Rais Kikwete karuhusu kampeni Urais CCM?

Rais Kikwete karuhusu kampeni Urais CCM?

"Nilipata bahati ya kufanya kazi Zanzibar. Kuna wakati Mzee Thabit Kombo aliniambia wakati ukifika jambo unalolitaka litakuwa hata watu wapinge na kama wakati bado hata ufanyeje halitakuwa. Mimi niligombea 1995, wakati ulikuwa bado halikuwa lakini 2005 wakati ulikuwa sahihi likawa. Kwa hiyo nawewe January lisipokuwa safari hii usiweke nongwa ila amini wakati bado"
Rais Kikwete - Soni Bumburi
9 July 2014
Source: Mkuu wa wilaya korogwe (Mh. Mrisho Gambo - Facebook page)

Kuna mzee alinitonya eti mwaka 1985 Thabiti Kombo ndiye aliyemkwamisha Salim Ahmed Salim pale JK Nyerere alipokuwa anataka awe mrithi wake wakati katiba ilikuwa haimruhusu Salim kutokana na umri Nyerere alizuga kumteua Mwinyi ili wakifika kwenye kikao mbele ya wajimbe jina lake likitajwa Mwinyi akatae ili dhamira ya Mwalim itimie. Thabiti Kombo akamfuata Mwinyi akamwambia isiwe mjinga wewe ukitajwa ukubali mzee ruksa jina lake lilipotajwa naye akakubali uteuzi we Nyerere hakuamini jinsi alivyoliwa chenga.
 
Wewe ulitaka aseme nini sasa hebu tuambie wewe unataka aseme nini.

Kwani magamba hakuna vikao vya chama? Kila mtu anakurupuka tuu...kuutaka urais.. nilitaja kikwete kama mwenyekiti wa magamba. ..aitishe kikao waonyane kwa vikao si kila mtu kupayuka payuka tuu...hivi magamba mkoje lakini?
 
Hivi mnavyomuita kikwete Dr, hiyo PHD aliipata lini? Na wapi? Hata kuongea English hawezi..hebu magamba acheni siasa..muiteni rais kikwete yatosha!
 
Akiwa Lushoto leo Rais Jakaya Kikwete amemuasa january makamba awe na subira katika kugombea Urais na asipopata nafasi ,akubali tu matokeo. Kwa hiyo nawewe January lisipokuwa safari hii usiweke nongwa ila amini wakati bado".
Haya ni manejo ya busara sana na ni kwa wasiojua tuu ndio watashangaa.

Alichokuwa anakifanya "pace maker" is is just to make the paces, ili mkimbiaji tarajiwa apite kwa ulaini!, JK amempa angalizo zuri dana kijana kwa sababu JK anamjua "mwenye zamu yake!".

Siku zote nasisitiza humu, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!. Kwa ushauri huu, JK ameonyesha busara za hali ya juu!.

Anamjua mwenye zamu yake!, hivyo ni busara kumshauri kijana asubirie!

Pasco
 
Wewe ulitaka aseme nini sasa hebu tuambie wewe unataka aseme nini.
Inaonekana wewe aidha siasa huzijui au ni ushabiki kama wa simba na yanga. Katika kampeni karipio ni kampeni tosha. Hapo kampigia kampeni ya kufa mtu. Katika hali ya kawaida, kama Rais na Mwenye Chama, alitakiwa kunyamaza tu. Naomba nijieleze, katika kampeni ukifanya rafu na ukapata karipio hapo unapanda chati kwani kila mtu atauliza huyo ni nani na hapo chati yako inapanda. Kumbuka mabaya ya mtu huwa ndiyo gumzo kuliko mazuri. Binadamu akiumwa na mbwa siyo habari ila binadamu akimng'ata mbwa ni bonge ya stori. Nadhani umenipatapata
 
Hivi mnavyomuita kikwete Dr, hiyo PHD aliipata lini? Na wapi? Hata kuongea English hawezi..hebu magamba acheni siasa..muiteni rais kikwete yatosha!

Kuongea English si kipimo cha Usomi ! Kuna wale wazaliwa wa London wanazungumza Kingereza kizuri na wengine hawajaenda shule, kuna wasomi wafaransa,wachina,wa-Rusia,wa-Italy ,Spain , na German wana Phd na English hawajui .
 
