Rais Kikwete ateua bodi mpya ya TANESCO

Rais Kikwete ateua bodi mpya ya TANESCO

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,030
Reaction score
59,682
Mwenyekiti ni Mboma....
je kutakuwa na mabadiliko yoyote? au kama jana tu

..........................................................................................................................................................................................................................
TAARIFA KWA UMMA

YAH: UTEUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)



Napenda kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.


Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-


1. Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3. Bw. Leonard R. Masanja
4. Bw. Vintan W. Mbiro
5. Bw. Beatus P. Segeja
6. Bw. Hassan Ally Mbaruk
7. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8. Bw. Abdul Ibrahim Kitula


Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

............................................................................................................................................................
Anawaweka sawa ili Dowans wajilipe bila mkwaruzo.

 
Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-
Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
  1. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
  2. Bw. Leonard R. Masanja
  3. Bw. Vintan W. Mbiro
  4. Bw. Beatus P. Segeja
  5. Bw. Hassan Ally Mbaruk
  6. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
  7. Bw. Abdul Ibrahim Kitula
[/LEFT]
 
..huyo Mwambalaswa siyo yule mwenye kampuni ya umeme akiwa na ubia na Dr.Mwakyembe?

.
 
Mboma tena du, nchi hii, halafu mbona wabunge bado wanachaguliwa kwenye bodi za mashirika, watayasimamia vipi hawa?
Ufisadi mwingine JWTZ: Mboma, Mkapa, Apson wanajua!

Nimevujishiwa habari kuwa kuna Ufisadi mkubwa ulifanyika ndani ya Jeshi letu lenye heshima la JWTZ. Ufisadi huo ulifanyika mwaka 2006 pale JWTZ ilpouziwa ndege na helkopta zilizochakaa wakati malipo yaliyofanyika ni kwa ndege mpya!

Habari zinasema kuwa ile Helokopta ya Agusta iliyotengenezwa Italia na iliyoanguka Arusha mwaka jana 2008 na kuuwa watu wanne akiwamo mpiganaji mwaminifu ambaye alikuwa Rubani ilikuwa ni chakavu! Helkopta hiyo ni miongoni mwa nyingine za aina hiyo zilzonunuliwa Italia kwa bei kubwa iliyopaishwa (kama kwenye ununuzi wa Rada!). Inasemekana kuwa Seikali iliunda tume ya kuchunguza ununuzi wa ndege helkopta hizo na Mhandisi wa Kiitaliano aliyekiri kuwa helkopta hizo ziliuzwa zikiwa zimechakaa baadaye alikutwa amekufa hotelini!

Nimefahamishwa kuwa kuna ndege nyingine ya kijeshi yenye uwezo wa kubeba tani 90 ilinunuliwa wakati huo huo. Dege hilo la kizamani ajabu lenye kuendeshwa na marubani watano (5 pilots)! lilinunuliwa na JWTZ baada ya nchi za Malawi na Namibia awali kukataa kulinunua!

Delas zote hizo zilifanyika wakati wa Utawala wa awamu ya pili ya Mkapa! Kilicho wazi ni kuwa Mkapa, Colnel Apson (Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wakati hu) na Mkuu wa Majeshi wakati huo Jenerali Mbona wanaufahamu fika ufisadi huo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa baada ya Ufisadi huo kubainika zaidi ya shahidi muhimu kukutwa amekufa hotelini!
 
Ingekuwa vyema angewapa Jeshi waendeshe TANESCO maana hawa ndugu zetu wa uraiani wameshindwa kabisa.

Nakubaliana na wewe 100% Bora Fisadi Kikwete akaikabidhi na Nchi Jeshini vilevile sio Tanesco pekee, Madudu yanayoendelea katika nchi hii bora Wakina Shimbo waimalize, wameshindwa kuilinda nchi wataweza kuiongoza? Ingawa wapo Wengi Serikali lakini hawana hata maana yoyote hao wanajeshi zaidi ya Kuendeleza Ufisadi kama alivyo Kikwete.

Jeshi la Tanzania lipo kwa ajili ya kulinda Ufisadi sio kutetea taifa
 
Jeshi la Tanzania ni lakifisadi halina maadili kwa Watanzania, Jeshi letu limegeuzwa kuwa kitengo cha kukwapua kodi zetu. CCM mnatuharibia nchi yetu kila sehemu, tumewakoseeni nini sisi Watanzania? au Upole wetu ndio mtaji wenu?
 
Back
Top Bottom