Rais Kikwete kuhutubia Taifa Jumapili

Rais Kikwete kuhutubia Taifa Jumapili

Makamba angalau alikuwa anamtayarishia hotuba nzuri kiasi lakini aliyeposasa hivi mh? Na sijui anapotayarishiwa hizo hotuba huwa hazipitii kwanza kabla ya kuzirusha hewani maana zingine ni uharo kama ya mwezi uliopita!! anyway ngoja tusubiri.
 
Atakutana nao Singida. Safai hii hatawapeleka Ikulu

Mkuu acha utani! Hata kama ni Singida angeanza nalo basi kwani ni la maslahi mapana kitaifa?!

Kuzindua miradi angetuma tu wasaidizi wake kama ingebidi!
 
Mwezi huu si alikuwa Marekani? Tegemea kama kawaida hotuba yake ijikite zaidi katika kuelezea jinsi alivyofurahia safari yake ya Marekani na jinsi Obama alivyofurahi kumuona zaidi ya kuzungumzia mambo makubwa yanayolikabili kitaifa!
 
Kwa vile JK ni Rais wa nchi, ni wazi kuwa ana haki ya kuongea na mtu yeyote na mahala popote

Hivi wazee anaongea nao, anakutana nao au ni kutafuta washangiliaji? Kwa uzoefu wangu huwa naona rais anaongea akimaliza anasepa. Wale wazee ni kama live wallpaper. Tuseme hivi: Rais anahutubia Taifa mbele ya wazee
 
Jakaya-Kikwete-na.jpg

Taarifa ambazo mtandao wetu umepata kutoka Serikalini ni Kwamba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete atahutubia Taifa August 31,2014 akiwa mkoani Dodoma. Taarifa hizo zimeeleza kuwa Rais atahutubia Taifa wakati akiongea na wazee wa mkoa wa Dodoma.

Taarifa hizo hazielezi hasa Rais ataongelea mambo gani yanayogusa Taifa kwa sasa, ingawa kwa hakika kila mmoja anatambua kuwa hivi sasa suala kubwa ni mkanganyiko juu ya hatma ya mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania.

Taarifa ambazo mtandao wa harakatinews.com umepata kutoka Serikalini ni Kwamba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete atahutubia Taifa August 31,2014 akiwa mkoani Dodoma. Taarifa hizo zimeeleza kuwa Rais atahutubia Taifa wakati akiongea na wazee wa mkoa wa Dodoma.

Taarifa hizo hazielezi hasa Rais ataongelea mambo gani yanayogusa Taifa kwa sasa, ingawa kwa hakika kila mmoja anatambua kuwa hivi sasa suala kubwa ni mkanganyiko juu ya hatma ya mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania.

Hivi sasa Mchakato wa Katiba unaendelea kupitia Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma ingawa kukiwa na sitofahamu juu ya mchakato huo.Bunge hilo linaendelea huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau wanaotaka bunge hilo livunjwe.

Wanalalamika kuwa suala la maridhiano halipewi nafasi maana wakati CCM na baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 wakiendelea na mchakato wenzao wa vyma vya upinzani wanojiita 'umoja wa Katiba ya wananchi ' UKAWA wapo nje baada ya kususia mchakato huo.
Pia bunge hilo linadaiwa kuchakachua maoni yaliyopendekezwa na wananchi katika rasimu ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge hilo na Jaji Joseph Warioba.

Aidha inadaiwa kuwa asilimia kubwa ya maoni ya wananchi yametupwa na juzi zimesikika habari kupitia vyombo vya habari ya Tanzania kuwa mwenyekiti wa Bunge hilo Samuel Sitta ameanza kukusanya upya maoni ya wananchi.

Katika mazingira haya ndipo tunatoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kusikia malalamiko haya na kuchukua maamuzi yatakayoliepusha Taifa kuingia katika machafuko yasiyo ya Msingi kama amabyo baadhi ya nchi zilivyoweza kutumbukia katika machafuko baada ya michakato ya Katiba kuvurugwa na wachache katika nchi zao.

Sisi wa Mtandao wa HARAKATINEWS BLOG tunachukua fursa hii kumuomba rais Kikwete kupitia hotuba yake kutoa mwelekeo mpya bila kutazama maslahi ya wanasiasa.

Tunaamini kuwa Hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa mwezi huu wa Agust ndiyo kimbilio la mwisho kwa watanzania kuona wanaendelea na mchakato 'ulioboreshwa' wa Katiba mpya.

Kwako Rais Kikwete,Chukua hatua,okoa Taifa kupitia hotuba yako.

Mhariri Mtendaji
www.Harakatinews.com
August 29,2014

Chanzo:HARAKATINEWS BLOG: Mhariri-Hotuba ya Rais Kikwete ya Mwezi August inusuru mchakato Katiba mpya
 
Hivi wazee anaongea nao, anakutana nao au ni kutafuta washangiliaji? Kwa uzoefu wangu huwa naona rais anaongea akimaliza anasepa. Wale wazee ni kama live wallpaper. Tuseme hivi: Rais anahutubia Taifa mbele ya wazee
Subiri utakuwa mzee na wewe utapata bahati , kupitia wewe Rais atahutubia
 
Mwezi huu si alikuwa Marekani? Tegemea kama kawaida hotuba yake ijikite zaidi katika kuelezea jinsi alivyofurahia safari yake ya Marekani na jinsi Obama alivyofurahi kumuona zaidi ya kuzungumzia mambo makubwa yanayolikabili kitaifa!
Haya shekhe kunduno ngoja tusuubiri tuone utabiri wako
 
Ni kweli...hizo safari zisizo na tija kwa taifa za kila siku sio kazi ndogo..jamaa ni jembe sijapata kuona
Wewe ni kiumbe kidogo sana, huwezi kujua umuhimu wa ziara za kikwete, subiri tu uletewe nyumbani ule kula kulala wewe
 
Mkuu acha utani! Hata kama ni Singida angeanza nalo basi kwani ni la maslahi mapana kitaifa?!

Kuzindua miradi angetuma tu wasaidizi wake kama ingebidi!
JK anajua vijana wake wanapiga kazi Dom hana tatizo na hilo, Ukawa kama wanaona wanachelewa wanaweza kutangulia
 
Back
Top Bottom