Inaonekana wewe aidha siasa huzijui au ni ushabiki kama wa simba na yanga. Katika kampeni karipio ni kampeni tosha. Hapo kampigia kampeni ya kufa mtu. Katika hali ya kawaida, kama Rais na Mwenye Chama, alitakiwa kunyamaza tu. Naomba nijieleze, katika kampeni ukifanya rafu na ukapata karipio hapo unapanda chati kwani kila mtu atauliza huyo ni nani na hapo chati yako inapanda. Kumbuka mabaya ya mtu huwa ndiyo gumzo kuliko mazuri. Binadamu akiumwa na mbwa siyo habari ila binadamu akimng'ata mbwa ni bonge ya stori. Nadhani umenipatapata

Kama ilivyo vigumu kwa Serikali kuhamia Dodoma,kumaliza foleni jijini Dsm,kutokomeza ujangiri,Ufisadi,wanywa Gongo,wavuta Bangi nk . Ndivyo hivyo hivyo ilivyo vigumu kwa January Makamba Kuwa Rais wa Tanzania . Hata ukitokea akapenya na kuteuliwa Kuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM atapata shida sana kwenye kampeni kwani afahamiki huku mikoani kwetu japo Ruge atajitahidi kumtangaza kwenye Radio yake,kisha kugawa,kanga,tshart,kofia lakini atambue mwisho wa siku kura ni ya Siri na anaweza akawa Daraja la Upinzani kuingia ikulu na Kuwa Kama Kenya Chama cha KANU kilivyogeuzwa Kuwa chama cha upinzani pasipo kutarajia.
 
Urais wa Tanzania sasa umekuwa ni Dili kwa Madalali wa Siasa ,wapo busy kula pesa za kila anayeonesha nia ya kutaka kuja kuishi ikulu ya Magogoni na kuonja Harufu ya Samaki wa Feli,Madalali wa siasa huu ni mda wao wa Mavuno hasa wale ndumila kuwili ambao hupenya kote kote kuomba pesa kwa wagombea, Wakazi wa jijini Dsm wao kero Yao ni Foleni za Magari wao wanamtaka Rais atakayehamia Dodoma ili alinisulu jiji na adha ya mfoleni mda wote,huku mikoani tunataka barabara,maji,madawati,Hosptal bora , huduma zote muhimu za jamii ,tunamtaka Rais ambaye atatekeleza ahadi zake kwa vitendo.
 
Kama ilivyo vigumu kwa Serikali kuhamia Dodoma,kumaliza foleni jijini Dsm,kutokomeza ujangiri,Ufisadi,wanywa Gongo,wavuta Bangi nk . Ndivyo hivyo hivyo ilivyo vigumu kwa January Makamba Kuwa Rais wa Tanzania . Hata ukitokea akapenya na kuteuliwa Kuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM atapata shida sana kwenye kampeni kwani afahamiki huku mikoani kwetu japo Ruge atajitahidi kumtangaza kwenye Radio yake,kisha kugawa,kanga,tshart,kofia lakini atambue mwisho wa siku kura ni ya Siri na anaweza akawa Daraja la Upinzani kuingia ikulu na Kuwa Kama Kenya Chama cha KANU kilivyogeuzwa Kuwa chama cha upinzani pasipo kutarajia.
Pamoja na mimi kuwa CHADEMA damu, hawa CCM huwezi kuwaunderrate hata siku moja. Kumbuka mtu aliyeua umaarufu wa CDM ni Mbowe kukataa kuachia madaraka. Kwa hali ilivyo nina wasiwasi hakuna mabadiliko mwaka 2015. Huyu January nahisi, narudia nahisi kuwa amewekwa ili kumdhoofisha mtu. Ametumwa huyu ili kambi fulani ipoteze wapenzi. Je, si alileta Wamarekani wakakataliwa na ikawa nongwa? Wait and see MKUU
 
Wewe ulitaka aseme nini sasa hebu tuambie wewe unataka aseme nini.

Ilibidi AMKEMEE wazi wazi kuwa aache kutangaza nia mapema kabla CCM haijaruhusu!

Badala yake kama sasa anampa go ahead aendelee na harakati zake
 
Back
Top Bottom