukomo wa uongozi chadema? au yule aliyesema kuna container la kura limeshikwa mbeya? u r not serious.
 
Huyu Kikwete anaboa tu. Natumai kutakuwa na mechi nzuri la premier league siku ya jumapili wakati anahutubia. It is worthy hundred times watching football match, than listening to his useless blah blah.
Dah
 
Back
Top Bottom