Rais Kikwete ateua makamishna wa Magereza - Oktoba 01, 2012

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza na maafisa wengine.

Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo amesema Rais amemteua Bwana John Casmir Minja kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kuwateua wengine kuwa maofisa kama ifuatavyo:

  • Dkt. Juma Ally Malewa ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na Uendelezaji wa Magereza.
  • Bwana Deonice Lwamahe Chamulesile ameteuliwa kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji.
  • Bwana Gaston Sanga ameteuliwa kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.
Wengine ni:

  • Bwana Fidelis M. Mboya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo kabla ya uteuzi huu Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza na;
  • Bwana James B. Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine.
Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 1, 2012 mjini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huu umeanza tangu tarehe 25 Septemba, 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012
 
Na yule kamshina aliekuwepo nae kaenda wapi ama ameshindwa kutekeleza ilani, mbona pia hatujaambiwa hao wateule wa juu wanne walikuwa na vyeo gani kabla ya kuula
 
Hizi ndiyo habarinusu nusu; hili jeshi lilikuwa na Kamishna wa magereza kabla ya huyu aliyeteuliwa? Na hizo idara ambazo zimepatiwa wakuu wapya ni idara mpya na hawa ni wakuu wake wa kwanza?
 
Hizi ndiyo habarinusu nusu; hili jeshi lilikuwa na Kamishna wa magereza kabla ya huyu aliyeteuliwa? Na hizo idara ambazo zimepatiwa wakuu wapya ni idara mpya na hawa ni wakuu wake wa kwanza?

Kamishna mkuu (Nanyaro) alistaafu tangu 30/09/2012 na tangu wakati huo Bw. mboya amekuwa akikaimu nafasi hiyo. Hata hilo jeshi bado lina safari ndefu kwani walioteuliwa sio wabunifu na wengi wao wana kashfa za matumizi mabaya ya rasilimali na madraraka
 
Hiyo ndo kazi kubwa ya Raisi wetu, kusafiri na kuteua! Bg up sana!!!
 
Hizi ndiyo habarinusu nusu; hili jeshi lilikuwa na Kamishna wa magereza kabla ya huyu aliyeteuliwa? Na hizo idara ambazo zimepatiwa wakuu wapya ni idara mpya na hawa ni wakuu wake wa kwanza?

Mkuu nakubaliana na wewe 100%. Maana tunawekewa taarifa halafu tutafute majibu
 
Kuteua na kusafiri(kutembeza bakuli)...nimewahi sikia kuwa JK ana akili nyingi sana za uendeshaji wa serikali!wanasema anajua sana systems machines...na kujua kuchezesha....mambo!!sasa nashangaa sana nchi imemshinda
 
Na huyo john minja nani anajua undani wake ktk utendaji atuwekee hapa cv yake.
 
Back
Top Bottom